Rais Samia, nchi haijengwi kwa kuzurura

Rais Samia, nchi haijengwi kwa kuzurura

Lorenzo Samike

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2021
Posts
1,184
Reaction score
1,914
Mpendwa Mama Samia,

Nchi hii haiwezi kujengwa kwa kuomba omba. Nchi inajengwa kwa kazi, bidii, na nidhamu ya utumishi wa umma.

Nchi yetu imebarikiwa kila aina ya rasilimali: Maji, Mito, Mabwawa makubwa, maziwa, madini ya kila aina, gesi, mafuta, chakula, nishati, ardhi kubwa yenye rutuba, nguvu kazi watu, mbuga, misitu, na kila aina ya rasilimali.

Kwa mambo hayo yote, hatuwezi kubabaikia wawekezaji. Wao ndio wanapaswa kutubabaikia sisi.

Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza. Kama tunavyo vitu vizuri, lazima waje wenyewe. Hizi ni basic principles za uchumi.

The Higher they demand, the better the price we get.

Unapojitembeza hovyo kwa wazungu kila kukicha wewe uko angani unaonekana Rais wa bei nafuu tu... Hamna watakachokupa zaidi ya kukutwika dozi za machanjo ya corona.

Halafu pia huko kuzunguka kwenda Ulaya mimi sijaona lolote la maana zaidi ya kunywa JUISI na wazungu tu na kuongea nao VIINGEREZA VISIVYOELEWEKA unabaki kuitikia tu YES YES YES YES YES... huku unatikisa kichwa kana kwamba unawaelewa kumbe hamna lolote!

Ukimaliza kunywa JUISI Ulaya unarudi unatuambia umetoka kutafuta wawekezaji!!!!!!

Hatuwezi kuendelea kama nchi kwa kuabudu wazungu. Lazima tutambue thamani tuliyo nayo na tujifunze kujitegemea. Itatuongezea potential.

Hii dependency syndrome inaua nchi. Ndio maana mnakabidhi wachina bandari kwa miaka hamsini na kwa bei chee ya kitapeli. Ati wahisani!!

Hatuwezi kuwa maomba omba milele. Jenga nchi! Tuache kuzurura hovyo!
 
Kunawanaoamini
1. Mwanamke akisimama imara pembeni yake pana mwanaume (and vice versa)
2. Mwanaume/Ke anaweza akasimama imara bila ya jinsia nyingine
 
Mkuu, hii mbegu (ya kuukataa utumwa na utegemezi), hata ikiota kichakani matunda yake lazima wajukuu wetu wayafaidi milele.
 
Hata waliojificha kipindi cha covid19 hakuna kilichobadirika zaidi ya kuzalisha waliokuwa wakizunguka na msafara wa magari mengi na ulinzi mkubwa kwa gharama kubwa kila siku kanda ya ziwa nini kilibadirika nchini. Tulieni enzi zile zimekwisha fanyeni kazi dezo kwenu basi.

Mama safiri tu matunda tunayaona kama hawataki wahame nchi zipo nyingi.
 
Mpendwa Mama Samia,

Nchi hii haiwezi kujengwa kwa kuomba omba. Nchi inajengwa kwa kazi, bidii, na nidhamu ya utumishi wa umma
Katika watu wapuuzi wewe jamaa unaonekana kama kabisa unachuki binafsi na hujui unachotaka kuongea. USA nchi tajiri inaitwa wawekezaji nchi kama UAE wanakila kitu ila kila leo wanaweka sera rahisi kuvuta wawekezaji. Unataka kuleta mambo ya miaka 80 hapa hatutaki kuomba tukabaki hata mishahara hatuwezi kulipa.

Uchumi wa dunia umekuwa kama kitu kimoja athari ikitokea kusini basi kaskazini wanapata athari. Kweli tuna kila kitu je tuna mtaji? sisi tuna mali wao wanamitaji na mitaji sio pesa tu na technology unaweza kuwa na Gas lakini kuchimba huwezi kiufundi wala kipesa.

Tulikuwa na Rais hapa miaka 5 kakaa tu nini kilifanyika tunajenga na pesa zetu leo siri zote hadharani ni mikopo. Nchi inakusanya 1.2 kwa mwezi hapo ukitoa mishahara ya wafanyakazi 570 billion bado gharama za kawaida pesa ya maendeleo itoke wapi?

una budget ya 32 trillion wakati makusanyo 18 trillion sasa 12 zitoke wapi.
 
Mpendwa Mama Samia,

Nchi hii haiwezi kujengwa kwa kuomba omba. Nchi inajengwa kwa kazi, bidii, na nidhamu ya utumishi wa umma...
Hivyo ulivyovitaja vimekuwepo miaka yote, hata kabla ya kuasisiwa kwa Tanganyika, mbona havijaibadili nchi?

Rasilimali kubwa kuliko zote, ipo kichwani, wala siyo idadi ya fisi au nyumbu, wala siyo maziwa au ardhi ya kilimo, siyo madini wala gas iliyopo chini ya ardhi.

Tanzania haifikii hata 25% ya rasilimali asilia ziluzopo DRC, lakini DRC ni miongoni mwa mataifa 5 Duniani yanayoongoza kwa umaskini.
 
wao wanamitaji na mitaji sio pesa tu na technology unaweza kuwa na Gas lakini kuchimba huwezi kiufundi.
You are so stupid like the incarnated version of Hangaya herself.

Kwahiyo tutakuwa tunawategemea wazungu kwa technology mpaka mwaka gani?

Baada ya miaka sitini ya uhuru, nilifikiri kwamba hii nchi tayari ingekuwa na wasomi ambao wana ujuzi na ufundi wa kushughulikia rasilimali za nchi?

Are you not ashamed of yourself to speak and write such rubbish!?

Jifiche kabisa, ingia uvunguni! FICHAMA. Unatia aibu.
 
Tanzania haifikii hata 25% ya rasilimali asilia ziluzopo DRC, lakini DRC ni miongoni mwa mataifa 5 Duniani yanayoongoza kwa umaskini.
Ni kwa sababu ya wapuuzi wachache kama nyie ambao mpo kwa ajili ya kutafuna nchi badala ya kujenga nchi.
 
Back
Top Bottom