Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 116
- 260
Mwaka 2021 unamalizika kwa kada ya utumishi wa umma kuwa na tabasamu bora la "Muongo". Hii ni kutokana na kero zilizofanyiwa kazi na Rais Samia tangu alipoingia madarakani mapema mwezi March.
Kwa mara ya kwanza chini ya mwaka mmoja kero nyingi za watumishi zimetatuliwa kwa uweledi mkubwa. Katika kupandisha madaraja Rais Samia amesaini zaidi ya vibali 91,000 kwa watumishi wenye sifa.
Ndani ya kipindi cha chini ya mwaka mmoja Rais Samia Suluhu ameweza kutoa fedha kwa madai ya malimbikizo yote ya watumishi. Mwezi Juni pekee watumishi 11,983 walitengewa kiasi cha bilioni 23 kwaajili ya malimbikizo huku bilioni 300 zikienda kwa waliopandishwa madaraja.
Watumishi kulipwa malimbikizo na stahiki zao na kupandishwa kwa madaraja kwa watumishi kumeenda sambamba na kutolewa vibali vya ajira katika sekta mbalimbali.
Neema hii iliyoshushwa na Mh.Rais ndani ya muda mfupi wa uongozi wake inatoa tumaini kubwa kwa watanzania. Mwenyezi Mungu amjaalie Rais wetu siha njema azidi kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.
#SisiTumekubali #kaziinafanyika