Rais umewadharau watanzania na nchi yao

Rais umewadharau watanzania na nchi yao

fisi 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
3,284
Reaction score
4,652
Nimesikiliza hotuba ya Rais juu ya uwekezaji kwenye madini na gesi. kwa kifupi imenisikitisha sana. Mbali na kukubaliana na mengi uliyoyafanya Rais wangu hili la madini nakupinga mapema sana. Rais kutoa kauli kuwa eti kuchimba kisima kimoja kutafiti gesi ni zaidi ya dola milioni 100 na kuuliza nani ataweza .... ni udhaifu na dharau kubwa kwa nchi na watu wake. Utafiti wa gesi ulianza miaka ya 1950s hapa Tanzania. Hebu tujiulize ni kwa nini mwalimu Nyerere aliacha madini yetu kwa miaka yote hii?Hakukuwa na wazungu wenye uwezo wa kuja na kuyafyonza yote na kutulipa % iwe 65% au 75%? Jibu ni moja kujenga uwezo kwa watanzania kumiliki na kuendeleza sekta hiyo ya madini. Hakuna unafiki hapo.

Sidhani kama Rais alitoa hotuba ya jana kwa kuambiwa au kusikia. Nilitegemea hili, Serikali iwaandae watanzania kumiliki na kuendeleza uwekezaji kwenye gesi na madini. Kauli ya kuwambia watashirikishwa IFUTWE kabisa ni uongo na dharau nyingine. Unaweza kushirikiswha kwa kutolewa hotuba tu kama hizi. Pamoja na kuwa ni biashara kubwa duniani kiundwe chombo cha kuwawezesha hao wenye mitaji midogo kuunganishwa kwa shares na kuwekeza kwenye gesi. vinginevyo isichimbwe tusubiri capacity building ifanyike. Hata makampuni mengi ya nje hayakutoka mbinguni na uwezo huo,yamewezeshwa na mitaji midogo iliyokusanywa na kuthibitiwa. Kupitia TPDC watanzania na mitaji yao wawezeshwe kwanza na sio wadharauliwe kama alivyofanya katibu mkuu wa wizara, waziri Muhongo na sasa Rais.

Njia moja pia ni kwa hayo makampuni yanayosifiwa kutoka nje yalazimishwe kuwapa shares watanzania moja kwa moja kwenye shughuli za gesi na madini. Yalazimishwe kuwaajiri watanzania asilia. Kama hiyo haifanyiki WAONDOKE. Tuangalie wenzetu wa Asia kusini wanafanya nini. tufahamu kwamba wao sasa hivi wanatuhitaji sisi zaidi kuliko hapo kabla.

Kwa hili Rais umekosea kama ilivyo kwenye sekta ya Ujenzi (Construction) ambapo tunaona miradi mikubwa wanapewa wageni kwa vigezo vya kutokuwa na uwezo. Baada ya ujenzi kukamilika hatuna wazalendo wanaokuwa na uwezo kuisimamia miradi hiyo tunawaita tena wageni hao na kuwapa ajira hizo for the life time of the project. Tutaona tu kwenye daraja la Kigamboni.Serikali imenunua vifaa vya ujenzi kwa mfano na kuwakodishia wazalendo ili kushindana kimataifa kama CRJC etc?

Hotuba ya Rais ni sawa na kudharau chakula cha nyumbani ukisema pamoja nakuwa mnajua kupika hamuwezi kupikia kwenye JIKO hili.Utakula huko nje hadi lini?

Rais wafanye watanzania waweze KUMILIKI NA KUTHIBITI SEKTA YA MADINI NA GESI KWANZA ( sio washirikishwe) Vinginevyo yote uliyofanya kwa kipindi chako yatakuwa hayana maana.

wana jf endeleeni...........
 
Hizi dharau za wanasiasa wa bongo ni mbaya sana. Hivi huwa hawataki hata kureview kwa viongozi wa nchi nyingine zilizokuwa na uchumi unaofanana na wa kwetu kuwa walifanyaje wakaweza? Mifano ipo mingi sana. Nchi kama Vietnam, Malasia, Singapore na Botswana waliwajengea uwezo wananchi wao kwa kuwapa mikopo isiyokuwa riba na wamewatengeneza mabilionea wa kutosha kila sekta. But maybe, ndo maana hajui kwanini watz ni maskini.
 
Kiherehere kama kawaida yake! Kulikuwa na ulazima gani kuanza kuchimba kwa hasara sasa kama unajua watanzania bado hawajaweza ???
 
Rushwa ndio motivation yao ya kuviuza hivi vitalu mbiombio kabla hawajatoka madarakani!!! Namkumbuka Nyerere wetu na laiti angekuwa hai huu ushenzi usingefanyika!!!
 
prof mhongo wakala wa vitalu vya gesi.

yuko wapi? Mbona hasikiki wala kuonekana? Hajafungua kampuni ya uwakala wa vitalu vya gesi na madini? Tujuzeni mnaoifahamu ilipo ofisi ya prof huyu mwenye dharau na kiburi anidalalie kitalu cha gesi kwani kuna tajiri wa kichina anakitaka.
 
10818376904_211a8bd116_b.jpg
E8sbG9jh.jpg
 
Serikali kwa sasa imebanwa na wafadhili pesa hakuna sasa kinachofanyika Ni kugawa maliasili ya Tanzania ili apate pesa ya kumalizia kipindi kilichobaki
 
wacha muda wake uishe akapunzike ale matunda aliyochuma
 
awamu ya rais huyu, umetokea ufisadi mkubwa kuliko hawamu zote.

eskro, epa, richmod, bomba la ges, vodacom skendo...
 
Nina wasiwasi huenda rais ajaye atamshtaki kwa kuruhusu ubadhirifu na ufisadi wa raslimali za nchi. Bora amwondolee kinga ashtakiwe ili liwe fundisho kwa viongozi wote wa umma.
 
Huu ni upuuzi wanataka kuiendesha nchi kama wanavyoziendesha familia zao
 
Nimesikiliza hotuba ya Rais juu ya uwekezaji kwenye madini na gesi. kwa kifupi imenisikitisha sana. Mbali na kukubaliana na mengi uliyoyafanya Rais wangu hili la madini nakupinga mapema sana. Rais kutoa kauli kuwa eti kuchimba kisima kimoja kutafiti gesi ni zaidi ya dola milioni 100 na kuuliza nani ataweza .... ni udhaifu na dharau kubwa kwa nchi na watu wake. Utafiti wa gesi ulianza miaka ya 1950s hapa Tanzania. Hebu tujiulize ni kwa nini mwalimu Nyerere aliacha madini yetu kwa miaka yote hii?Hakukuwa na wazungu wenye uwezo wa kuja na kuyafyonza yote na kutulipa % iwe 65% au 75%? Jibu ni moja kujenga uwezo kwa watanzania kumiliki na kuendeleza sekta hiyo ya madini. Hakuna unafiki hapo.

Sidhani kama Rais alitoa hotuba ya jana kwa kuambiwa au kusikia. Nilitegemea hili, Serikali iwaandae watanzania kumiliki na kuendeleza uwekezaji kwenye gesi na madini. Kauli ya kuwambia watashirikishwa IFUTWE kabisa ni uongo na dharau nyingine. Unaweza kushirikiswha kwa kutolewa hotuba tu kama hizi. Pamoja na kuwa ni biashara kubwa duniani kiundwe chombo cha kuwawezesha hao wenye mitaji midogo kuunganishwa kwa shares na kuwekeza kwenye gesi. vinginevyo isichimbwe tusubiri capacity building ifanyike. Hata makampuni mengi ya nje hayakutoka mbinguni na uwezo huo,yamewezeshwa na mitaji midogo iliyokusanywa na kuthibitiwa. Kupitia TPDC watanzania na mitaji yao wawezeshwe kwanza na sio wadharauliwe kama alivyofanya katibu mkuu wa wizara, waziri Muhongo na sasa Rais.

Njia moja pia ni kwa hayo makampuni yanayosifiwa kutoka nje yalazimishwe kuwapa shares watanzania moja kwa moja kwenye shughuli za gesi na madini. Yalazimishwe kuwaajiri watanzania asilia. Kama hiyo haifanyiki WAONDOKE. Tuangalie wenzetu wa Asia kusini wanafanya nini. tufahamu kwamba wao sasa hivi wanatuhitaji sisi zaidi kuliko hapo kabla.

Kwa hili Rais umekosea kama ilivyo kwenye sekta ya Ujenzi (Construction) ambapo tunaona miradi mikubwa wanapewa wageni kwa vigezo vya kutokuwa na uwezo. Baada ya ujenzi kukamilika hatuna wazalendo wanaokuwa na uwezo kuisimamia miradi hiyo tunawaita tena wageni hao na kuwapa ajira hizo for the life time of the project. Tutaona tu kwenye daraja la Kigamboni.Serikali imenunua vifaa vya ujenzi kwa mfano na kuwakodishia wazalendo ili kushindana kimataifa kama CRJC etc?

Hotuba ya Rais ni sawa na kudharau chakula cha nyumbani ukisema pamoja nakuwa mnajua kupika hamuwezi kupikia kwenye JIKO hili.Utakula huko nje hadi lini?

Rais wafanye watanzania waweze KUMILIKI NA KUTHIBITI SEKTA YA MADINI NA GESI KWANZA ( sio washirikishwe) Vinginevyo yote uliyofanya kwa kipindi chako yatakuwa hayana maana.

wana jf endeleeni...........

Viongozi wetu hawana uzalendo wala huruma na watanzania.Inawezekana kabisa wazawa wakawa wamiliki wakuu wa hivi vitalu vya gesi na madini.Kikubwa ni Serikali yetu kuwa na nia na uthubutu wa kuwandaa Watanzania ili wawe wamiliki wakuu
 
Linapokuja swala la uwekezaji wazawa huwa wanapuuzwa kutokana na maslahi binafsi ya viongozi, kwanini wang'ang'anie wawekezaji kutoka nje ikiwa kuna wazawa? Hata kama wana mitaji midogo hao walio na mitaji mikubwa je hawakuanza na hiyo midogo?
 
Ukitaka kujua uwezo wa wasomi wa kitanzania angalieni mji wa Dar es salaam ulivyo mji hauweleweki ndio mtaweza kuchimba Gas nyie.

Acheni maneno ya kwenye vijiwe jitambueni kwanza , wengi wenu mnau cold blood (albino) na mnawatia vilima vya Maisha innocent kwa ajili ya utajiri au politics.
 
Back
Top Bottom