Rais wa Nchi anapofariki akiwa madarakani Nchi huwa katika nyakati za hatari zaidi kuliko wakati wowote ule

1)Makamu wa Rais

2)Kuhusu "Twende na dunia inavyotaka" umeelewa lipi la ajabu?!!!
Lini Tanzania ilikwenda kinyume na dunia inavyotaka ilihali tu wanachama wa UMOJA WA MATAIFA NA JUMUIYA YA MADOLA...

Una mfano upi wa Tanzania kupata kuishi "kuzimu"?!!!
Lock down ya Uviko-19, haikuwa twende na Dunia. Je, alienda nayo?
 
Bos usiongee kwa hisia .Ebu jiulize JPM alikua na nguvu gani CCM had kuwa Rais?Sasa huoni kwamba kulikua na nguvu nyuma ya pazia iliyomweka?Mfumo wa ulinzi na Usalama wa hii Nchi ni zaidi ujuavyo.Mwalimu Nyerere huyu Mzee hakuna wa kawaida kwa mambo aliyoyafanya.

Pia fahamu kuwa Rais wa Nchi yoyote yenye mfumo wa ulinzi na Usalama uliomadhubuti Huwa hatokei ghafula tu Huwa anaandaliwa na mfumo wa Usalama zeni mnaletewa tu kupiga kura .Hiyo ipo duniani kote kwa Nchi ambazo zipo vizuri kiulinzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi huo usalama mnaouengelea humu ni wa namna gani, mbona beberu likiamua kumchomoa madarakani kiongozi wasiyemtaka huo usalama unaufyata?

Tazama Libya, ghadafi alichomolewa kwenye mtaro wa maji machafu na baadae akalambwa shaba ninao uhakika usalama wa Taifa hilo ni imara kuliko bongo, the same na Sadam Hussein alichomolewa Kwenye handaki akiwa amefuga ndevu huku Afya yake ikiwa dhaifu huo usalama wake wa Taifa ulikuwa wp?

Msijilishe upepo humu kwa madai ya usalama wa Taifa ni hatari sn kuliko kitu kingine labda kidogo ungetaja jw, wapo serious kidogo japo sio kiasi cha kumtisha beberu kufanya atakacho kwenye nchi zetu hizi za dunia ya tatu.
 
Huyo anafanya maskhara na CCM....anaongea kama yuko ndotoni vile......
Mimi sio CCM na Sijawahi kufikiria kuwa katika CCM. Ikitokea wameogopa kushindanisha Mawazo na Hoja katika kumpata mgombea na badala Yake kumwachia mama pekee nitachukua Kadi ya Uanachama na kisha kuchukua Fomu ili kuwafundisha kuwa Fikra za kuzawadiana Uongozi wa Nchi sio Fikra za Chama Bali genge la watu wanaotafuta kufanya Biashara na kutoa nyongo Zao dhidi ya Wanaume wanaowaona wamepata kuwa vikwazo katika maisha yao.
 
Aisee umeweka mkwara mzito poti, lakini sie tupo na Mama.

#Mama 2025.
 
Sawa....

Basi kaa ukijua CCM ina mila zake....si lazima mila zake uzipende....na ndio maana sisi tuliozipenda HATULALAMIKI....vipi unamlazimisha muislam kuwa na mke mmoja tu?!!!!!Khaaa 😲😲😲

Unataka kusema mh.Rais SSH anawachukia wanaume?!!!!!Khaaa 😳😳😳😳

#SiempreJMT
 
Huyo waziri mkuu wa Israel unayesema ni Isack Rabin ndio huyu nayemjua kwa jina Yitzhak Rabin? KJB ni nani au unamaanisha KGB? Hivi kumbe bado KGB ipo sio ilikufa baada ya Soviet kuparanganyika?
 
Aisee umeweka mkwara mzito poti, lakini sie tupo na Mama.

#Mama 2025.

Sawa....

Basi kaa ukijua CCM ina mila zake....si lazima mila zake uzipende....na ndio maana sisi tuliozipenda HATULALAMIKI....vipi unamlazimisha muislam kuwa na mke mmoja tu?!!!!!Khaaa 😲😲😲

Unataka kusema mh.Rais SSH anawachukia wanaume?!!!!!Khaaa 😳😳😳😳

#SiempreJMT
Mila za kufurahia kifo cha mwanachama mwenzako eti hali hiyo imempa fursa ambayo akiacha kuitumia Mungu atamdharau! Kumbe Watanzania walikuwa wanalia na kumtandikia JPM khanga Barabarani huku yeye akiwa anafyatua Picha kichwani jinsi atakavyokuwa sasa mwanamke wa kwanza kwa kuchaguliwa 2030.
 
S
Aisee umeweka mkwara mzito poti, lakini sie tupo na Mama.

#Mama 2025.
Sio Mkwara bali Ni Ukweli mtupu. Chama sio yeye. Ni lini chama kimekaa na kumpitisha awe mgombea pekee? Yeye anadhani ana uwezo kuliko wenzake wote na kama sivyo anataka kugombea kwa sababu gani kama hawashindi wenzie? .
Kama kweli anaamini ana Uwezo atangaze na wenzie wachukue Fomu aone kama atapasua.
 
Mila za kufurahia kifo cha mwanachama mwenzako eti hali hiyo imempa fursa ambayo akiacha kuitumia Mungu atamdharau! Kumbe Watanzania walikuwa wanalia na kumtandikia JPM khanga Barabarani huku yeye akiwa anafyatua Picha kichwani jinsi atakavyokuwa sasa mwanamke wa kwanza kwa kuchaguliwa 2030.
Kwakweli mtu anayefurahia kifo cha mwenzie basi amekosa ubinadamu lakini kila mtu ameandikiwa siku yake ya ahadi ambayo atarejea kwa muumba wake kutoa hesabu ya matendo yake.

#Mama 2025.
 
S

Sio Mkwara bali Ni Ukweli mtupu. Chama sio yeye. Ni lini chama kimekaa na kumpitisha awe mgombea pekee? Yeye anadhani ana uwezo kuliko wenzake wote na kama sivyo anataka kugombea kwa sababu gani kama hawashindi wenzie? .
Kama kweli anaamini ana Uwezo atangaze na wenzie wachukue Fomu aone kama atapasua.
Mbona umefura namna hiyo? Katiba yenyewe ilitambua kwamba kuna mauti na kama yakitokea nini kifanyike? Muacheni huyu Mama afanye kazi.

#Mama 2025.
 
Mila za kufurahia kifo cha mwanachama mwenzako eti hali hiyo imempa fursa ambayo akiacha kuitumia Mungu atamdharau! Kumbe Watanzania walikuwa wanalia na kumtandikia JPM khanga Barabarani huku yeye akiwa anafyatua Picha kichwani jinsi atakavyokuwa sasa mwanamke wa kwanza kwa kuchaguliwa 2030.
Mkuu wangu hebu shusha pumzi kwanza....

Si mimi si mh.SSH alifurahishwa na kifo cha kipenzi chetu hayati JPM....mola alimpenda zaidi ,wewe ungeweza kuzuia asinyakuliwe mawinguni?!!!!

Maisha inabidi yaendelee.....

Ndio maana KATIBA ikatuchorea mchoro wa kipi cha kufuatwa ikitokea hali ile...je katiba nayo mbaya....ilimchukia JPM?!!!!

Unemtafsiri vibaya mh.Rais pale aliposema "fursa"....kwani uongo si fursa ya yeye kutokea umakamu na leo kuwa RAIS?!!!

Kwani angeweza kukataa na "kustep down" asingeheshimiwa msimamo wake.....yeye alikubali kuendana na katiba na kuibeba DHIMA ya URAIS WA JMT....je kutaka kuwa Rais wa kuchaguliwa na kuiweka historia kwa mwanamke wa kwanza kupigiwa kura za Urais ni kubaya?!!!

Bila ya kutokea kile kifo unadhani ingetuchukua miaka mingapi kwa mwanamke kushika/kuchaguliwa URAIS?!!!

Tatizo mjadala tunauendea KIHISIA zaidi ya UHALISIA....

Kwako mwenyekiti......
 
Mbona umefura namna hiyo? Katiba yenyewe ilitambua kwamba kuna mauti na kama yakitokea nini kifanyike? Muacheni huyu Mama afanye kazi.

#Mama 2025.
Kwa hiyo, Katiba ndio imesema 2030 nako arithi nafasi hiyo bila kushindana na wenzie kwenye Chama? Unaisingizia Katiba kuwa inatoa Uraisi kama Njugu zinavyoweza kugawiwa madhali Muombaji awe na meno ya kuzitafuna?
 
Nisaidie wapi nilipo andika #2030 Mkuu, kamhemko kamekupata sasa.

Anyway tumpe support Mama.
 
SSuki
Mkuu wangu hebu shusha pumzi kwanza....

Si mimi si mh.SSH alifurahishwa na kifo cha kipenzi chetu hayati JPM....mola alimpenda zaidi ,wewe ungeweza kuzuia asinyakuliwe mawinguni?!!!!

Maisha inabidi yaendelee.....

Ndio maana KATIBA ikatuchorea mchoro wa kipi cha kufuatwa ikitokea hali ile...je katiba nayo mbaya....ilimchukia JPM?!!!!

Unemtafsiri vibaya mh.Rais pale aliposema "fursa"....kwani uongo si fursa ya yeye kutokea umakamu na leo kuwa RAIS?!!!

Kwani angeweza kukataa na "kustep down" asingeheshimiwa msimamo wake.....yeye alikubali kuendana na katiba na kuibeba DHIMA ya URAIS WA JMT....je kutaka kuwa Rais wa kuchaguliwa na kuiweka historia kwa mwanamke wa kwanza kupigiwa kura za Urais ni kubaya?!!!

Bila ya kutokea kile kifo unadhani ingetuchukua miaka mingapi kwa mwanamke kushika/kuchaguliwa URAIS?!!!

Tatizo mjadala tunauendea KIHISIA zaidi ya UHALISIA....
,
Kwako mwenyekiti......
Sikiliza mkuu, anayejiamini havizii Weakness itokee. Kama yeye anaamini pamoja na uanawake anao uwezo wa kuwashinda wanaume au wanawake wenzie Ni kwa nini hakuwahi kugombea hiyo nafasi?

Je, kama anaona wanaume wamewakandamiza wanawake kwa muda mrefu kwa kutokuwapitisha kugombea na sasa Ni muda Wao, Ni kwa nini asitangaze Fomu za Uraisi zitolewe kwa wanawake wengine pia wachuane? Kwa nini yeye kujitangaza mgombea pekee haoni naye anarudia makosa yaleyale ya ubaguzi? Au tuseme kwa Tanzania mpaka sasa yeye ndo mwanamke pekee mweny uwezo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom