Rais Samia azindua mfumo wa usafirishaji wa dharura wa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-Mama)

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Aprili 06, 2022 anatarajia Kuzindua Mfumo wa Usafirishaji wa Dharura wa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-MAMA). Uzinduzi wa Mfumo huu muhimu katika kuwasaidia Wajawazito na Watoto Wachanga unafanyika kwenye Viwanja vya Chinangali- Dodoma kuanzia Majira ya Saa 5 Asubuhi hii. Utafuatilia matangazo haya ya moja kwa moja kupitia Televisheni mbalimbali, Radio na Mitandao ya Kijamii. Chini ya Rais Samia, Kazi Inaendelea.

#TunaImaninaSamia
#Hakunakinachokwama
#KaziInaendelea

=========

Anaongea kwa sasa ni Dkt. Festo Ndungange kutoka ofisi ya Rais-Tamisemi na anaongelea uhusika wa wizara yake na mfumo wa M-Mama. Dkt. Festo amepongeza juhudi za Rais kuboresha miundombinu utoaji huduma katika sekta ya afya.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge-Huduma na maendeleo ya Jamii
Stanslaus Haroon Nyongo: Kwa ufupi, kwa niaba ya kamati pamoja na bunge tuna furaha kubwa sana tukikuona wewe ukiwa mstari wa mbele kutoa huduma kwa wananchi wako, tulishuhudia majuzi ulipotutangazia watanzania kwamba umechukua mkopo wa trilioni 1.3, sisi tulifatilia katika kamati yangu na tuliona zaidi ya asilimia 75 ulipeleka kwenye huduma za jamii na hasa mambo mawili, afya na elimu, mheshmiwa Rais tunakupongeza sana kwa hatua yako.

Pia waziri wa afya, Ummy Mwalimu nae alitoa neno ambapo amemshukuru Rais Samia kwa kazi yake ikiwemo kampeni ya kitaifa ya jiongeze tuwavushe salama ikiwa na lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.

Ummy Mwalimu: Mheshimiwa Rais, mimi niseme, upele umepata mkunaji, linapokuja suala la afya ya mama na mtoto, sitamuonea aibu mtumishi wowote wa sekta ya afya ambae hatatizmiza wajibu wake kikamilifu kuhakikisha tunaokoa maisha ya kina mama wajawazito na watoto.

Nape Nnauye: Wizara inaendelea na programu ya miaka mitano ya awamu ya tatu ya mpango wa maendeleo wa Taifa unaosisitiza matumizi ya tehama kwenye kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Katika kipindi cha miaka mitano hususan mwaka 2015-19 sekta ya mawasiliano ya simu nchini ilichangia jumla ya trilioni 13.5 katika mapato ya Serikali pamoja kwamba katika mwaka 2020/21 taarifa za kampuni nyingi bado hazijatolewa rasmi, hata hivyo kampuni ya vodacom imetoa taarifa yake ya mahesabu ya mwaka wa 2020 ambapo katika kipindi hiki imewekeza bilioni 448.5 katika sekta ya mawasiliano.

Hatua hii inaonyesha dalili za kuanza kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta ya mawasiliano na nichukue nafasi hii kuwapongeza Vodacom na kuwaomba wawekezaji wengine katika sekta ya mawasiliano leteni muwekeze mitaji yenu, Tanzania ndio eneo salama la kuwekeza mitaji yenu.

Huduma za kifedha zitokanazo na mawasiliano ya simu mkononi hasa kwa watanzania wengi walio kwenye mazingira magumu ambazo huduma za kibenki hazikuwa zimewafikia hasa maendeo ya vijijini, huduma za kifedha kupitia simu za mkononi imekuwa mkombozi mkubwa.

Tunajua mabenki hayajafika maeneo mengi lakini leo wananchi wengi wanaweza wakatumia huduma za simu za mkononi kama benki, ukiangalia transactions kwenye mifumo hii ya simu za mkononi yamekuwa makubwa kwenye baadhi ya maeneo kuliko hata zile zinazofanyika kibenki na hii inatusukuma kuangalia uwezekano wa kutunga sheria zitakazotambua miamala inayofanywa kwenye simu za mkononi zitambulike kama dhamana na namna ya kufuatilia uchumi wa mtu ili hata kama anakwenda kukopa, kutumia utaratibu huo na akapata fedha.

Tunatambua kuongezeka kwa matumizi ya tehama na mabadiliko ya ukuaji wa teknolojia duniani unapelekea changamoto za usalama za mtandao pamoja na uhitaji wa ulinzi wa taarifa zinazokusanywa kwenye mfumo.

Mheshimiwa Rais, wizara imeendelea kuchukua jitihada mbalimbali wezeshi katika maeneo haya ikiwemo kuratibu mafunzo kwa waendesha mashtaka, wapelelezi na namna ya kushughulikia uhalifu mtandaoni.

Kwasasa tuko hatua za mwisho za mchakato wa kukamilisha utungaji wa sheria wa taarifa binafsi ili kuongeza ulinzi na udhibiti wa taarifa zinazokusanywa kwenye mifumo mbalimbali yaani data protection and privacy act.

RAIS SAMIA: SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI IKAMILISHWE
-
Akizindua Mfumo wa Usafirishaji wa Dharura wa Wajawazito na Watoto Wachanga Jijini Dodoma, Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuhakikisha inakamilisha uandaaji wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi za Watu
-
Kwa upande wake, Waziri Nape Nnauye amesema wapo katika hatua za mwisho za mchakato wa kukamilisha utungaji wa Sheria hiyo ili kuongeza ulinzi na udhibiti wa taarifa zinazokusanywa kwenye mifumo mbalimbali
-
JamiiForums imekuwa mstari wa mbele kuitetea Haki hii ya Faragha ambayo ipo kwa mujibu wa Ibara ya 16 ya Katiba ya JMT

ikulu_mawasiliano~p~Cb_7MqWtJri~1.jpg
 
Safi Sana mama na pongezi lukuki. Taifa lolote linalowapa kina mama na watoto kipaumbele ni taifa lenye maono madhubuti na mustakabali imara uliotukuka.

Ndo maana mataifa yalioendelea Children fest, women second, elderly thed and fourth are dogs (pets). Ya mwisho ni midume.
 
Kwahiyo pets ni bora kuliko midume??
 
Fest and thed umetisha mkuu
 
Kwahiyo pets ni bora kuliko midume??
Ndo hapo mkuu yani sijui swala la IQ Hawa wenzetu wanalitafsir vipi. Unakuta wanambagua muafrika binadamu mwenzako lakini wanawaheshimu mbwa. Kiukweli likija swala la kujiheshimu muafrika na mwarabu tunajitahidi Sana tuna mipaka flani hivi ya kujisitiri na kujiheshimu.

Binadamu mwenye akili timamu hawezi kuishi ndani ya nyumba yake na mnyama kama mwanafamilia. Eti mbwa hadi ana kitambulisho, passport na bima.

Bora tubaki tu na IQ zetu zenye Mushkel.
 
Kwa foleni hii ya Kibaha kuanzia Picha ya ndege Hadi Mlandizi sijui itakuwaje, hasa hasa hapa picha ya ndege maana hakuna mchepuko.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Aprili 06, 2022 anatarajia Kuzindua Mfumo wa Usafirishaji wa Dharura wa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-MAMA). Uzinduzi wa Mfumo huu muhimu katika kuwasaidia Wajawazito na Watoto Wachanga unafanyika kwenye Viwanja vya Chinangali- Dodoma kuanzia Majira ya Saa 5 Asubuhi hii. Utafuatilia matangazo haya ya moja kwa moja kupitia Televisheni mbalimbali, Radio na Mitandao ya Kijamii. Chini ya Rais Samia, Kazi Inaendelea.

#TunaImaninaSamia
#Hakunakinachokwama
#KaziInaendelea

Amekosa kabisa miradi ya kuzindua?
 
Safi Sana mama na pongezi lukuki. Taifa lolote linalowapa kina mama na watoto kipaumbele ni taifa lenye maono madhubuti na mustakabali imara uliotukuka.

Ndo maana mataifa yalioendelea Children fest, women second, elderly thed and fourth are dogs (pets). Ya mwisho ni midume.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Aprili 06, 2022 anatarajia Kuzindua Mfumo wa Usafirishaji wa Dharura wa Wajawazito na Watoto Wachanga (M-MAMA). Uzinduzi wa Mfumo huu muhimu katika kuwasaidia Wajawazito na Watoto Wachanga unafanyika kwenye Viwanja vya Chinangali- Dodoma kuanzia Majira ya Saa 5 Asubuhi hii. Utafuatilia matangazo haya ya moja kwa moja kupitia Televisheni mbalimbali, Radio na Mitandao ya Kijamii. Chini ya Rais Samia, Kazi Inaendelea.

#TunaImaninaSamia
#Hakunakinachokwama
#KaziInaendelea

LEO HAJAMRUSHIA MADONGO MWENDA ZAKE?
 
Safi Sana mama na pongezi lukuki. Taifa lolote linalowapa kina mama na watoto kipaumbele ni taifa lenye maono madhubuti na mustakabali imara uliotukuka.

Ndo maana mataifa yalioendelea Children fest, women second, elderly thed and fourth are dogs (pets). Ya mwisho ni midume.
MKUU ina maana Hakuna hata kiwanda cha kuzindua hadi mambo kama haya!!!?KAZI KWELI !!
 
Back
Top Bottom