Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Alhaj Dr Ali Mohamed Shein amewaonya wapinzani wanaotaka kukwamisha mipango ya serikali yake hawatavumiliwa huku akiweka bayana kuwa hakuna uchaguzi mwingine wala serikali ya mpito.
Alhaj Shein ametoa msimamo huo katika hotuba yake ya baraza la eid kwa wananchi wa Zanzibar katika sherehe za eid el-fitr ambazo zinatokana na kumalizika kwa mwezi mtukufu wa ramadhani zilizofanyika katika ukumbi wa zamani baraza la wawakilishi na kuhudhuriwa na viongozi wastaafu na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vinavyoshirikiana na serikali akiwemo makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano Mh Samia Suluhu Hasan ambapo kabla ya kuhutubia Dr Shein aliwasili akiwa katika msafara mzito na kupokea salamu za heshima kwa gwaride la kikosi maalum cha FFU na wimbo wa taifa.
Akihutubia umati huo Dr Shein amesema wanaopita kutangaza kuwepo kwa uchaguzi mwingine au ujio wa Serikali ya mpito wanawadanganya wananchi kwa vile uchaguzi halali umeshafanyika kwa mujibu wa sheria na katiba na serikali iko kazini.
Dr shein pia alisisitiza umuhimu wa nchi kuwa katika amani ambayo ameahidi kuwepo wakati wote na kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kuweka maslahi ya nchi kwa kupendana na sio kubaguana kwa vile Zanzibar ni ya wote.