wankuru nyankuru
JF-Expert Member
- Feb 11, 2019
- 491
- 763
Kumekuwepo na changamoto ya kukatika kwa umeme kwa takribani siku nzima katika Kata ya Moshono iliyopo jijini Arusha Kwa takribani mwezi mzima Sasa.
Sambamba na changamoto hiyo, kumekuwepo pia Kwa changamoto ya maji kwenye kaya za watu kwa takribani wiki ya pili Sasa.
Pamoja na changamoto hizo, wananchi hawajapewa sababu za kuwepo Kwa changamoto hizo.
Hata hivyo, kuna baadhi ya wananchi wamedai kuna uwezekano wa Taasisi za Tanesco na Auwsa kufanya hujuma hiyo kwa maslahi yao binafsi (upigaji). Hivyo uchunguzi ufanyike kubaini tuhuma hizo.
Na kipindi hiki tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ndiyo wanaanza kukata maji na umeme kitendo kinachotafsiriwa kuwa wanakufanyia hujuma.