Rais Samia, Wazee Kama Makamba hawakusaidii bali ni wachumia tumbo

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,800
71,222
Matukio mawili yaliyo jitokeza kwenye huo mkutano mkuu wenu yameonyesha wazee mastaafu aina ya Makamba hawapo ndani ya CCM kukusaidia bali kulinda maslahi yao na watoto wao kwa kutumia style za uchawa wanazotumia hasa wasanii.

1. Alipokuwa nje ya ukumbi akihojiwa na waandishi, lilipofika suala muhimu la umeme akapandwa na jazba za wazi kuonyesha kumlinda mwanae badala ya kutumia busara kulielezea na jinsi ccm itakavyo isaidia serikali kutafuta utatuzi. Yeye kafanya ni la familia kwa sababu ya mlo wa January na mfanya biashara wa majenereta Mwamvita.

2. Pamoja na Magufuli kuwa na matatizo yake (hasa nje ya ccm) Makamba hakupaswa kutamka maneno mabaya kama yale kuwa wema hawafi katika kipindi hiki kifupi ambacho ndio umeingia madarakani baada ya mtangulizi wako KUFA. Tena mbele ya mjane wa marehemu, watu wa kanda ya ziwa alikototea mtangulizi wako nk.

Hakuna aliye shindwa kuelewa kuwa alilengwa Magufuli na kwa vile yeye anamuona mbaya kwake kwani alikataa unafiki wake na ujanja ujanja wa mwanae January.

Ni vile tuu busara za mwenyekiti zilitumika ku sawazisha kauli ile lakini Chama kilikuwa kinasamvaratikia kauli ile baada ya mkutano kwisha.

Huyu mzee ni wa kukaa naye kwa machale, na mbaya zaidi katika hali ya kawaida kuna sifa ya Wasambaa kuwa ni wapenda majungu na unafiki. Najua sio wote lakini majority wako hivyo ni asili yao tuu.

Anyway, kama atasikilizwa basi iwe huko ndani ya CCM yenu ila kama Rais na taasisi hiyo ya kitaifa wajiepushe naye huyo mzee mchumia tumbo maana huyo anayemlinda January ni mtumishi wa umma na uzembe wake unaumiza taifa.
 
JamiiForums428144445_680x453.jpg
 
Nikimtazama Mzee Makamba kwa ujumla, alitawaliwa sana na mihemko ya kitoto muda wote wa ule mkutano wao.

Mfano, alipoanza kumshambulia mwandishi wa habari alipomuuliza kuhusu mgao wa umeme, hapa alipata moto baada ya kuona kipenzi chake aliyembeba mwanae anaguswa, alitawaliwa na hisia kwenye kujibu zaidi ya logic.

Pia, alipokuja kutoa kauli kwamba "wazuri hawafi" hapa napo alikuwa kwenye ule ule muendelezo wake wa mihemko, anajilazimisha kuongea muda mwingi mpaka anajikuta anawakosea wasikilizaji.

Kutoa kauli ya namna ile mbele ya wafiwa ni kosa, ujinga wake wa kudhani anampamba Samia, akajikuta anawakosea wengine, na ndio maana Samia kwa kutambua ukosefu wake akaja na majibu kwamba "kati yetu hakuna ambaye hajafiwa" akijua wazi kauli ya Makamba itakuwa imewaumiza wafiwa waliokuwepo pale.

Kitendo chochote cha kujaribu kumtetea Mzee Makamba, ni kuleta ushabiki tu, hakina logic yoyote ndani yake, na wala kosa lile halihitaji kutafutiwa sababu nyingine yoyote nje ya pale kama kuleta siasa nk.
 
Tutofautishe kati ya Uzee na Makamba.

Halafu tukumbuke pia kuwa uzee haumaanishi busara na hekima. Hivyo ni vipawa ambavyo hata wasiokuwa navyo nao pia hupata fursa ya kuzeeka.

Kwa hiyo siyo kila aliyezeeka ana vipawa hivyo. Inaweza ikawa kinyume chake.
 
Tutoke vp sasa kwenye huu mkwamo?
Pengine kabla ya nyumba yetu hatujaipa muonekano mzuri wa nje lazima kuteketeza viroboto na kunguni wanaotutafuna ndani.
Watu kama Zitto na wafuasi wake ndani ya upinzani ndio viroboto na kunguni bila kuwateketeza kudhoofika kutaendelea kwani wananyonya damu zetu.
Kisha kuhakikisha hakuna uchaguzi bila katiba mpya na tume huru

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hiki chama cha mambuzi, tunakosa tu upanzani uliojipambanua kupigania ustawi wa wananchi wa Tanzania. La sivyo kingeshatoka madarakani siku nyingi sana.
Ukweli 100%.Wapinzani wa kweli wapo uzunguni kwa mabwanyenye kwenda kuwapigania watanzania. Nonsense
 
Ukweli 100%.Wapinzani wa kweli wapo uzunguni kwa mabwanyenye kwenda kuwapigania watanzania. Nonsense

Hapa ndani wapinzani wanalimwa risasi na kupewa kesi za ugaidi. Usisahau Ni miaka Saba na ushehe upinzani wamepigwa pin kufanya mikutano ya hadhara, hata hiyo mikutano ya ndani masharti ni mengi Sana.

Kama ndani mazingira siyo mazuri Bora tukafanye siasa nje ya nchi. Mbona Bobby Wine kafanya mkutano wa wanachama wake Kenya?. Ipo siku tutaomba kibali kufanya mkutano wa hadhara namanga Kenya.
 
Matukio mawili yaliyo jitokeza kwenye huo mkutano mkuu wenu yameonyesha wazee mastaafu aina ya Makamba hawapo ndani ya CCM kukusaidia bali kulinda maslahi yao na watoto wao kwa kutumia style za uchawa wanazotumia hasa wasanii.

1. Alipokuwa nje ya ukumbi akihojiwa na waandishi, lilipofika suala muhimu la umeme akapandwa na jazba za wazi kuonyesha kumlinda mwanae badala ya kutumia busara kulielezea na jinsi ccm itakavyo isaidia serikali kutafuta utatuzi. Yeye kafanya ni la familia kwa sababu ya mlo wa January na mfanya biashara wa majenereta Mwamvita.

2. Pamoja na Magufuli kuwa na matatizo yake (hasa nje ya ccm) Makamba hakupaswa kutamka maneno mabaya kama yale kuwa wema hawafi katika kipindi hiki kifupi ambacho ndio umeingia madarakani baada ya mtangulizi wako KUFA. Tena mbele ya mjane wa marehemu, watu wa kanda ya ziwa alikototea mtangulizi wako nk.

Hakuna aliye shindwa kuelewa kuwa alilengwa Magufuli na kwa vile yeye anamuona mbaya kwake kwani alikataa unafiki wake na ujanja ujanja wa mwanae January.

Ni vile tuu busara za mwenyekiti zilitumika ku sawazisha kauli ile lakini Chama kilikuwa kinasamvaratikia kauli ile baada ya mkutano kwisha.

Huyu mzee ni wa kukaa naye kwa machale, na mbaya zaidi katika hali ya kawaida kuna sifa ya Wasambaa kuwa ni wapenda majungu na unafiki. Najua sio wote lakini majority wako hivyo ni asili yao tuu.

Anyway, kama atasikilizwa basi iwe huko ndani ya CCM yenu ila kama Rais na taasisi hiyo ya kitaifa wajiepushe naye huyo mzee mchumia tumbo maana huyo anayemlinda January ni mtumishi wa umma na uzembe wake unaumiza taifa.
Ukitaka kumjua huyu mzee kwanini yupo hivyo nenda YouTube andika neno " Cyprian Musiba na Makamba" huko utashiba na utajuwa kinachowatafuna ndugu zetu
 
Back
Top Bottom