Rais Samia kwa Rais wa Ghana: Kila kitu kipo salama Tanzania baada ya uchaguzi

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
710
Reaction score
1,610
Ya kweli haya ndugu zangu?

Kila kitu pipo shwari baada ya uchaguzi? Mambo yamerejea kama kawaida na uchumi umekua?

=====

"Tanzania tuko watulivu na tuko sawa. Kisiasa, kila kitu kiko chini ya udhibiti baada ya uchaguzi wetu wa Oktoba. Sasa nchi imerejea katika hali ya kawaida na tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida.

Kama mnavyoweza kuona hapa Arusha, kila kitu kiko sawa. Baada ya matukio yale, niliunda Tume ya Uchunguzi ambayo tunasubiri ripoti na mapendekezo yake. Hii itatuongoza kuunda Tume ya Maridhiano itakayotekeleza mapendekezo hayo, na baadaye tutafanya mapitio ya Katiba yetu.

Kiuchumi, tunafanya vizuri sana. Mwaka jana tulikua kwa asilimia 6% na mfumuko wa bei umebaki katika tarakimu moja, tukiwa tunacheza kati ya asilimia 3.5% hadi 4%. Bado hatujafika asilimia 5%.

Lengo letu kuu kiuchumi ni kuleta mabadiliko kupitia kuongeza thamani ya bidhaa na ukuaji wa viwanda. Pia, tunajikita katika kuendeleza rasilimali watu, tukizingatia kuwa asilimia 60% ya nguvu kazi ya taifa letu ni vijana. Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa ajili yao."


Rais Samia amesema hayo wakati wa majadiliano kuhusu ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Ghana yaliyofanyika katika Ikulu Ndogo mkoani Arusha.

Your browser is not able to display this video.
 
well done madam President, Dr.Samia Suluhu Hassan,

you are doing very good job for Tanzanians.
we thank you Mama
 
Tuko sawa kwa utekaji , tuko sawa kulemaza upizani, tuko sawa kwa kumshikilia lissu na wengne, tuko sawa kwa kuuza dhahabu, tuko sawa kwa kutopeana miili izikwe, tuko sawa kuvuruga wakristo, tuko sawa tuko sawa kweli kazi nzur tuko sawa
 
Ingawa sijaelewa mantiki ya kumualika huyo Rais wa Ghana ambae Nchi yake ndio ililaani kile kilochotokea Oktoba 29
 
Hongera amiri jeshi mkuu, wazalendo tunakupenda
 
Anataka maridhiano ya nini .?
Mimi hapo ndo anaponichanganya.
Amegombana na nani?
 


Mama anaongea mambo ya uchumi ya 2025 kabla ya uchaguzi. Mama amezoea uongo
 
Damu za watanganyika hazitowahi kwenda bure hadi haki ipatikane hao wanaomdanganya mambo yamerudi kama kawaida watakuja kumkataa.
 
Kuna kipindi vitu havikuwa sawa ? Afunguke zaidi 😁
 

Labda anazungumzia yeye na familia yake. Kwa kweli Maza hana mpango wa kuomba msamaha kwa yaliyotokea MO29 wala haonekani kujutia kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…