GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,659
- 128,083
"Siko tayari kukubali niangushiwe Mzigo wa lawama wakati Madhambi yalifanyika katika Awamu zilizopita" Rais Samia jana alipokuwa Bandarini ambapo pia kwa Hasira zake Kali alizokuwa nazo aliivunjilia mbali na Bodi ya Bandari (TPA)
Rais wangu Samia sasa kwa mfano ukisema kuwa usihusishwe na Madhambi ya Awamu zingine kwani Wewe hukuwa sehemu ya Awamu ya Tano ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kama Makamu wake wa Rais?
Rais wangu Samia kwa mfano ukisema kuwa tukome Kukuhusisha na Madhambi ya Awamu zilizopita je, siyo Wewe ambaye katika Awamu ya Nne ulishawahi hadi kuwa Waziri? Je, Waziri siyo sehemu ya Serikali na Waziri siyo Msaidizi Mkuu wa Rais wa nchi Kiutendaji katika Wizara aliyomteua?
Rais Samia ni nani labda amekudanganya kuwa tokea uwe Rais wa Kumalizia Awamu ya Tano ya Hayati Rais Dkt. Magufuli ( japo Wewe unatulazimisha tutambue ni Rais wa Awamu ya Sita ) hakuna 'Madudu' yanayotendeka?
Hivi Rais Samia kwa mfano Mtu kama Freeman Mbowe Kukamatwa akidaiwa ni Gaidi mpaka Wazungu ( unaozunguka Kwao kuwatembezea Bakuli na wanakupa Hela za Masharti wanakushangaa ) hii haiwezi Kutafsiriwa ni sehemu ya Awali ya 'Udhaifu' wa Awamu hii yako?
Na uliponishangaza hasa GENTAMYCINE nj sehemu moja tu kwamba umetupiga 'Mkwara' kuwa tusikutupie Mizigo ya Lawama na Madudu ya Awamu zote zilizokutangulia lakini Wewe huyu huyu Kutwa huachi Kuomba Ushauri kwa Rais wa Awamu ya Nne Mzee Jakaya Kikwete je, hapa tukueleweje labda Mheshimiwa?
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika moja ya Hotuba zake aliposema Ikulu si mahala pa Mchezo si mlidhani alikuwa anatania au hataki muwe huko?
Yaani hata Mwaka Mmoja tu wa Urais bado hujautimiza umeshaanza Kufura kwa Hasira vipi ikipita hii miaka yako Minne si unaweza sasa ukatuchukia Watu wote (akina GENTAMYCINE) ambao tunakupenda Kidhati ndiyo maana tunakukosoa ili ujirekebishe lakini kwa bahati mbaya unatuona Sisi tunakuchukia, tunaichukia Awamu yako na tunatumika na 'Mabeberu' ambao Wewe ukisafiri Kwao kwenda kuwaomba Misaada ( Pesa ) huwa wanakuwa Wazuri Kwako.
Ninamalizia kwa Kukuambia Rais wangu Mpendwa Samia Suluhu Hassan (ambaye najua tuko wote hapa JamiiForums na huwa unanisoma mno tu GENTAMYCINE tena tokea ukiwa Makamu wa Rais) kuwa iepuke kabisa hii Kauli ya Kuwatupia Lawama za Kiutendaji Watangulizi wako.
Bali onyesha Ukomavu (Maturity) kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa Kuyameza Mapungufu yao, Kuyabeba na kuanza Kuyatatua taratibu kwani itakujengea Sifa zaidi Kwetu na watakaokuja watakuiga na hatimaye Taifa kusonga mbele bila manung'uniko (visununu ) tulivyovizoea kama Watanzania (Waswahili) sie.