PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 1,059
- 1,133
Baada ya Mama Kuupiga mwingi kwa Mwaka huu kwa kumwaga Maelfu ya ajira kwenye sekta za Huduma hasa Afya na Elimu kupitia utumishi ameendelea kuupiga mwingi kwa kupandisha madaraja na Vyeo Maelfu ya Watumishi.
Kama alivyosema Mama Nyumba ulioizoea kuihama Tabu sasa ameshindwa kuiacha adhma yake ya Ajira kwa Vijana na ni majuzi tu kupitia Maelekezo yake kama Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama tumeona kwa namna ambavyo vikosi vyetu vya Majeshi vimemwaga ajira ikiwemo Jeshi la Polisi Maelfu ajira zilitolewa, Jeshi la Magereza, Jeshi ya Zimamoto na Uokoaji na haikuishia hapo tu na Jeshi la Uhamiaji wakaona isiwe Tabu nao wakamwaga Ajira.
Tukasema Sasa Mhe Rais amepumzika kidogo kumbe usilolijua ni Sawa na Usiku wa Giza ni wiki hii ambapo Tunaona Chifu Hangaya na Mpira wake amehamia Kwenye Mashirika ya Umma ambapo ipo kama ifuatavyo.
Shirika la TANESCO walitoa Ajira
Taasisi ya kupambana na Rushwa (TAKUKURU )wamemwaga Ajira 350 bado sijatafakari kidogo
Juzi tena Sekretarieti ya Ajira ( Public Service Recruitement Secretariet ) kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamwaga Ajira 1097 katika fani mbalimbali za Utaalamu na haya ni machache tu kati ya Mashirika Mengi yaliyofanya hivi .
Mimi nikadhani labda fursa wanapata tu sekta Rasmi au kupitia kuajiriwa moja kwa moja kumbe hata sisi wajasiriamali vijana nasi fursa zinatufuata huku tulipo na ni juzi tu kwenye ziara ya Chifu Hangaya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan tuliona akikabidhi zaidi ya Milioni 300 kwa vikundi mbalimbali kwa vijana ,wanawake na wenye ulemavu katika Jiji la Arusha kama Mtaji wa kuwawezesha kujiajiri katika sekta na fursa Mbalimbali lakini pia kuwaongezea uwezo kwa kile walichaonzisha .
Kwa hakika Chifu Hangaya na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan hajaishia tu kwenye Uendelezwaji wa Miradi mikubwa ya kimkakati,uboreshwaji wa Huduma na miundombinu bali pia na Upatikanaji wa Ajira na mazingira bora ya Ajira kwa watanzania hasa vijana.
Kazi Iendelee
#TwendePamoja