Rais wa FIFA aipongeza Yanga!!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984


Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino, ameipongeza timu ya soka Young Africans ya Dar es Salaam, kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16.


Young Africans imetwaa ubingwa huo kwa msimu wa pili mfululizo, lakini ikiwa ni mara ya 26 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara mwaka 1965.

Katika salamu zake, kupitia barua yake ya Mei 18, 2016 kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, Infantino ameelezea ubingwa wa Young Africans kwamba umetokana na kazi kubwa inayofanywa na uongozi wa timu hiyo, makocha, wachezaji pamoja na mashabiki.

“Yanga ndiyo mabingwa wa Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Young Africans na timu nzima isiyoshindika kwa mafanikio haya makubwa. Taji la Young Africans ni matokeo ya mshikamano ulioko ndani ya Young Africans,” amesema Infantino katika barua hiyo yenye kichwa cha habari kinachosema: Salamu za Pongezi kwa Young Africans.

Amesema pongezi zake ziende kwa uongozi wa klabu, makocha na benchi nzima la ufundi, wachezaji, madaktari pamoja na mashabiki wote wa Young Africans.

“Kwa niaba ya familia ya soka, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Young Africans na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa jinsi mnavyopeleka ujumbe chanya wa soka kwa jamii ya michezo,” alisema Infantino katika barua hiyo iliyotua TFF Mei 21, mwaka huu.

Tayari Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikwisha kuipongeza Yanga ambayo imepewa Kombe na medali kwa wachezaji 24, viongozi saba wa benchi la ufundi na viongozi wanne wa Kamati ya Utendaji na kwa sasa wanasubiri zawadi ya fedha Sh 81,345,723
 
Ataachaje kuipongeza wakati YANGA ni WAKIMATAIFA....lakin utakuja shangaa wale wa Chura Matopen Fc wakisema Raisi wa FIFA anaibebya YANGA


Rais wa Fifa, Gianni Infantino ameipongeza Yanga kutokana na hatua iliyofikia.
Yanga imekuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kucheza hatua ya makundi au robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho iliyo chini ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf).

Hivi punde, tutawaletea taarifa kamili kuhusiana na hilo.
Ataachaje kuipongeza YANGA wakati anatambua kuwa hao ndio WAKIMATAIFA? Ila utasikia wale Chura matopen FC wakisema Raisi wa FiFA anaibeba YANGA
 
Japo mimi ni mwana msimbazi lakini Watani zetu mwaka huu wapo vizuri.....kulikataa hilo ni sawa kujitia presha isiyo na sababu....
905c9536ee09620d4cc659f5e9dd9d35.jpg
 
Inawezekana hata hajui kama kuna kitu kinaitwa Yanga dunia hii.

Wasaidizi wake wameandika na yeye akaishia kusign.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom