Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 116
- 260
Moja kati ya mambo yanayofanya uongozi wa nchi yoyote upendwe ni jitihada za wazi za kustawisha maisha ya wananchi, kutatua kero zao na kutekeleza maono yenye dhamira njema na maisha ya watu.
Rais Samia amefanya vizuri katika maeneo haya kiasi cha kuandika historia ya kipekee. Mwezi huu inatarajiwa kuwa wanafunzi wote walioshinda mitihani ya darasa la saba wataingia kidato cha kwanza kutokana na ujenzi wa vyumba vya madarasa nchi nzima.
Kwa upande wa uchumi, hadi kufikia Disemba 2021, ukubwa wa soko la hisa umeongezeka kwa karibu 4.5% kutoka Trilioni 15.4 hadi Trilioni 15.8, ikiwa ni karibu Bilioni 500. Hii imetokana na sera nzuri za uchumi zinazotekelezwa na Rais Samia Suluhu katika kuimarisha uchumi wa nchi.
Aidha, kutokana na mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini, ukusanyaji wa mapato umeongezeka kwa kasi, kwa Mwezi Disemba pekee kiasi cha Trilioni 2.51 kimekusanywa na kuandika historia ya fedha nyingi zaidi kwa mwezi tangu kuanzishwa kwa mamlaka ya mapato nchini(TRA).
Katika kipindi cha mwezi July hadi Disemba 2021, kimekusanywa kiasi cha Shilingi Trilioni 11.1, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Rekodi hii inatoa dira ya ushindi kwa wapenda maendeleo na uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
#SisiTumekubali #kaziinafanyika