Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, ameungana na Watanzania wengine katika zoezi la kuboresha taarifa za Mpiga Kura kwa mwaka 2025, ambapo leo ameboresha taarifa zake katika shule ya Amani Gomvu, iliyopo Mtaa wa Minondo, Kata ya Somangila, wilayani Kigamboni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Hersi ameandika: "Leo nimejumuika na Watanzania wenzangu wa Kigamboni kuboresha taarifa zangu za Mpiga kura. Zoezi hili lilifanyika katika shule ya Amani Gomvu, Mtaa Minondo, Kata ya Somangila, wilaya ya KIGAMBONI."
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la Mpiga Kura ili waweze kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa miaka mitano ijayo.
Hersi alihitimisha kwa kusema: "Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Kigamboni."