Rais Samia, jumba bovu humwangukia wa mwisho

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,796
Reaction score
18,053
Rais Samia, kwa nafasi yake, amejitahidi katika mengi, kaharibu katika machache, lakini yaliyo ya msingi:

1) Amejitahidi kuhimiza mazingira rafiki ya uwekezaji lakini kahimiza kwa mdomo. Mwekezaji makini hawezi kuzingatia. Rais, nenda katazame sheria na sera ya uwekezaji. Ukaweke msingi huko. Tunatakiwa kuwa na sheria rafiki ya uwekezaji, isiyobadilika ovyo ovyo, isiyoweza kuchezewa ovyo ovyo na Rais, kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya 5.

2) Amejitahidi kuhimiza haki za msingi bila kugusa sheria, na hapo inaonekana ni usanii, blabla na unafiki. Kama tunataka nchi yetu iwe nchi inayojali haki, demokrasia na uhuru wa watu, ni lazima kurudi kuitazama katiba na sheria zetu. Lazima tuangalie sheria iliyounda Jeshi la Polisi maana kwa sasa taasisi hii ndiyo inayoongoza kwa kuvunja sheria na kukanyaga haki za msingi za raia. Lazima kuangalia sheria iliyounda mahakama, TISS, DPP, na Bunge. Taasisi hizi badala ya kuwa huru, kwa sasa zinafanya kazi kama taasisi vikaragosi vya Serikali na Rais.

3) Rais kajitahidi kufanya mabadiliko madogo madogo lakini ameamua kuning'inia kwa miguu juu ya kamba nyembamba inayotenganisha haki na dhuluma. Anataka asiangukiwe na jumba bovu lililojengwa na awamu ya 5, lakini ameendelea kusimama ndani karibia na mlango wa jumba bovu. Hujuma na uovu dhidi ya makomandoo, Mbowe, wanaoitwa wahujumu uchumi, ni jumba bovu lililojengwa na awamu ya 5, Rais amesimama ndani ya jumba bovu, karibia na mlango wa kutokea, kuta za jumba bovu zinaendelea kumeguka, naye anapiga kelele kuwa karibu litaniangukia, lakini hatoki nje ya jumba bovu. Mh. Rais Samia, ukitaka usidondokewe na jumva bovu, toka nje ya jumba hilo bovu, liache lianguke, ujenge nyumba imara. Rais akumbuke kuwa uongozi ni mbio za kupokezana vijiti, mkimbiaji anayesifiwa sana au kukaumiwa, ama kwa kupata au kokosa ushindi ni yule aliyepokea kijiti mwishoni na kuhitimisha mbio. Uovu, ubaya na uzuri wa mbio zinazoendelea sasa, au utakupa heshima na sifa wewe au kukuharibia heshima na sifa wewe, hata kama makosa yalifanywa na aliyeanza kukimbia.

Rais Samia, kama una dhamira njema , nenda zaidi kwenye mambo ya msingi, huko ndiko utumie muda na akili yako zaidi. Jenga mfumo utakaozuia Polisi kuwa chombo cha ugandamizaji, jenga mfumo utakaoifanya mahakama iwe huru, iongozwe na watu waadilifu na wenye weledi kuliko ilivyo sada, na itende haki. Jenga mfumo utakaozuia DPP kumfungulia mtu yeyote kesi, bila kujali mtu huyo ni mhalifu au mtu mwema. Jenga mfumo utajaowezesha kuwa na Bunge huru lenye wabunge wenye uwezo na weledi, kuliko hawa ambao kwa kiasi kikubwa ni wateule wa watu watatu, Jenga mfumo utakaozuia Rais kuingilia na kuzifanya taasisi zilizotakiwa kuwa huru, kuwa mali yake binafsi.

Jumba bovu unaloishi ndani yake, ni mifumo mibaya ya utawala. Madamu ni jumba bovu, lazima litakuangukia. Hatujui ni lini, lakini usipotoka humo, tuna uhakika litakuangukia.
 
Hivi hamuwezi andika nyuzi fupi makini ya kumtetea kuliko hili gazeti refu kiasi hiki?,busara zero?
User mpya hii kwa kazi maalumu
 
Ujinga ni kufikiria hakuna anayeweza kuwaza chochote bila ya kumuegemea kiongozi fulani.

Mimi ni User Mpya! Kazi maalum! Ipi hiyo? Fuatilia ili utambue kama nimewahi kuwa mpambe wa mtu. Mimi ni mpambe wa kudumu wa weledi.

Kama uwezo wako wa kusoma ni mdogo, pita tu, waachie wanaoweza kusoma kwa kuangalia mantiki na siyo ufupi au urefu wa mada.
 
Rubbish
 
Rais anatakiwa awe na "thick skin" ajue hiyo nafasi yake itamletea lawama lazima awe tayari kukabiliana nayo, habari ya "ukinizingua tutazinguana" kwa sababu tu mpinzani katoa maoni yasiyompendeza ndio aamue kumsukumia kesi ya uongo kwasababu tu ya mamlaka aliyonayo hilo halikubaliki, na ni dhambi mbele za muumba, kuchezea haki ya mtu ni kujitafutia laana.
 
Ukiona hivyo Ujumbe unachoma. Jumba bovu huko ccm.wanataka kulikimbia wote
 
Rais anatakiwa awe na "thick skin" ajue hiyo nafasi yake itamletea lawama lazima awe tayari kukabiliana nayo, habari ya "ukinizingua tutazinguana" kwa sababu tu mpinzani katoa maoni yasiyompendeza ndio aamue kumsukumia kesi ya uongo kwasababu tu ya mamlaka aliyonayo hilo halikubaliki, na ni dhambi mbele za muumba, kuchezea haki ya mtu ni kujitafutia laana.
Kama kuna kosa kubwa alilolifanya Samia, ni wa kukubalia waliojenga jumba bovu, kumbambikia kesi Mbowe na wale makomandoo. Hapa maana yake ameamua kuingia ndani kuishi kwenye jumba bovu lililojengwa na marehemu.
 
Rais Samia, kwa nafasi yake, amejitahidi katika mengi, kaharibu katika machache, lakini yaliyo ya msingi:

1) Amejitahidi kuhimiza mazingira rafiki ya uwekezaji lakini kahimiza kwa mdomo. Mwekezaji makini hawezi kuzingatia. Rais, nenda katazame sheria na sera ya uwekezaji. Ukaweke msingi huko. Tunatakiwa kuwa na sheria rafiki ya uwekezaji, isiyobadilika ovyo ovyo, isiyoweza kuchezewa ovyo ovyo na Rais, kama ilivyokuwa wakati wa awamu ya 5.

2) Amejitahidi kuhimiza haki za msingi bila kugusa sheria, na hapo inaonekana ni usanii, blabla na unafiki. Kama tunataka nchi yetu iwe nchi inayojali haki, demokrasia na uhuru wa watu, ni lazima kurudi kuitazama katiba na sheria zetu. Lazima tuangalie sheria iliyounda Jeshi la Polisi maana kwa sasa taasisi hii ndiyo inayoongoza kwa kuvunja sheria na kukanyaga haki za msingi za raia. Lazima kuangalia sheria iliyounda mahakama, TISS, DPP, na Bunge. Taasisi hizi badala ya kuwa huru, kwa sasa zinafanya kazi kama taasisi vikaragosi vya Serikali na Rais.

3) Rais kajitahidi kufanya mabadiliko madogo madogo lakini ameamua kuning'inia kwa miguu juu ya kamba nyembamba inayotenganisha haki na dhuluma. Anataka asiangukiwe na jumba bovu lililojengwa na awamu ya 5, lakini ameendelea kusimama ndani karibia na mlango wa jumba bovu. Hujuma na uovu dhidi ya makomandoo, Mbowe, wanaoitwa wahujumu uchumi, ni jumba bovu lililojengwa na awamu ya 5, Rais amesimama ndani ya jumba bovu, karibia na mlango wa kutokea, kuta za jumba bovu zinaendelea kumeguka, naye anapiga kelele kuwa karibu litaniangukia, lakini hatoki nje ya jumba bovu. Mh. Rais Samia, ukitaka usidondokewe na jumva bovu, toka nje ya jumba hilo bovu, liache lianguke, ujenge nyumba imara. Rais akumbuke kuwa uongozi ni mbio za kupokezana vijiti, mkimbiaji anayesifiwa sana au kukaumiwa, ama kwa kupata au kokosa ushindi ni yule aliyepokea kijiti mwishoni na kuhitimisha mbio. Uovu, ubaya na uzuri wa mbio zinazoendelea sasa, au utakupa heshima na sifa wewe au kukuharibia heshima na sifa wewe, hata kama makosa yalifanywa na aliyeanza kukimbia.

Rais Samia, kama una dhamira njema , nenda zaidi kwenye mambo ya msingi, huko ndiko utumie muda na akili yako zaidi. Jenga mfumo utakaozuia Polisi kuwa chombo cha ugandamizaji, jenga mfumo utakaoifanya mahakama iwe huru, iongozwe na watu waadilifu na wenye weledi kuliko ilivyo sada, na itende haki. Jenga mfumo utakaozuia DPP kumfungulia mtu yeyote kesi, bila kujali mtu huyo ni mhalifu au mtu mwema. Jenga mfumo utajaowezesha kuwa na Bunge huru lenye wabunge wenye uwezo na weledi, kuliko hawa ambao kwa kiasi kikubwa ni wateule wa watu watatu, Jenga mfumo utakaozuia Rais kuingilia na kuzifanya taasisi zilizotakiwa kuwa huru, kuwa mali yake binafsi.

Jumba bovu unaloishi ndani yake, ni mifumo mibaya ya utawala. Madamu ni jumba bovu, lazima litakuangukia. Hatujui ni lini, lakini usipotoka humo, tuna uhakika litakuangukia.

Ngoja tuone ..
 
Back
Top Bottom