Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,354
- 23,760
Ndugu zangu Watanzania,
Siku zote Nawaambieni Ya Kuwa Usishindane na aliyebarikiwa Na Mungu ,usishindane na aliyeinuliwa na Mungu ,usishindane na aliyepewa kibali na Mungu. Aliyepewa kapewa tu, aliyebarikiwa kabarikiwa tu. Hata ungemchukia vipi ama kumpiga vita huwezi kuondoa kibali cha Mungu juu yake.
Kibali cha Mungu hakiondolewi na Mwanadamu ,kibali cha Mungu kikitolewa na kukabidhiwa mtu inakuwa hakuna mwanadamu awezaye tena kukiondoa. Rais Samia ni chaguo la Mungu ,Rais Samia Kainuliwa na Mungu ,Rais Samia kafikishwa hapo alipo na Mungu Mwenyewe.
Kama utakuwa na macho ya rohoni utagundua na kutambua ya kuwa Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kuliongoza Taifa hili.
Sasa Baada ya muda na wakati wote kutajwa na kuzungumzwa na watu wengi kama kiongozi mwenye ushawishi na nguvu zaidi Barani Afrika. Hatimaye Kaendelea Kuonyesha Umwamba wake na umashuhuri wake baada ya kutajwa kuwa Miongoni mwa Wanawake wenye ushawishi na nguvu zaidi Barani Afrika.
Hili halijanishangaza Mimi Binafsi Mwashambwa Lucas kwa sababu natambua kuwa Rais Samia ni Miongoni Kwa watu Kumi wenye nguvu na ushawishi zaidi Duniani Kote. Ndio sababu sote tuliona akiwa mwenyekiti Mwenza katika mkutano uliofanyika kule Paris Ufaransa katika mjadala ambao ulijikita katika kujadili matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.
Tuliona namna Rais Samia alivyoiteka Dunia nzima hasa pale alipoelezea athari za matumizi ya kuni na mkaa namna yalivyo athiri wanawake na hata kusababisha vifo kwa akina Mama . Alieleza uzoefu wake kama Mwanamke na namna wanawake na watoto wa kike ama wasichana walivyo wahanga na waathirika wakubwa.
Jambo ambalo lilifanya Dunia nzima kusimama wima na kumuunga mkono na kuanzisha kampeni za matumizi ya nishati safi ya kupikia. Kwa hiyo ni lazima watanzania Tujivunie Rais wetu na tuendelee kumuunga mkono.
Kama Afrika ingekuwa ni Nchi moja yenye Rais mmoja kwa hakika Rais wetu Mpendwa Mama Samia angechaguliwa kwa kishindo kikuu kuliongoza Bara hili bila ukomo. Hii ni kutokana na ukweli kuwa Kwa sasa amekuwa ndio Sauti ya Afrika na waafrika. Ndio maana tuliona akipewa na kupata mualiko mzito kushiriki katika mkutano wa nchi 20 matajiri Duniani kote . Mkutano uliofanyika kule Brazil .
Tuliona pia akipata heshima ya kualikwa na kutoa hotuba zake katika nchi za Angola ,Namibia n.k. hiyo yote ni kutokana na Afrika na Dunia nzima kutambua mchango wake katika Mapinduzi ya kiuchumi . Kila mmoja anamuona Rais Samia kama Sauti kwa wasio na Sauti na nguvu kwa wasio na nguvu. Kwa hakika Rais Samia ni Nuru na Mwanga wa Afrika . Ndio tumaini la watu wote.
Watanzania wenzangu hatuna Budi kuendelea kumuunga mkono Rais wetu na kumtetea pale wenye chuki binafsi na wivu kwa Rais wetu watakapo jaribu kutaka kumkwamisha Mama yetu.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.