πππππππππ πΌππππΌπ ππΌππππ
Alipoulizwa kama aliweka mali zake chini ya uthibiti wa mama yake kwaajili ya Ndoa:
Hakimi alisema:
"Hapana! Hii haina uhusiano wowote na ndoa, kwa sababu kama ilivyosemwa ilikuwa hivyo tangu utoto. Ukiwa na umri chini ya miaka 18 huwezi kutumia akaunti yako ya benki. Kwa hivyo mama yangu alidhibiti kila kitu na kwa sababu kila kitu kilikuwa kizuri.....tuliacha mambo kama yalivyokuwa, haswa wakati mafanikio yangu yalipoongezeka.
Alidhibiti kila kitu na tulikuwa tukimwambia kila kitu."
"Ukweli ni kwamba tangu nikiwa mdogo, nilipata pesa nyingi sana kutokana na soka... lakini sikuweza kumudu. Kwa hiyo mama yangu alisimamia yote hayo.
Kwa hiyo, nilijifunza kutoka kwake jinsi ninavyoweza kusimamia mambo haya. Sikuzote mimi huchukua maoni yake kuhusu pesa ninaponunua nyumba au gari au ninapopata pesa nyingi. Na ndio maana pia tuliamua kwamba hatarudi kazini alikokuwa akifanya kazi. Yeye ndiye atakuwa msimamizi wa kila jambo."
"Nadhani hilo ni jambo zuri, kwa sababu mwishowe, unapokuwa na pesa au umaarufu, unaweza kuamini watu wachache tu. Na nadhani mama yako ndiye mtu pekee anayekupenda kwa dhati, iwe una pesa au huna
Na nadhani ukiwa na pesa mama yako atakuwekea akiba ili uwe na pesa hizi kila wakati...na pia nadhani hatajaribu kukuibia! Kwa sababu hicho ni kitu ambacho nyote wawili mlipata pamoja. Kitaalam pesa yako ni yake kwani wakati anafanya kazi na kupata pesa alikupa kutoka kwa pesa hiyo na hadi dakika hii mama ananitakia mema. Yeye kamwe hatatamani ubaya juu yangu au juu ya ndugu zangu au familia kwa hivyo yeye ndiye mtu ninayeweza kumwamini na anaweza kunisaidia badala ya ndugu zangu."
Kuhusu Ndoa Iliyopita:
"Imenifundisha kujipenda zaidi, kujijali zaidi na kuwajali watu wanaonizunguka.
Unapokuwa kwenye uhusiano, unavumilia mambo mengi ambayo huwezi kuvumilia na watu wengine. Nilijifunza hilo peke yangu. Nilipofunga ndoa, nilivumilia mambo mengi ambayo sitayavumilia sasa..na nikajiuliza, kwa nini nilivumilia mambo haya?"
"Ile ndoa ilinifundisha mengi na kunifanya kuwa na nguvu zaidi, na pia ilinifanya kujua ninachotaka. Na sasa najua kwamba nikiingia kwenye uhusiano naweza kulishughulikia vizuri sana!"
Alipoulizwa kama ataoa tena, Hakimi alicheka kabla ya kujibu:
"Watu wengi wanasubiri hii! Kwa kweli, sijui! Sipingani na hili hata hivyo mimi bado ni mdogo. I'm SINGLE and OPEN, na ninajisikia vizuri. Ninafurahia wakati wangu na familia yangu, na mimi mwenyewe. Ni ngumu kupata mtu sahihi! Lakini nikikutana na mtu sahihi, why not?"
Follow Wagulimba OG