Mkuu wa Mkoa wa Arusha fanya ziara Kata ya moshono ujionee maji yanavyovuja hovyo

wankuru nyankuru

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
491
763
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella fanya ziara katika Kata ya moshono hususani mtaa wa losirway karibu na msikiti utajionea jinsi maji kutoka Idara ya maji ya Jiji la Arusha ( auwsa) yanavyovuja ( njia panda) na hii ni wiki ya pili tangu yaanze kuvuja na hakuna anayefuatilia.

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamefanya eneo hilo linalovujisha maji kuwa kisima Cha Bure Cha kuchota maji.

Baadhi ya wakazi wanakosa maji kutokana na kuvuja Kwa maji hayo.

Naomba ufuatilie hili mkuu wa mkoa.

Serikali inatumia fedha nyingi kusukuma maji ( kupump maji) alafu yanapotea njiani bila kuwafikia watumiaji ipasavyo kutokana na uzembe wa watumishi wa Idara ya maji ya Jiji la Arusha wa kutofanya ufuatiliaji.


Lakini pia Kuna maji karibu na Mataa ya friends corner Kuna chemba la maji linavujisha maji Kwa wingi sanaa.

Maji hayo yanatiririka Kwa wingi kuelekea soko la samunge ( round about), swali la kujiuliza je Idara ya maji licha ya ofisi zao kuwa karibu na eneo hilo hawajaona/ hawajapata taarifa kuhusiana na hiyo changamoto????.
 
Back
Top Bottom