Nchi yetu imepita vipindi vingi, vyote vikiwa chini ya utawala wa TANU na baadaye CCM. Kila lililo jema na lililo baya katika Taifa letu lazima lishikamanishwe na CCM kama chama, japo tofauti zilikuwepo vipindi mbalimbali kutokana na matakwa ya Rais aliyekuwepo katika kipindi fulani.
Kuna tawala, mambo yalikuwa afadhali, kuna tawala mambo yalikuwa mabaya, na kuna utawala mambo yalikuwaabaya sana.
Mimi siyo shabiki wa Rais Samia wala mtu yeyote bali ni shabiki wa kudumu wa nchi yangu Tanzania ambayo kuna watu wanaihangaikia kila siku ili paweahali pema, lakini wapo wanaohangaika kuimaliza.
Ukilinganisha katika vipindi vyote, kipindi hiki, chinibya uongozi wa Samia, kila mmoja akienenda kwa hekima, kuna nafasi kubwa ya kujenga misingi bora mipya kwa Taifa letu katika nyanja zote, yaani kuanzia haki, demokrasia, uhuru wa maoni, na uchumi huru.
Rais Samia siyo malaika, kuna hapa na pale anaweza kutenda yasiyo matarajio ya baadhi yetu, lakini kwa ujumla, chini ya uongozi wa Rais Samia, kuna nafasi kubwa sana ya kuitengeneza Tanzania mpya, yenye mambo mengi yaliyo chanya. Jambo la muhimu tumpe moyo, tushirikiane naye (bila ya kujali tofauti za kivyama) ili kuijenga Tanzania iliyo njema kwa kila Mtanzania. Lakini tusitarajie mabadiliko yote kwa haraka na kwa wakati mmoja. Tujue kila atakalofanya kuna uoinzani mkubwa, na hasa ndani ya chama chake.
Nawasihi viongozi wa upinzani, jengeni ukaribu na ushirikiano na huyu Rais (hamzuiwi kukosoa, kwa staha), kwa lengo moja tu , ili Rais katika katika kipindi chake cha uongozi, amalize akiwa ameweka misingi imara maeneo yote. Tanzania imara ni faida kwa kila Mtanzania.