Mwendawazimu pekee ndiye anaweza kutarajia amani huku akidhulumu haki. Mtu yeyote anayedhulumiwa hawezi kuacha kuipambania haki yake. Anaweza kutulia kwa sabau hana la kufanya, lakini utulivu wa namna hiyo ni mwendawazimu pekee ndiye anaweza kuutafsiri kuwa ni amani.