Mshikawezi Mwizi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2013
- 751
- 375
Mheshimiwa Rais tunazitambua vema jitihada zako za kulipeleka Taifa kule ulikokusudia na kunakostahili. Mh. Rais wapo watendaji ambao bado wanapingana na jitihada zako, mfano mzuri ni wafanyakazi wa Tanesco Morogoro mjini. Wiki iliyopita siku ya jumatatu walifanya zoezi la kubadilisha mita za umeme za zamani katika baadhi ya maeneo na kuweka mita za luku. Zoezi hili lilienda vizuri japo ilipofika jioni siku hiyo ya jumatatu nyumba nyingi zilizofungiwa mita hizo za luku zilikumbwa na tatizo la kukatika kwa umeme. Kila aliyepatwa na tatizo hili alifika siku ya jumanne katika ofisi za Tanesco kutoa taarifa. Walichukua details na kuahidi kurudi kushughulikia tatizo , cha ajabu leo jumamosi lakini bado hawajafika maeneo hayo. Watu wengi wanakosa nishati hii ya umeme kwa uzembe wao. Tunaomba mamlaka husika ziwashughulikie kupitia shinikizo lako mtaalamu wa kutumbua majipu.