Rais Samia: Kila mzazi achunge mtoto wake kwenye malezi na sio kulaumu Serikali kwa kila kitu

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Rais Samia ameyasema hayo akihutubia kwenye Baraza la Eid ambapo amesema kuna usasa na tunaona ndio maendeleo na ustaarabu, akisema tunatakiwa kwenda na usasa kwa kuendana na tamaduni zetu na kwamba tutunze watoto wetu vile sisi tulitunzwa.

Akaendelea kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa upande wake uli kuokoa kizazi hiki na kuaribiwa pamoja na upotoshwaji na kwamba mambo yasiyotuhusu tuwaachie wenyewe.

Badala ya kupeleka lawama zote kwa serikari kila mzazi anatakiwa kudhibiti alichotoa tumboni.

Akiongeza kuwa, tubuni mbinu za kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa usasa tulionao, kwa kufundisha watoto shuleni na sehemu watakazopatikana sababu watoto wanaelewa.
 
Kama Kawaida sana hilo tuko nalo Mida yote

USSR
 
.......yupo sahihi tu mheshimiwa, taifa bora linaanza nyumbani kwenye familia.....serikali ina nafasi yake katika kushughilika na maadili na nidhamu, tunatambua kuna mahakama, polisi na idara kama ustawi wa jamii, nk, sawa umemuelewa na tutaafanyia kazi wito wake, tutashughulika ipasavyo na wanetu.......
 
Watoto pia wafundishwe kuwa kuiba fedha za umma ni maadili mabovu.
Nani anaweza kuwafundisha watoto kuwa wizi wa mali za umma ni maadili mabovu wakati miaka michache iliyopita, aliekuwa kiongozi, Katibu wake alimuagiza gavana wa Central Bank kuruhusu watu wakwapue fedha toka bank ya umma.

Fedha zilitolewa kwenye masandarusi na hamna alieshikwa kuhojiwa.

Mmoja wa wapigaji akaingia kwenye kutembeza mgao kwa wazeiya wa serikali wengine wakipata 40m, 80m, 400 mpaka kuna mmoja akavuta 1.6bn na akadai ni fedha ya mboga.

Imagine wote hao hawakuchukuliwa hatua. Watoto wanaona, au mtawaambia wafuate mafunzo ya maadili bili kulinganisha wanaokali public office wana-behave vip??

Uzuri watoto wa sasa wanajua ku-google na technology haisahau madhambi yaliyofanywa na yanayofanywa.

Au mnadhani watoto hawafuatilii report ya CAG akionesha SGR wajanja wame-inflate bei/km; ndege ya mizigo wamesikia nini kimetokea.

Kuna kazi kweli kuwafundisha wanetu uadilifu. Unless tuje na new working definition ya uadilifu.
 
Rais Samia ameyasema hayo akihutubia kwenye Baraza la Eid ambapo amesema kuna usasa na tunaona ndio maendeleo na ustaarabu, akisema tunatakiwa kwenda na usasa kwa kuendana na tamaduni zetu na kwamba tutunze watoto wetu vile sisi tulitunzwa.

Akaendelea kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa upande wake uli kuokoa kizazi hiki na kuaribiwa pamoja na upotoshwaji na kwamba mambo yasiyotuhusu tuwaachie wenyewe.

Badala ya kupeleka lawama zote kwa serikari kila mzazi anatakiwa kudhibiti alichotoa tumboni.

Akiongeza kuwa, tubuni mbinu za kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa usasa tulionao, kwa kufundisha watoto shuleni na sehemu watakazopatikana sababu watoto wanaelewa.
Muhimu
 
Nyumbani tumewadhibiti watoto. Mitaani wao waingilie. Kwenye mitandao watu wanapojitangaza au wanapoonyesha uchafu wenye jukumu la kuzuia ni serikali.

Wanaweza kutengeneza sheria ndogo a kuwabana watu wa hivyo.

Serikali haiwezi kukwepa. Asilikwepe hilo.
 
Rais Samia ameyasema hayo akihutubia kwenye Baraza la Eid ambapo amesema kuna usasa na tunaona ndio maendeleo na ustaarabu, akisema tunatakiwa kwenda na usasa kwa kuendana na tamaduni zetu na kwamba tutunze watoto wetu vile sisi tulitunzwa.

Akaendelea kuwa kila mtu anapaswa kuwajibika kwa upande wake uli kuokoa kizazi hiki na kuaribiwa pamoja na upotoshwaji na kwamba mambo yasiyotuhusu tuwaachie wenyewe.

Badala ya kupeleka lawama zote kwa serikari kila mzazi anatakiwa kudhibiti alichotoa tumboni.

Akiongeza kuwa, tubuni mbinu za kukabiliana na mmomonyoko wa maadili kwa usasa tulionao, kwa kufundisha watoto shuleni na sehemu watakazopatikana sababu watoto wanaelewa.

Mtoto anatunzwa na jamii sio mzazi peke yake. Ndo kusema ukienda kazin uwe nae akienda shule ukae nae akienda kucheza mtaani umsindikize? Wewe utaweza? Jamii nzima kwa ujumla wake inajukumu kubwa kwa Malezi na makuzi ya mtoto. Anatakiwa kuiasa jamii anayoiongoza umhimu wa kuona kuwa ni jukumu letu kwa pamoja kwenye malezi ya mtoto.” Mtoto wa mwenzio pia ni mwanao” Busara Ndio nguzo kubwa kwenye kila neno na kauli imtokayo kiongozi.
 
Makampuni na Serikali zitaanza ajiri kwa kupitia huko mitandaoni.

Kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe
 
Mama kaja.....

Ni zama za kuendelea kusimama madhubuti kama taifa bora kwani changamoto za dunia ya UTANDAWAZI NA SOKO HURIA hazikuwepo huko nyuma....

#MamaKaja
#MamaAnaendeleaKunena

#SiempreSSH
 
Nani anaweza kuwafundisha watoto kuwa wizi wa mali za umma ni maadili mabovu wakati miaka michache iliyopita, aliekuwa kiongozi, Katibu wake alimuagiza gavana wa Central Bank kuruhusu watu wakwapue fedha toka bank ya umma.

Fedha zilitolewa kwenye masandarusi na hamna alieshikwa kuhojiwa.

Mmoja wa wapigaji akaingia kwenye kutembeza mgao kwa wazeiya wa serikali wengine wakipata 40m, 80m, 400 mpaka kuna mmoja akavuta 1.6bn na akadai ni fedha ya mboga.

Imagine wote hao hawakuchukuliwa hatua. Watoto wanaona, au mtawaambia wafuate mafunzo ya maadili bili kulinganisha wanaokali public office wana-behave vip??

Uzuri watoto wa sasa wanajua ku-google na technology haisahau madhambi yaliyofanywa na yanayofanywa.

Au mnadhani watoto hawafuatilii report ya CAG akionesha SGR wajanja wame-inflate bei/km; ndege ya mizigo wamesikia nini kimetokea.

Kuna kazi kweli kuwafundisha wanetu uadilifu. Unless tuje na new working definition ya uadilifu.
Ni majuzi tu....

TAKUKURU imeongea na wizara ya elimu kuingiza mitaala ya "KUKURU" katika mifumo yetu ya elimu angali chini.....

Ni hatua mujarabu.....

#SiempreJMT
 
A very good point from Madan President. Maadili yanafundiswa nyumbani. Tusiwaache watoto walelewe na dada wa kazi, TV na mwalimu shuleni.
 
Badala ya kupeleka lawama zote kwa serikari kila mzazi anatakiwa kudhibiti alichotoa tumboni.
Kweli kabisa yaan Sasa hivi mtoto wa kiume kuingiza mwanamke ndani nyumbani kwao na kufanya nae ngono anaonekana ni Dume la Simba, Ila mtoto wa kike akiingiza mwanaume ndani nyumbani kwao na kufanya nae ngono haonekani km Jike la Simba bali anaonekana km Malaya mtarajiwa, inafikirisha sana sijasema Mimi lakini maadili yanaanzia nyumbani

In Chimamanda Ngozi Adchiyes Voice
 
Watoto pia wafundishwe kuwa kuiba fedha za umma ni maadili mabovu.
Sahihi kabisa.

Tumekazania tu ushoga ushoga, lakini ukweli ni kuwa jamii yetu ipo ovyo sana, na ina matatizo mengi:

1) mimba za utotoni na kuzaa ovyo bila mpangilio.

2) wizi na udokozi kila mahali. Wengine wanawatumia watoto kwenda kuiba kwa kuwapitisha madirishani baada ya kukata nondo.

3) Uvivu umetapakaa. Vijana badala ya kufanya kazi wanashinda wanabet.

4) Vijana badala ya kufikiria, kupanga mambo ya maendeleo, wanashinda wanaongelea na kuhadithiana mambo ya mapenzi.

5) Watu ni waongo na wenye hadaa nyingi. Katika mambo 10 anayoongea, 8 ni uwongo.

6) watu wazima, wenye viungo vyote, badala ya kufanya kazi, wamebakia kuzunguka na kuwa ombaomba. Wengine kwa bahati mbaya ndani ya familia akazaliwa mlemavu, badala ya kuchukua jukumu la kumsaidia huyo mwanafamilia mlemavu, wanamgeuza kuwa mtaji wa biashara. Wanashinda kutwa nzima wanamzungusha kila mahali kuomba pesa.

7) Watu kujivunia uovu badala ya wema. Hujasikia watu wakisema kuwa, fulani ameitumia nafasi yake vizuri sana, na sasa hivi ni tajiri? Na wakati fulani wengine wakisema, fulani kwa nafasi aliyo nayo asipotoka kimaisha itakuwa ni uzembe wake? Huko kutumia nafsi vizuri, wanamainisha asipoiba au kula rushwa. Na hup uzembe wanaosema ni mtu kutoiba. Yaani mwizi ndiye anaonekana kuwa na akili.

8) baadhi ya mabinti nao baadhi huwa wanafikia kusema kuwa eti binti fulani kwa umbile lile akiwa maskini ameamua mwenyewe. Wanachomaanisha ni kuwa umbile lake ni la mvuto kwa wanaume, hivyo afanye umalaya kuweza kupata pesa.

9) Fikiria madereva wa magari ya Serikali na makampuni, wengine hunyonya mafuta yaliyopo kwenye magari wanayoyaendesha na kwenda kuyauza. Wengine huvua matairi na kuyauza. Halafu wanavalisha matairi yaliyochoka, na kwenda kudai mapya kwa waajiri wao.

10) Maofisa wa Serikali wanatengeneza invoices za uwongo, wanatengeneza safari wakilenga posho, watu wanagombea ubunge ili wateuliwe kuwa mawaziri, na wakiwa mawaziri, biashara zao zisiguswe, n.k.n.k.

Jamii ya namna hii, ni jamii iliyooza kimaadili. Kwa hiyo hata huo ushoga ukiongezeka itakuwa ni kuongezea katika uozo uliopo.
 
Serikali lazima ilaumiwe kwasababu ndiyo inayoruhusu kuingizwa kwa mikataba mingi yenye masharti kuhusu watoto.
Kwenye suala la malezi ni kweli wazazi wanahusika kwa asilimia kubwa. Ingawaje serikali haipaswi kujitoa kwani ndiyo hasa inayodhibiti jamii yake kwenye masuala ya maadili. Mfano kuzuia wasanii wanaoimba nyimbo zisiszo na maadili ya kitanzania na wanaovaa mavazi yasiyo ma staha.
 
Ni kweli Mama Samia, wazazi tusilee watoto tukiigiza uzungu mwingi.
Rais yuko sahihi, hilo liko wazi. Kwa upande mwingine watoto wetu wanatumia muda mwingi zaidi mashuleni, pengine kuliko hata nyumbani isipokuwa siku za mwisho wa juma. Sasa huko mashuleni na kwenye mitandao wazazi watafanyaje kudhibiti makuzi na maadili ya watoto. Inavyoonekana tatizo ni mtambuka na sote itabidi kushirikiana katika kulidhibiti.
 
Back
Top Bottom