Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,358
- 23,760
Ndugu zangu Watanzania,
Hayo ni Maneno ya upendo yaliyotamkwa na Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge katika muendelezo wa Kampeni zake za kusaka kura za Urais kuongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Embu soma hapa 👉Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaomba watanzania kukipa kazi Chama chake ili kikafanye kazi ya kustawisha, kunawirisha na kuheshimisha utu wa Mtanzania pamoja na kuiheshimisha nchi Kimataifa kwa kuwa na Raia wenye maisha mazuri na huduma zote muhimu.
Dkt. Samia ametoa kauli hiyo leo Oktoba 18, 2025 kwenye muendelezo wa Kampeni zake Mkoani Rukwa, Wilayani Nkasi kwenye Viwanja vya Sabasaba, akieleza pia kujipanga Vyema yeye na Chama Cha Mapinduzi katika kumuwezesha mwananchi kiuchumi ikiwemo uendelevu katika utoaji wa Mikopo ya Halmashauri pamoja na uanzishwaji wa mfuko wa Wafanyabiashara wadogo utakaoanza na Mkopo wa Shilingi Bilioni 200.
"Ndugu zangu sisi Chama Cha Mapinduzi kazi yetu ni kufanya kazi, kufanya kazi kustawisha, kunawirisha na kuheshimisha utu wa mtu na ndiyo maana tunasema kazi na utu na niwaombe sana mtupe kura zenu Oktoba 29, chagueni Chama Cha Mapinduzi tukafanye kazi tujenge utu wenu, tuimarishe utu wa Mtanzania na kwa ujumla tuiheshimishe nchi yetu Tanzania kwa watu wake kuwa na maisha mazuri." Amekaririwa akisema Dkt. Samia.
Awali Dkt. Samia amezungumzia kuhusu suala la madai ya fidia kwa wananchi wa Nkasi ikiwemo wananchi waliopisha ujenzi wa barabara ya Kanazi- Kipili, akiwahakikishia wananchi kuwa mara baada ya uhakiki kufanyika wananchi wote watalipwa stahiki zao, akiwashukuru pia kwa kukubali kupisha utekelezaji wa mradi huo wakati wakisubiria fidia zao kutoka serikalini.
Mgombea wa nafasi hiyo ya Urais ameeleza pia kuhusu miradi ya Maji Wilayani Nkasi akisema tayari wameanza mpango wa kutumia maji kutoka kwenye Ziwa Tanganyika, mradi utakaoondoa changamoto ya Maji kwenye Mji wa Namanyere na Wilaya ya Nkasi kwa ujumla.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.