Rais wa TP MAZEMBE kuwania urais DRC

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Kutoka kuwa rais wa klabu maarufu katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo TP Mazembe, bwana Moise Katumbi sasa anataka kuwa rais wa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati.

Bwenyenye huyo maarufu, ni mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu unaoratibiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Katumbi ambaye amewahi kuwa gavana wa jimbo tajiri zaidi nchini humo la Katanga alijiuzulu na kumshtumu rais Kabila kwa uongozi duni.

[http://ichef]Image captionMoise Katumbi kama rais wa TP Mazembe na gavana wa katanga

Sawia na viongozi wengine wa upinzani Katumbi amemsihi mshirika wake wa zamani rais Joseph Kabila, kutokiuka katiba ya nchi hiyo kwa kuacha madaraka wakati muhula wake wa pili utakapomalizika Desemba mwaka huu.

''Jambo la muhimu kwa wakati huu, sio kuwa rais, jambo muhimu kwetu ni katiba iheshimiwa, na mamlaka ya nchi ikabithiwe kwa mshindi kwa njia ya amani nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, na pia kalenda ya uchaguzi kuheshimiwa, na pia kuunganisha upinzani''.

''Nafahamu raia wa nchi hiii wanamatarajio makubwa kutoka kwangu, na sasa tutaketi ili kumchagua mmoja ambaye atakuwa mgombea wa pekee wa upinzani'' alisema bwana Katumbi.

Moise Katumbi ni kiongozi wa pekee wa upinzani nchini Congo ambaye anaushawishi mkubwa na ufuasi mkubwa miongoni mwa raia wa Congo na anayetarajiwa kuumpa rais Kabila ushindani mkali endapo atawania tena.

Haijabainika ikiwa viongozi wa upinzani wataungana na kumteua kuwa mgombea wa pekee.

1457434477633.jpg
Mashabiki wa TP Mazembe

Lakini baadhi ya wakosoaji wamehoji utawala wake wakati alipokuwa gavana.

Katumbi anashukiwa kutumia mamlaka yake ya kisiasa kujinufaisha kiuchumi.

Donat Ben Bella Mpiana ni afisa wa shirika la kutetea haki za kibinadam nchini Congo...''kuna kampuni ambazo zimekuwa zikifadhili TP Mazembe kwa hali na mali.''

''Lakini siwezi kusema au kuthibitisha ikiwa alitumia ushawishi wake au la kuyashurutisha kampuni hizo kufadhili klabu hiyo, ili nazo zipewe ruzuku na serikali ya jimbo hilo''

Kampuni ya kimataifa ya kuchimba madini, imesemekana kulipa zaidi ya dola milioni mbili klabu hiyo ya TP mazembe, kama sehemu ya jukumu lake la kuwekeza katika jamii.

''Hii ni mbali na ufadhili zaidi kwa timu hiyo, ufadhili ambao haujatangazwa rasmi'' aliongezea Mpiana.

Lakini Katumbi amekanusha madai hayo ya kutumia mamlaka yake vibaya.

Wafuasi wa TP Mazembe na Moise Katumbi

''madai haya hayana msingi wowote na hayana adhari yoyote kwa umaarufu wangu, mimi sijawai kuchanganya siasa na biashara, mimi mimetoka kwa familia ambayo ilikuwa ikifanya biashara na mimi moja kwa moja nikaanza kufanya biashara.

Kama ningelikuwa mfisadi watu hawange niunga mkono''

Kwa watu wengi, kuna thibitisho kuwa Katumbi alitumia mamlaka yake kuendeleza miradi ya maendeleo.

Ufanisi wa klabu yake ya TP Mazembe, kampuni zake na miundo mbinu aliyoweka katika mkoa wa katanga wakati wa utawala wake, ni baadhi ya masuala yanayomuweka katika nafasi nzuri kama mgombea wa kiti cha urais kuliko wanasiasa wengine wa upinzani.

Na muda mfupi baada ya TP Mazembe kushinda kombe la Supercup, mamia ya raia wa Congo walijitokeza barabarani mjini Lubumbashi wakimsifu bwana Moise Katumbi.
 
Back
Top Bottom