Rais Samia anatarajiwa kuzindua daraja la Magufuli, Kigongo - Busisi Juni 19 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua daraja la Kigongo- Busisi (KM 3) juu ya Maji linalounganisha wilaya za Misungwi na Sengerema ifikapo tarehe 19 Juni, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa na Abdallah Ulega (MB) Waziri wa Ujenzi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika katikati ya daraja hilo alipokua akielezea kazi zilizotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi imefanikiwa sana kwenye ujenzi wa madaraja, barabara, vivuko na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii pamoja na kukuza uchumi wa watanzania.

Ulega amesema pamoja na kukamilika kwa daraja hilo lililogharimu Bilioni 716, serikali ya awamu ya sita imejenga madaraja mengine mengi kama Tanzanite (KM 1) juu ya bahari, Wami (Mita 510), Kitengule (140 Mita), Msingi- Singida (Mita 100).

Amesema, daraja la Kigongo Busisi limejengwa na kampuni ya CCECC kwa kushirikiana na wataalamu wazawa ambao ni wabobevu kwenye kazi hizo na kwamba nchi za jirani wajiandae kwa neema ya barabara hiyo.

Aidha, amebainisha kuwa daraja hilo lina uwezo wa kupitisha magari zaidi ya elfu 20 kwa siku na kwa dakika 3 hadi 5 tu gari itakua imeshavuka kutoka upande mmoja na mwingine.

Vilevile, amefafanua kuwa kwa umahiri wa Rais Samia amefanisha kukamilisha daraja hilo ambalo wakati anaingia madarakani lilikua limejengwa kwa asilimia 25 tu lakini serikali yake imekamilisha asilimia 75 zilizobaki kwa kulipa zaidi ya Bilioni 500.

Vilevile Waziri Ulega amebainisha uwezo wa daraja hilo kuwa lina uwezo wa kubeba gari zenye uzito usiozidi tani 160 kwa wakati mmoja sawa na magari manne yenye tani zaidi ya 45 na amewataka wananchi kulinda rasilimali za daraja hilo na miundombinu mingine kwa manufaa ya watanzania wote.

Sambamba na madaraja amefafanua kuwa mtandao wa barabara umeongezeka kutoka Kilomita elfu 36 hadi 37. 4 kutokana na kupandishwa kwa hadhi ya barabara kutoka wilaya kwenda kuwa za mikoa huku akizitaja barabara za Mbambabay (KM 66), Kigoma-Kasulu (KM) 100
SnapInsta.to_503623095_18061615580236473_5866321691814212947_n.jpg

SnapInsta.to_504445807_18061615571236473_7079848793364820343_n.jpg
 
Hiyo miradi ni ya Magufuri ajenge ya kwake nayeye

Juzi niliona msigwa kapost tren ya mzigo ya mwendokas

Kwenye comment kila mtu akawa anachangia anamwambia hiyo ya Magufuri
Tatizo hamfikiri vizuri,maza angeitelekeza ingekamilika?..hiyo sgr huyo Mungu wenu aliiacha 30%,hilo daraja liliachwa %ngapi?
 
Ni kupoteza muda daraja lilishaanza kazi na watu wanaendelea angeweza kwenda waziri wa ujenzi tu.

Majizi yanatengeneza mianya ya kupiga pesa kwa matukio kupitia per diem

Maaana hapo watasafirishwa wakuu wa mikoa jirani.

Wakuu wa wilaya jirani na wilaya ya mkoa husika

RPC wa mkoa husika na mikoa jirani .

Waziri wa ujenzi na wafanyakazi toka wizara ya ujenzi .

Watumishi wengine toka mashirika ya serikali .

Wakuu wa uhamiaji, magereza , usalama wa taifa , zimamoto n.k

Vidampa, kunguni , chawa na wapambe kutoka mikoani kujazia idadi kama kina Lucas Mwashambwa , hawa hulipwa pia posho ingawa wengi hata hawajui waliochoitiwa zaidi ya kujaza idadi na kusifu hata wanachosifia hawakijui.

Hiyo ni chain ndogo tu ya ufujaji wa pesa za umma.
 
Wivu tu ndio unaokusumbua
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Ukweli haujifichi!
Mama apewe tu Maua yake!

Kazi kubwa imefanyika!

Kubwa sanaaaa!
 
Sijuinkitapigwa kijembe Gani siku hiyo

Najua sa hizi Kanda ya wazi mandalizi yamepamba moto maigizo mbalimbali yameandaliwa
 
Kama mwananchi wa kawaida, kuna mengi ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hasa kutokana na mambo haya makubwa ya maendeleo. Hapa kuna baadhi ya sababu kuu ambazo mtu binafsi anaweza kusema kwa dhati:

Ninachomshukuru Mheshimiwa Rais kama Mwananchi:

1. Kwa kutujengea Daraja la Kigongo–Busisi, ambalo linaondoa adha ya kusubiri vivuko kwa muda mrefu. Sasa tunaweza kusafiri haraka kati ya Sengerema na Misungwi bila usumbufu.

2. Kwa kutuunganisha kama taifa barabara na madaraja haya si tu miundombinu, ni njia za kufungua fursa za kiuchumi, kibiashara, na kijamii. Vijana wanaweza kusafirisha bidhaa, watu wa kawaida wanaweza kufikia masoko na huduma za afya kwa urahisi zaidi.

3. Kwa ujasiri wake wa kuendeleza miradi mikubwa licha ya changamoto za kiuchumi duniani. Amethibitisha kuwa mwanamke anaweza kuwa kiongozi wa kiwango cha juu kabisa na mwenye matokeo makubwa.

4. Kwa kuweka mbele maisha ya wananchi wa kawaida kwa kutujengea barabara vijijini, madaraja ya kuunganisha wilaya, na kuongeza upatikanaji wa huduma za msingi.

5. Kwa kuongoza kwa upendo, utulivu na busara, akituhakikishia amani na mshikamano kama taifa.

KWA MOYO MKUNJUFU
"Mheshimiwa Rais, kwa niaba ya wananchi wa kawaida kama mimi, nakushukuru kwa moyo wako wa kujali watu wa chini. Umekuwa daraja la matumaini kwa taifa letu si kwa maneno, bali kwa vitendo. Tunakuombea afya njema, hekima na ulinzi wa Mungu katika
kila hatua ya uongozi wako."
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua daraja la Kigongo- Busisi (KM 3) juu ya Maji linalounganisha wilaya za Misungwi na Sengerema ifikapo tarehe 19 Juni, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa na Abdallah Ulega (MB) Waziri wa Ujenzi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika katikati ya daraja hilo alipokua akielezea kazi zilizotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi imefanikiwa sana kwenye ujenzi wa madaraja, barabara, vivuko na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii pamoja na kukuza uchumi wa watanzania.

Ulega amesema pamoja na kukamilika kwa daraja hilo lililogharimu Bilioni 716, serikali ya awamu ya sita imejenga madaraja mengine mengi kama Tanzanite (KM 1) juu ya bahari, Wami (Mita 510), Kitengule (140 Mita), Msingi- Singida (Mita 100).

Amesema, daraja la Kigongo Busisi limejengwa na kampuni ya CCECC kwa kushirikiana na wataalamu wazawa ambao ni wabobevu kwenye kazi hizo na kwamba nchi za jirani wajiandae kwa neema ya barabara hiyo.

Aidha, amebainisha kuwa daraja hilo lina uwezo wa kupitisha magari zaidi ya elfu 20 kwa siku na kwa dakika 3 hadi 5 tu gari itakua imeshavuka kutoka upande mmoja na mwingine.

Vilevile, amefafanua kuwa kwa umahiri wa Rais Samia amefanisha kukamilisha daraja hilo ambalo wakati anaingia madarakani lilikua limejengwa kwa asilimia 25 tu lakini serikali yake imekamilisha asilimia 75 zilizobaki kwa kulipa zaidi ya Bilioni 500.

Vilevile Waziri Ulega amebainisha uwezo wa daraja hilo kuwa lina uwezo wa kubeba gari zenye uzito usiozidi tani 160 kwa wakati mmoja sawa na magari manne yenye tani zaidi ya 45 na amewataka wananchi kulinda rasilimali za daraja hilo na miundombinu mingine kwa manufaa ya watanzania wote.

Sambamba na madaraja amefafanua kuwa mtandao wa barabara umeongezeka kutoka Kilomita elfu 36 hadi 37. 4 kutokana na kupandishwa kwa hadhi ya barabara kutoka wilaya kwenda kuwa za mikoa huku akizitaja barabara za Mbambabay (KM 66), Kigoma-Kasulu (KM) 100
View attachment 3360818
View attachment 3360820
Binafsi ni mmoja wa watu waliokuwa pro-Magufuli kindakindaki na wasiwasi wangu namba moja baada ya mama kumrithi Magufuli ilikuwa je mama ataweza kuendeleza miradi ya Magufuli?

So far naweza kusema maza na Magufuli wanatofautiana parefu sana staili zao kiuongozi lakini kuna kitu kimoja maza hajaniangusha. Miradi ya kimkakati aliyoianzisha Maguguli maza anatembea nayo vizuri sana.

Ni kwa muktadha huo nafikiri anaweza kusimama na kuwa Rais miaka mitano ijayo. Nitampigia kura.

Yes, kuna majambazi yanautamani sana urais na kuna figisu nyingi sana dhidi yake, but kwa wastani na kwa sasa maza anavumilika.
 
Back
Top Bottom