Enzi zile wazungu walikuja kwa nguvu na kufanya uporaji wa rasilimali zetu na tukajitahidi kuonyesha ukakamavu wetu kuzuia ukoloni.
Leo hii bado Tanzania na nchi zingine za Afrika hazioni haya ya kufungua milango yote kukaribisha mifumo mipya ya ubepari na ubeberu.
Inajulikana wazi kwamba China hawaweki nyuzi za masharti yoyote kwenye mikataba tunayofanya nayo na wanamezea Ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu ili mradi wao wanapata rasilimali wazitakazo.
Leo hii barani mwetu kuna wachina wasiopungua milioni mbili wakifanya shughuli ambazo zingeweza kufanywa na waafrika wenyewe hata uchuuzi wa bidhaa mitaani, je watanzani atupo wangapi kule Uchina?