Rais Samia ameanza kushtuka? Kwa wengi hakunaga kitu kinachoitwa nidhamu ya hiari

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,211
Rais Samia wakati anawaapisha viongozi mbalimbali aliowateua amesema kama kuna jambo ameligundua na linamtesa ni kwamba watumishi wengi wa umma hawajielewi na ili wawe na nidhamu ya kufanya kazi ni mpaka wapewe vitisho na kusukumwa sukumwa, bila vitisho nidhamu hakuna!

Rais amewataka viongozi wapya aliowateua wakaone ni jinsi gani ya kushughulikia tatizo hilo ili watumishi wa umma wajue wajibu na mipaka yao ya kazi.

 
Watumishi waumma sio watoto wadogo, wanaona jinsi wanasiasa wanavyotafuna mali za umma halafu wanaendelea kupeta.

Sasa hivi na wao wanatafuna tu maana sa100 aliwapa go ahedi ya kula kwa urefu.

Acha wale ilihali waribariki hili ni wanasiasa.

Kingine bila sheria kali zinazosimamiwa ipasavyo..hii nchi itaendelea kutafunwa tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sheria iwe msumeno sio inaumiza vidagaa ilihari mafisadi papa yanapeta tu kwenye serikali.

Takukuru naye kutwa kuhangaika na watumishi wa halmashauri wakati bungeni kuna mafisadi yanatafuta mali za umma hawajawahi itwa hata siku moja kuhojiwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hapo ni kutembea na mkono wa chuma tuu hakuna namna, wazungu hawakuwa wajinga kutumia mjeledi
Mwafrika kaumbwa kiajabu sana...ukitaka a-perform msimamie kwa ukali tena ukihakikisha anafuata taratibu ulizompa kwa kutoa adhabu punde anapokengeuka.

Au, kwa vile ni kiumbe kinachotaka sana kuabudu ngozi nyeupe, basi muweke chini ya mzungu, (hata kama ni mtoto)mwarabu, hata mhindi au mchina..utashangaa atakavyopiga kazi kwa matumaini ya kusifiwa na kuonekana ni bora kuliko waafrika wenzake mbele ya huyo mtu mweupe.

Hopeless kabisa!
 
Hapo ni kutembea na mkono wa chuma tuu hakuna namna, wazungu hawakuwa wajinga kutumia mjeledi
Nadhani watu wakiiona china , Uingereza, Marekani, Singapore, Korea Kusini, Japan, Russia zipo vile wanadhani zilikuwa vile kwa nidhamu ya hiari ila wangejua mabalaa waliyopitia mpaka kuwa vile wangejua Jinsi Israel inavyojengwa kwa jasho na damu. Inabidi Tanzania tupate kiongozi Kama Mao Zedong atembeze mkono wa chuma kwa washenzi ili nchi ikae kwenye mstari ulionyoofu👍
 
Sheria iwe msumeno sio inaumiza vidagaa ilihari mafisadi papa yanapeta tu kwenye serikali.

Takukuru naye kutwa kuhangaika na watumishi wa halmashauri wakati bungeni kuna mafisadi yanatafuta mali za umma hawajawahi itwa hata siku moja kuhojiwa.

#MaendeleoHayanaChama
Upo sahihi kabisa kiongozi kwa Jinsi inchi yetu ilipofikia tunahitaji sheria Kali Kama za china na tunaitaji viongozi wenye roho ngumu kupambana na mafisadi na wazembe serikalini kwa mkono wa chuma mpaka nchi ikae mstari mnyoofu alfu ndio tupate mwenye maono ya uchumi na mwenye roho ngumu Kama Deng Xiaoping ili kaa la Moto liendelee kuwaunguza wahujumu uchumi na mafisadi hii ndo Tanzania inayotakiwa kuwa kwa miaka zaidi ya 30 mfululizo kikitoka chuma kinaingia chuma ili sisi wananchi na viongozi tunyooeke kwenye mstari mnyoofu wa maendeleo 👍
 
Back
Top Bottom