Rais wa Sudani Omar al Bashir achaguliwa tena kuwa rais

Rais wa Sudani Omar al Bashir achaguliwa tena kuwa rais

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,943
Reaction score
63,709
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Sudan NEC imetangaza kuwa, rais Omar al-Bashir amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo baada ya kupata asilimia 94.5 ya kura zote.

Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume Mukhtar al-Asam amesema, Al-Bashir amefuatiwa na mgombea urais wa Chama cha Federal Truth, Fadl Elsid Shuaib aliyepata asilimia 1.43 ya kura zote.

Al-Bashir alishindana na wagombea wengine 15, ambao baadhi yao wanawakilisha vyama vidogo vya kisiasa na wengine ni wagombea huria. Ilitarajiwa kuwa Bashir atashinda kirahisi na chama chake kitapata ushindi mkubwa.

========================

_82593825_82591137.jpg

President Omar al-Bashir says the charges against him are politically motivated


Sudan's President Omar al-Bashir has been re-elected with 94% of the vote, according to official results.

His victory, which was widely expected, means he can now extend his 25-year rule by a further five years.

The country's main opposition parties boycotted the elections.

Turnout was about 30-35%, African Union observers said.
Mr Bashir denies International Criminal Court charges of ordering a genocide in the Darfur conflict.

Official turnout was 46.4%, but the BBC's James Copnall, who reported on the elections from Khartoum, says many believe the real figure was even lower.

Western countries, including the US, Britain and Norway, criticised the polls for not being free and fair.

The African Union monitors said that basic freedoms and human rights would have "enhanced" the polls.


Source:BBC
 
Marais wa Afrika bwana wala hawana haya..eti kapata asilimia 94.5%...Kwa hiyo alikuwa anashinda na kivuli chake sio...maana ni kama alikuwa anajipiga 'photocopy' hivi🙂
 
Marais wa Afrika bwana wala hawana haya..eti kapata asilimia 94.5%...Kwa hiyo alikuwa anashinda na kivuli chake sio...maana ni kama alikuwa anajipiga 'photocopy' hivi🙂


Ndo miafirika ilivyo ukanda huu, ukitoka kwa Albashir unamkuta Mseven, ukitoka kwa mseven unamkuta Kagame, Ukitoka kwa Kagame unamkuta Ngurunziza, Ukitoka kwa Ngurunziza unamkuta Kabila na ukitoka kwa kabila unamkuta baba yao Mugabe. Hapo bado hatujafika kaskazini mwa jangwa la sahara, hao viongozi wanaamini kua wao tu ndio waliozaliwa kwa ajili ya kuwatawala wengine.
 
Back
Top Bottom