Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,796
Waheshimiwa wananchi wa Tanzania. Nimesikia taarifa za kuvamiwa kwa kituo cha habari cha Clouds Media.
Mkuu wa Mkoa katika nchi yetu sio kamanda wa kikosi chochote cha jeshi lolote lililoanzishwa kwa mujibu wa sheria.
Mamlaka aliyo nayo kwa mujibu wa sheria za nchi yetu hayajumuishi kuamrisha askari jeshi au polisi au usalama wa taifa kuvamia makazi au sehemu za biashara za watu.
Mkuu huyu wa mkoa hastahili kuendelea kwenye madaraka hayo kwa siku moja zaidi. Hana tena sifa wala maadili wala sababu za kuendelea kuwa kiongozi wa umma.
Namshauri Rais Magufuli atengue uteuzi wake haraka iwezekanavyo kabla hajachafua zaidi taswira ya serikali na ya Rais Magufuli mwenyewe.
Aidha, namshauri Rais Magufuli amchukulie hatua stahiki kamanda au mkuu wa kikosi chochote cha Jeshi lolote aliyeruhusu askari wake kutumiwa na Paul Makonda kwa namna iliyoripotiwa.
Tundu Antiphas Lissu, Rais, Chama cha Mawakili wa Tanganyika.