ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 79,081
- 84,973
My Take
Samia hajawahi kuwa na Mbambamba ni ahadi na matokeo.
Safari ya kuwafanya wanawake mabilionea wa sekta ya ujenzi imeanza.
---
Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) leo Jumanne Juni 10, 2025 imeweka historia kwa kusaini mikataba minne ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, mikataba iliyolengwa mahsusi kwa ajili ya kuwawezesha wakandarasi wanawake nchini.
Hafla hiyo ya kihistoria imeongozwa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta, huku thamani ya mikataba hiyo ikifikia jumla ya shilingi bilioni 55.
Mhandisi Besta amesema, miradi hiyo inalenga kuboresha barabara ya Ruanda–Nyimbili–Hasamba – Humba yenye urefu wa takribani kilomita 79.8, ambapo kila mkataba unahusu ujenzi wa kilomita tano kwa kiwango cha lami.
Ameongeza kwa kusema kuwa, kazi hiyo imekabidhiwa kwa makampuni manne yaliyoundwa kwa ubia wa wanawake (JV Groups), yakijumuisha jumla ya kampuni 12 zinazomilikiwa na kuendeshwa na akina mama Watanzania.
"Miradi hii si ya matengenezo bali ya kuinua hadhi ya barabara kutoka changarawe hadi kiwango cha lami. Tunashukuru kwa msukumo mkubwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alituagiza kuhakikisha mikataba hii inasainiwa na kusimamiwa kikamilifu ili ijengwe kwa ubora wa hali ya juu," alisema Mhandisi Besta.
Akizungumza kwa hisia kali za shukrani, Rais wa Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania, Mhandisi Judith Odunga, amesema leo ni siku ya kihistoria isiyosahaulika kwa wanawake nchini.
"Ni mwaka 2020 tulipoomba kwa Rais Dkt. Samia kusaidia wakandarasi wanawake. Leo, miaka mitano baadaye, tumesaini mikataba mikubwa ya kihistoria. Tunamshukuru sana mama yetu Rais kwa kutimiza ahadi yake," alisema Mhandisi Odunga huku akishukuru pia Wizara ya Ujenzi, Bodi ya Wakandarasi (CRB), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na TANROADS kwa ushirikiano mkubwa.
Aidha, amebainisha kuwa kila mkataba mmoja unahusisha kampuni tatu, hivyo jumla ya kampuni 12 zitanufaika moja kwa moja na ajira kwa vijana wa maeneo husika zitapatikana kupitia utekelezaji wa miradi hiyo.
TANROADS imeahidi kushirikiana kwa karibu na wakandarasi hao wanawake ili kuwajengea uwezo na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango vya juu, ikiwa ni utekelezaji wa azma ya serikali ya kuwainua wakandarasi wazawa na kuleta usawa wa kijinsia katika sekta ya ujenzi.
Chanzo: TANROADS