Rais Samia, kwanini kwenye hotuba yako UN umeshindwa kuinadi Tanzania?

Maneno Meier

JF-Expert Member
May 12, 2013
2,469
1,697


Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwako Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumbadilisha waziri wa ujenzi na uchukuzi, Waziri Chamriho, ambaye kwa mtanzamo wa wengi hatukuona nini anakifanya kwa kupewa majukumu makubwa yale ya kuiongoza wizara yetu nyeti ya Ujenzi na Uchukuzi.

Kwa uamuzi huo ambao Mama umeuchukua wa kufanya hayo mabadiliko ya mawaziri, imekuwa faraja kubwa sana kwetu na hivyo ni mategemeo yetu kuwa waziri aliyepewa hiyo dhamana sasa, ataleta msukumo mkubwa wa maendeleo ambayo yatatoa matokeo chanya tunayo yategemea.

Nikirudi kwenye mada yangu yenye umuhimu wa kipekee kwa siku hii ya leo ningependa kwanza kukupa pole kwa uchovu wa safari yako iliyo kugharimu kutuwakilisha huko UN.
Mbili ni kuhusu hotuba yako uliyoitoa kwenye mkutano mkuu wa UN.

Kwenye mkutano wako leo wa mapokezi umegusia hizo Agenda nne ambazo mlizizungumzia kwenye vikao vyenu huko UN, lakini sijaelewa bado kwanini ulipo pewa jukwaa la kujinadi, speech yako ikawa ile ile ya mambo ambayo mlikwisha yazungumza kwenye vikao vyenu? Kwanini hukutumia nafasi hiyo kuinadi nchi yako kisawasawa?

Mama, kumbuka kuwa kwa kipindi cha miaka takribani sita hivi, wakati ule ukiwa Makamu wa Rais kwenye serikali ya Kipenzi chetu Hayati Rais Magufuli, mmefanya mambo mengi sana makubwa ya kiuchumi ambayo yalistahili kusikiwa na wengi duniani.

Kwa nchi ambayo wao wana i-categorize kama developing country, mafanikio ambayo mmeyapata katika kipindi kifupi cha miaka sita tu iliyopita, sio mchezo. Ulitakiwa kuyatoa kwenye speech yako huko UN.

Kwenye majukwaa kama hayo mama ndiyo mda wa kuyanadi mafanikio yako kama kiongozi na pia kuiweka nchi yako ionekane positive kwenye maswala ya uchumi ili kuwavutia wawekezaji unao wataka.

Ulipozungumzia mambo ya utalii, kwa mfano sikujua kwanini hujachomekea mambo makubwa positive ambayo wewe na mtawala mwenza, Hayati Rais Magufuli mmeyafanya katika ku-boost hili swala la utalii nchini?

Nilitegemea ungeelezea measures ambazo mmechukua kwa pamoja katika kudumisha na kuboresha sekta ya utalii ili kuongeza ufanisi katika huduma na comfort kwa watalii na vile vile kuongeza idadi ya watalii nchini.

kununua ndege 11 kwa mkupuo na kujenga Airport mpya kubwa ya kimataifa Dar es salaam na Airports nyingine katika kila mkoa na hasa mikoa yenye vivutio vingi vya kitalii, ili kurahisisha usafiri wa anga kwa watalii na wananchi kwa ujumla, ni mambo makubwa sana ambayo ulimwengu ulipaswa kuyasikia

Katika hotuba yako hiyo ungeweza hata kuonyesha picha za miradi hiyo mikubwa mliyo ifanya na hayati Rais Magufuli na pia picha za mbuga zetu za wanyama kama Serengeti na Ngorongoro na kuunadi mlima wetu wa Kilimanjaro ili watu wausikie na kuuona.

Miradi mikubwa ya SGR na Bwawa la Nyerere na malengo yake na faida kubwa tunazo zitegemea kuzipata, pia ni mambo ambayo ulitakiwa kuwabwagia.

Miradi mingine ambayo ingekuwa muhimu pia kuisemea ni miradi ya barabara za lami za mikoa kwa mikoa, wilaya kwa wilaya na usambazaji wa umeme na barabara mpaka vijijini na mafanikio yake.

Ujenzi na ufufuzi wa meli zetu kwenye maziwa yetu makubwa Victoria, lake Tanganyika na lake Nyasa/Malawi ili kurahisisha usafiri wa majini.

Sikuona umuhimu wa hotuba yako yote kujaa mambo yanayo husu COVID 19 na vaccination? Mambo ya kutajataja chanjo kila wakati ni kuyatengenezea makampuni yao sifa na kuwaletea faida ambazo wao wanazitumia kutunyanyasa sisi kwa kutuona sisi ni masikini na hatuwezi kitu.

Ilitakiwa utoe maelezo kidogo tu juu ya COVID 19 pandemic na chanjo yao. Sifa kubwa ungezitoa kwa hatua ambazo nchi yetu au serikali yako ilizichukua kupambana na awamu mbili za kwanza za COVIDI 19 za kutumia dawa zetu za asili kama kupiga nyungu na kadhalika, kwani kipindi hicho ulimwengu haukuwa na vaccines bado na Lockdown ingeweza kuathiri maisha ya watanzania.

Hapa Rais wangu ulitakiwa ujigambe kwa kuuonyesha ulimwengu kuwa tulipita kipindi hicho kwa ubunifu wetu na ndiyo maana hatukupoteza maisha ya watu wetu wengi kama huko kwao. Ungewakandia ile vibaya na kuonyesha kuwa sio kila mawazo yanayotoka kwao yanabaraka za Alah kwa wana ulimwengu, hata sisi tuna uwezo wa kutumia akili zetu pia.

Hii platform ilikuwa pia fursa ya kwako Rais kuzitangaza rasilimali zetu kama Gas asilia, chuma, boxite, Gold, diamond, na rare Gas Helium na kuonyesha jinsi gani tumejitahidi kufungua kiwanda chetu wenyewe cha kuchakachua dhahabu Mwanza na kwamba tuna mpango wa kufungua kiwanda cha kuchakachua Gas yetu asilia LNG na kujenga reli ya kwenda kwenye machimbo yetu ya chuma, Mchuchuma na Liganga, kwa ajili matumizi yetu na kuitafutia soko dunuani.

Nimesikitika jinsi Rais wetu ulivyo kwenda kinyonge na kukubali kuzungumza Themes ambazo wao wanataka kuzisikia kutoka kwenye mataifa ya watu wasio jiamini.
Mambo ya Gender, Demokrasia na Multilateralism kwa mfano haikuwa wakati wake kwenye stage.

Kuhusu maswala ya uhuru wa haki, wenyewe wanajua kuwa sisi tuko piecefull na ndiyo maana tumekuwa na Rais wa kwanza mwanamke bila mbinde.

Haya makachero au kwa kiswahili kizuri vibaraka wa wazungu, akina Lissu, Lema, Maria Sarungi, Shangazi Fatma Karume na wengineo achana nao, hawana market tena kwa wazungu. Wamesha tupwa na ndiyo maana unawasikia kila mara wanalialia kutaka kurudi Tanzania.

Nguvu yao kubwa nafikiri umesha itambua ni Kenya. Kenya kuna mitambo yote ya kibepari ya kuwa-undermine watanzania na wa Uganda. Wakenya wengi hasa kwenye uongozi hawana interest ya kuona hizi nchi mbili zinapiga hatua kuliko nchi yao. Na ndiyo maana uliona hili tukio la hivi juzi la Mr Alkael Mbowe la kutaka kuamsha dude la maandamano ya kudai katiba huko Mwanza baada ya kuwa mda mrefu Kenya.

Waasi wote wa Tanzania wanapitia Kenya. Bila Kenya au tuseme Kenya ingekuwa na msimamo wa kujiamini, nafikiri hawa watu wasingekuwa na support kubwa.

Ndiyo maana ombi langu kwako Mama, kuwa makini sana na wakenya. Kama hawa watu walidiriki kumsaliti Mwasisi wetu baba wa Taifa Mwalim Nyerere, itakuwa wewe?

Siasa za Rais Mstaafu Kikwete ningekuomba achana nazo. Hazitakufikisha mbali. Na wala Rais Kikwete hataingia kwenye records ya watanzania kuwa ni Rais ambaye amefanya mambo makubwa kwa watanzania na nchi yake. Rais Kikwete alijali sana kukutana na wazungu juu kwa juu, kitu ambacho kili wa-cost watanzania maisha yao.

Mama usionyeshe tabia ya kumkana Hayati Rais Magufuli, wewe yaendeleze yake na fanya yako mengine mapya. Tabia ya kumkana Hayati Magufuli inaweza ikaku-cost. Watanzania wengi bado wanampenda sana Magufuli.

Endelea kuwapenda na kuwajali watanzania wenzako. Shirikiana na watendaji wako kuhakikisha kuwa rasilimali zetu zinaleta maendeleo ya watu na ya vitu. Watanzania tunataka matumaini ya maisha mazuri na upendo. Hatutaki matatizo yasio na mguu wala kichwa. Matatizo yatakayo tu-cost sisi kuvunja amani, umoja na undugu wetu hatuyataki.

Tunataka matumaini ya uchumi wa kila mtu.
 
Wewe ni mpuuzi kabisa,fanya utafiti utaona mchango wa jakaya,pia isome hotuba ya samia utaona jinsi alivyoisemea nchi yake

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Hutuba ya samia imejikita kuomba TZ iletewe misaada ya chanjo kwa wingi wakati kwenye zile chanjo million moja tulizoletewa tumeweza kutumia chanjo laki tatu tu 🤣
 
Wewe ni mpuuzi kabisa,fanya utafiti utaona mchango wa jakaya,pia isome hotuba ya samia utaona jinsi alivyoisemea nchi yake

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Ondoa upumbavu wako hapa. Jakaya alifanya nini zaidi ya kushamiri kwa ufisadi na madawa ya kulevya? Wizi wa kimikakati mikataba ya kipumbavu hadi ccn kukataliwa na watu haikuwa kwa ajili llya jakaya? Mama amesema nini quantitatively kwa ajili ya taifa?

Kama na wewe uwezo wako unaishia hapo, acha kuasambaza haurfu ya uozo hapa.
Tanzania deserves more intellectual abilities than upumbavu wa level sifuri zako.
 
Nimekupata vizuri mkuu je, Kama taifa tufanye Nini?
Yapo mengi ya kufanya moja wapo ni nguvu na muda unaotumika kwa kila mtu kujifanya kujua majukumu ya mwenzake yanapaswa yatimizwaje,nguvu hiyo itumike kwa kila mtu kutimiza majukumu yake kama ipasavyo,smart phone zimeleta wataalamu wasiokua wataalamu,kila mtu anamlalamikia mwenzake,so watu wote tunalalamikiana,na muda nao haumsubiri mtu!
 
Ondoa upumbavu wako hapa. Jakaya alifanya nini zaidi ya kushamiri kwa ufisadi na madawa ya kulevya? Wizi wa kimikakati mikataba ya kipumbavu hadi ccn kukataliwa na watu haikuwa kwa ajili llya jakaya? Mama amesema nini quantitatively kwa ajili ya taifa?

Kama na wewe uwezo wako unaishia hapo, acha kuasambaza haurfu ya uozo hapa.
Tanzania deserves more intellectual abilities than upumbavu wa level sifuri zako.
Kwani sasa ndiyo Ccm inakubalika ?!
 
Ile hotuba ilikuwa kama ifuatavyo:-
31% ilikuwa ni kujidhiri/kujishusha/kuchuchumaa, 58% kutembeza Bakuli la kuomba misaada ya COVID na 11% kushukuru.
 
Yapo mengi ya kufanya moja wapo ni nguvu na muda unaotumika kwa kila mtu kujifanya kujua majukumu ya mwenzake yanapaswa yatimizwaje,nguvu hiyo itumike kwa kila mtu kutimiza majukumu yake kama ipasavyo,smart phone zimeleta wataalamu wasiokua wataalamu,kila mtu anamlalamikia mwenzake,so watu wote tunalalamikiana,na muda nao haumsubiri mtu!
Kuna mazuri na mabaya yote yanatambulika kwa aliyetimamu. Watu wanajisahau wanachosimamia ni kipi! Wanasimamia ukweli au wanasimamia kipi?

Ikiwa kama tunakubaliana kila binadamu ana ukurasa wa jema na baya inakuwaje watu hawataki kuangazia kwa hayo, na ndiyo tafsiri na ndiyo maana ya kuamrishana mema na kukatazana mabaya.

Sawa Mamlaka imembambikizia Mbowe kesi. Penye uovu tunapaswa kuuonyesha, kuukemea na kukatazana. Lakini linafungamana vipi na kupinga au kukosoa hata lile jema mamlaka ikitenda? Yaani kesi ya Mbowe na mema ambayo mamlaka ikitenda vina mahusiano gani mpaka yanapingwa?

Hii hali ndiyo wanayo CHADEMA hivi sasa, sawa kosoeni mamlaka wanapokosea lakini wanapopatia mnakosoa tena hawa wanasimamia nini? Wanasimamia kama wanachodai na kukitangaza na kujinasibisha nacho ulimwenguni?

CHADEMA hawasimamii haki kama wanavyonadi bali wanasimamia msimamo wao wanaouamini wenyewe na siwapingi kwani ndiyo msimamo wao. Laiti kama wangelikuwa wanasimamia haki wangepongeza hata dogo linalofanywa na serikali. Na ninavyosema hivi simaanishi serikali ipo safi sana.

CHADEMA hawana tofauti na CCM. Utofauti wao ni kuwa bado wao hawajashika dola.

Na ukiwaambia ukweli watakunadi wewe ni Mataga na lugha za kebehi na matusi juu kana kwamba wameambiana jinsi ya kujihami kwao. Twitter wameshaiweka chini ya utawala wao na hii nyendo ndiyo wanaitaka kuikamilisha Jf.

Binafsi hii hali inayokwenda imenichosha na kuingia JF na Twitter naona uvivu hata kuandika kujadili naona uvivu, upuuzi puuzi umekuwa mwingi mno! Tanzania bado hajatokea mpinzani wa kweli.
 
Wewe ni mpuuzi kabisa,fanya utafiti utaona mchango wa jakaya,pia isome hotuba ya samia utaona jinsi alivyoisemea nchi yake

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Unauhakika kaisemea nchi yake? Wengi wameelewa kuwa 70% ya speech yake yote kwenye stage amezipigia debe chanjo zao.

Inaonekana kuwa agenda kubwa ya huo mkutano huko UN ni kuhusu COVID 19 na njia za kuchukua ili kukabilina nao.

Yaani Rais wetu amekubali kuingizwa mzimamzima kwenye kushabikia janga la Corona Virus ambalo pamoja na upuuzi wao wote wa vaccination bado upo tu.

Kwa maana nyingine Rais wetu na wataalam wa nchi yetu wakae kusubiri uamuzi wa wafalme wetu lini sisi nasi tupate kibali cha kutengeneza na kusambaza hizo chanjo za makampuni ya mabepari wao kama akina Bill Gates.

Hiyo ndiyo Agenda kubwa iliyovuma huko na sio kingine.

Sikiliza mkuu UN na Organisations nyingine zote za kimataifa zimebuniwa kwa misingi ya kuzinufaisha nchi za kibepari na mabepari wao. Na ndiyo maana utaona kuwa kwenye huo mkutano theme kubwa ilikuwa kutiana uoga kuhusu COVID 19 ili nchi masikini zikubali kununua hizo chanjo kwa mikopo ambayo itatolewa na aidha World Bank, IMF au ECB.

Kwa maana nyingine ni kwamba hivyo ni vyombo vya mabepari kupiga madeal.
Utasikia tu mda sio mrefu.

Hiyo ni principle na sio mimi.

Msikilize Polepole hapa.
 
Back
Top Bottom