Rais wa Uturuki awasili akiambatana na ujumbe wa watu 150 kwa ziara ya siku mbili

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Rais wa Uturuki, Recep Erdogan na mkewe wamewasili nchini kwa ziara ya siku mbili, wamepokelewa na Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais Magufuli.

Aidha kiongozi huyo aliyenusurika kupinduliwa mwaka jana ameambatana na ujumbe wa watu 150.

=======
RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak
.
Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wa nchi hiyo.
 
Mleta uzi huyo rais kuja na watu 150 ni kitu cha kawaida ila hatuoni mabadiliko ya maana kwenye maisha yetu. Alikuja rais wa China na watu kibao, Akaja Obama na watu kibao, akaja mfalme wa Morocco na watu wa kumwaga. Lakini huku nyuma bado tunapambana umeme upande ama usipande. Polisi ndio wanatangaza mapato yao na wala sio TRA!!
 
Mkuu hizi ziara zinawanufaisha wachache sana
 
Kwa magufuli kila goti litapigwa.

Wanasaga nauli kutoka kote duniani kuja kutubu na kuimba hapa kazi Tu
Naskia ameshindwa kwenda kumpokea baada ya mkarimani kukosekana....

Wenzio wanapitisha ajenda zao za maendeleo ndio maana kaja na wafanyabiashara 150, nyie endeleeni na English course
 
Kwa magufuli kila goti litapigwa.

Wanasaga nauli kutoka kote duniani kuja kutubu na kuimba hapa kazi Tu

Ndio unavyojidanganya hivyo wewe unadhani wamekuja kushangaa bahari hapo, hawa wamekuja kuchukua fursa zao. Kaa chini angalia tokea wavietnam, india na wengine waliokuja nani kanufaika sana??? Sie tunafanya siasa kwenye mambo ya msingi mwisho wa siku kupayuka kama vichaa tunanyonywa na mataifa mageni kumbe hatujiandai vizuri tunakuwepo kwenye meza ya mazungumzo tunaishia kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
 
Back
Top Bottom