GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,443
- 120,800
Wakati nikitegemea kabisa kuwa leo katika Mkutano wako na Waandishi wa Habari utaonyesha ni jinsi gani ulivyokomaa katika medani ya Kandanda / Soka / Mpira wa Miguu kwa kutoa sababu za kiukweli na kiufundi pia huku ukikubali kuwa Simba Sports Club tumefanya vibaya katika hali tu ya kimpira hali haikuwa kama nilivyotegemea.
Kwanza nianze kwa kusema kuwa Mimi ni Mshabiki tena wa kindakindaki wa Klabu ya Simba Sports Club na ninaweza kusema kuwa pengine naipenda timu yangu ya Simba Sports Club kuliko hata Girlfriend wangu na kama hiyo haitoshi naweza pia kukuambia kuwa kwa kukuonyesha kuwa Mimi ni Simba lia lia nilifanya kazi kubwa sana ya " kiutamaduni / kiufundi " kwa kushirikiana na mtani wangu wa Kirangi ambaye sasa ni Mbunge na miaka kama mitatu minne iliyopita alikuwa Naibu Waziri wa hii sekta lengwa hapa ( nadhani wote mmemjua ) na yule Mhindi mwenye mghahawa wake pale Posta karibu kabisa na picha ya Askari ( zamani fast food na sasa huo mghahawa wake unaanzia na herufi " H " ) ambapo kwa pamoja tulijisahaulisha kuwa kuna Mungu na tukajitia uchizi kisha tukachinja paka kama watatu ( 3 ) hivi kwa mikono yetu ambapo tuliweza kuifunga Enyimba goli moja ( 1 ) lililofungwa na Emanuel Gabriel " Batigol " japo halikutosha kutuvusha kwa sababu ambazo hata Wewe Aveva unazijua ambapo hiyo mechi baadhi yenu watu wa friends of Simba mliiuza kwa Enyimba.
Kuna mifano mingi sana ningeweza kutoa hapa ambayo ilipelekea Simba yetu kufanya vizuri ila kwa muda sitaelezea japo Marehemu ambaye leo tunakumbuka Kifo chake Mchezaji mahiri wa Kiungo Patrick Tabu Mutesa Mafisango " Petit Makambo " alinipenda kwa moyo wangu mkubwa wa kujitolea kuisaidia Simba ili ipate ushindi na kuna michezo mingi sana ya hatari nimeweza kuifanya huku nikihatarisha hadi maisha yangu ili tu niiwezeshe timu yangu ninayoipenda ya Simba Sports Club ishinde na ndiyo maana kila siku namlilia sana Marehemu Mafisango kwani alituheshimu sana sisi Watendaji wa " Fitna, Kiufundi na Kiutamaduni " wa Simba Sports Club kwa wakati huo.
Rais Aveva hakuna siku ambayo umeniumiza kama leo na hasa kwa kutoa sababu ambazo naomba tu niseme ukweli kuwa ni za kipumbavu sana na sikutegemea kama Wewe ninayekujua leo ungepopomika vile na nimeshangaa pia hata wale Waandishi wa Habari waliokuwepo kushindwa kukuuliza very technical questions na badala yake wote walikuwa wakiuma uma tu kalamu zao huku wengine wakisinzia na baadhi yao kuchati ili umalize kuwaboa waondoke zao.
Rais wa Simba Sports Club hivi Wewe ni wa kusema sababu hizi zifuatazo kweli?
Rais wa Simba Sports Club Mimi nimeumbwa na uso wa haya na sipendi au siwezi kuwa mnafiki na huwa ni Mtu wa kunyoosha maneno hata kama yatauma lakini ndiyo nimesema hivyo. Unajua fika kuwa Mimi ni Mwana Simba Sports Club lakini nisifiche kwa kusema kuwa Yanga ilistahili kuchukua ubingwa kwa sababu zifuatazo:
Akhsanteni nyote ila Viongozi wa Simba tusaidieni mtufurahishe ili majina kama wa mchangani, mara wa matopeni na sasa chura na inavyoelekea karibuni tu tutaitwa Bata au hata Kenge yasitokee tena kwani yanatuuma mno jamani. Jioni njema nyote!

- Kwamba Simba tumefanya vibaya kwakuwa mchezaji Hassan Kessy katufungisha.
- Kwamba Simba tumefanya vibaya kwakuwa mchezaji Ajib alienda Afrika ya Kusini.
- Kwamba Simba tumefanya vibaya kwakuwa E fm Radio ilituandama.
- Kwamba Simba tumefanya vibaya kwakuwa Waamuzi walituuma sana michezoni.
- Kwamba Simba tumefanya vibaya kwakuwa Wachezaji wa Kigeni wanagoma goma.
- Kwamba Simba tumefanya vibaya kwakuwa TFF ilipanga ratiba yake vibaya.
- Kwamba Simba tumefanya vibaya kwakuwa Yanga inabebwa / kupendelewa na TFF.
- Hivi si ni Mchezaji huyu huyu Hassan Kessy alitusaidia sana Simba katika mechi zetu zile saba za ushindi mfululizo?
- Kama leo unasema kuwa Mchezaji Hassan Kessy anatumiwa na Yanga sasa ilikuwaje nyie Viongozi wa Simba kutwa mlikuwa mnaenda pale TFF kukumbushia ile barua yenu ya malalamiko baada ya Kessy kuchezewa rafu mbaya na Donald Nombo Ngoma wakati wa mechi yetu ya mzunguko wa kwanza?
- Umesema kuwa Mchezaji Ibrahim Ajib " abracadabra " kuondoka kwake majuzi kwenda kufanya majaribio Afrika ya Kusini kuliiponza sana Simba kufanya vizuri na hata kuchukua Ubingwa. Hivi Ajib alipoondoka ile wiki iliyopita Simba ilikuwa na points ngapi na ilikuwa nafasi ya ngapi na Yanga ambao tulikuwa tukiwafukuzia wao walikuwa na points ngapi?
- Umesema kuwa E FM radio ilituandama. Naomba kuuliza E FM walikuwa wanawashika miguu Wachezaji wetu wa Simba kiasi kwamba wanashindwa kufunga magoli? Hivi unajua Kazi ya Vyombo vya Habari lakini Rais wangu?
- Umesema kuwa Waamuzi ( Referees ) walituuma sana hadi tukafanya vibaya. Naomba kuuliza kwahiyo Wewe ulitaka Waamuzi wawe wanatubeba Simba? Hata kama kweli wangeamua kutubeba kwa Timu yetu ilivyo na aina ya mpira wa KIPOPOMA tuliokuwa tunacheza hiyo " mbeleko " ingefaa kweli kwetu?
- Unadai wachezaji wa Kigeni wa Simba walikuwa wanagoma. Naomba kukuuliza ulitaka wacheze tu mechi zetu huku matumbo yao yakiwa yamejaa tu " minyoo " na kuwaza jinsi wenye nyumba wao watakavyowafuza kwa kushindwa kulipa Kodi zao? Lakini kama haitoshi hivi Rais wangu inamaana hadi leo umeshindwa tu kujua tofauti ya Mchezaji wa Kigeni na hawa wetu wa madafu? Kabla ya kuliongelea hili mbele ya Press leo ulijiridhisha vizuri Kisheria na kihoja ili usije kuwa Kituko kwa " Majiniasi " kama sisi wenye kujua kufikiri kisawasawa?
- Umesema TFF ilipanga ratiba vibaya. Naomba kukuuliza hivi kati ya Simba na TFF nani ndiyo Baba na nani ndiyo Mtoto? Hivi Simba siyo mmoja wa Mwanachama wa Kamati ya kupanga ratiba za ligi kuu nzima ambayo ninavyojua hushirikisha timu zote shiriki na mwishowe wote hukubaliana na ratiba ambapo mkiiridhia basi ndipo TFF huitoa hadharani. Hata kama TFF wamepangua ratiba ila Wewe kama mpambanaji unatakiwa muda wote uwe tayari kwa dharura yoyote sasa je ina maana Wewe Kamanda Mkuu wa Simba ulishindwa kujipanga kidharula?
- Umesema kuwa Yanga imebebwa na TFF. Rais wangu kumbe ulikuwa unajua Yanga inabebwa na TFF sasa kwanini ulishindwa tu kuamuru Simba tusicheze mechi zetu na badala yake tu tuwaombe TFF wawape Yanga ubingwa lakini badala yake na sisi tukijua kabisa Yanga inabebwa bado tunacheza ligi? Kama Yanga inabebwa ilikushinda nini na Wewe kuwavutia TFF wakubebe?
- Acheni kubadili makocha kila mara kwa chuki binafsi na kukosa 10%.
- Kazi ya usajili ifanywe na Kocha Mkuu na si mtu mwingine yoyote na Kocha aaminiwe.
- Timu ijengwe Kisayansi na tuache kuwekeza kwa Waganga Morogoro na Pemba.
- Vunja Kamati zote ulizoziunda na ibaki moja tu kwani inatosha ikijipanga.
- Hakikisheni mnawajali na kuwapenda Wachezaji ili kuwajenga Kisaikolojia.
- Timu yetu ya B iangaliwe na itunzwe kama mboni za macho yetu kwani ndiyo mkombozi.
- Viongozi tujengeeni umoja wa kuaminika na kuaminiana sisi Wapenzi wenu.
- Ukiendelea na Viongozi hawa Godfrey Nyange Kaburu na Said Tully Simba isahau Ubingwa kwani nina uhakika na hata wao wanajua fika kuwa nawajua kuwa Wao ni Mashabiki wa Yanga tena ile Kindakindaki ( Wakikubishia rudi kwangu nikupe usilolijua na hutaamini )
- Acheni kutaka mbeleko za Waamuzi bali chezeni mpira.
- Acheni kila mara akili yenu kuiweka kwa Yanga bali jipangeni nyie kama nyie.
- Acheni kupoteza muda wenu mwingi kutaka kununua mechi ili mshinde muonekane wema kwa Wanachama hilo halitawasaidia nyie kama Viongozi lakini hata timu yetu ya Simba na Soka la Tanzania kiujumla.
Rais wa Simba Sports Club Mimi nimeumbwa na uso wa haya na sipendi au siwezi kuwa mnafiki na huwa ni Mtu wa kunyoosha maneno hata kama yatauma lakini ndiyo nimesema hivyo. Unajua fika kuwa Mimi ni Mwana Simba Sports Club lakini nisifiche kwa kusema kuwa Yanga ilistahili kuchukua ubingwa kwa sababu zifuatazo:
- Yanga wana umoja.
- Yanga wamesajili kiufundi.
- Yanga wanawajali sana Wachezaji wao.
- Yanga wamediriki kufuata ueledi wote wa mchezo wa mpira kwa Wachezaji wake.
- Yanga wamewekeza katika upendo wa Kinidhamu kwa Wachezaji wake.
- Yanga wana malengo ya mbali na ya kimafanikio zaidi.
- Yanga hawawekezi sana katika " ndumba " kama sisi Simba ambao " ndumba " imetukolea kunakotukuka hadi sura zetu wana Simba wote sasa zimekaa kichawi chawi tu.