Mapito ya Safari ya Peter Mutharika kwenye taaluma na maisha ya kukazimishwa kwenda uhamishoni Tanzania
Maisha ya Awali na Elimu
Peter Mutharika alisomea sheria katika vyuo vikuu vya juu. Alipata shahada yake ya kwanza ya sheria kutoka Chuo Kikuu Cha London mwaka 1965.
Baadaye, alipata Shahada za Uzamili ya Sheria (LL.M.) na Udaktari wa Sayansi ya Sheria (JSD) kutoka Chuo Kikuu cha Yale mwaka 1966 na 1969.
Baada ya masomo ya sheria ya juu, alikuwa mkimbizi na kuishi nchini Tanzania, Arthur Peter Mutharika alipata cheti cha uwakili kitaaluma nchini Tanzania mwaka 1971.
Akiwa profesa, Mutharika alifundisha sheria katika vyuo vikuu kadhaa ulimwenguni. Hizi ni pamoja na UDSM Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Haile Selassie nchini Ethiopia, na chuo kikuu cha Rutgerscha Marekani. Pia alifundisha kwa miaka 37 katika Chuo Kikuu cha Washington huko Marekani.
Kujitosa kwenye Siasa za Malawi
Peter Mutharika alimsaidia kaka yake, Bingu wa Mutharika, wakati wa kampeni zake za kuchaguliwa tena kuwa rais mwaka 2009. Peter Mutharika kisha aliingia katika siasa za Malawi yeye mwenyewe. Alipata kuwa Waziri serikalini na aliendelea kumshauri Rais kuhusu masuala muhimu hadi kifo cha kaka yake mwaka 2012.