Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
Rais Samia, hivi karibuni ametoa kauli nyingi nzuri na ametenda baadhi ya mambo mazuri.
Kwa kauli:
1) Ameihakikishia jamii ya kimataifa kuwa utawala wake utazingatia demokrasia na haki.
2) Amewahakikishia wawekezaji kuwa utawala wake hautapora pesa wala kuwabambikizia kesi wafanyabiashara na wawekezaji.
3) Amewahakikishia watanzania kuwa hatatumia wasiojulikana kuwapoteza wanaokosoa utawala wake.
Kwa Matendo:
1) Akaunti zilizotekwa na TRA zimeachiwa
2) Baadhi ya waliobambikiwa kesi wameachiwa
SASA NI WAKATI WA KUPIMA DHAMIRA
1) Je, Samia anayafanya haya kwasababu dhamira yake inamtaka ayafanye haya kwa kuwa anaamini kwa dhati kuwa Taifa letu linatakiwa kuwa lenye utawala wa kidemokrasia, haki, na linaloheshimu tawala wa sglheria, AU mazingira yamemlazimisha kufanya hivyo lakini siyo kilichopo katika dhamira yake?
YANAYOKINZANA NA KAULI ZAKE
1) Kinyume cha matakwa ya katiba, amezuia mikutano ya vyama vya upinzani akiruhusu ya chama chake CCM kufanya mikutano ya ndani na ya wazi.
2) Kinyume cha haki za kikatiba za watu kukusanyika, kwa maelezo ya RPC wa Mwanza, amezui kongamano la katiba ambalo lilikuwa mkutano wa ndani.
2) Kinyume cha katiba, inayomtaka kumtendea haki kila mtu bila ya kujali imani yake, kabila au dini, serikali yake imewakamata watu wanaosadikiwa ni wanachama wa CHADEMA , au walitaka kushiriki kongamano la katiba, watu 128, tena wengine wakiwa hotelini, na wamefungiwa mahabusu, bila kosa lolote.
3) Kinyume na kauli yake ya kuheshimu katiba na haki za msingi za demokrasia, hajazungumzia chochote wala kufanya chochote kuhusiana na bunge batili lililoundwa na Serikali, wala hajazungumzia juu ya uchaguzi batili wa 2020 ambao yeye na bunge ni zao lake, na wala hajazungumzia chochote wala kufanya lolote ili chaguzi zitakazofuata ziwe huru na za haki tofauti na alichofanya mtangulizi wake.
HAYA YANATOA TAHADHARI KUBWA KWA:
1) Wawekezaji : Je, waziamini kauli za Rais kwa 100% wajati tayari kuna mambo aliyoahidi kwa kauli kuyafanya, lakini anatenda kinyume?
2) Jamii ya kimataifa: Je, iamini kauli zake kwa 100% wakati abayoyatenda ni kinyume chake?
3) Watanzania: Je, tumwamini Rais ataishi na kutembea kwenye kauli zake nzuri alizozitoa kwa 100%?
4) Vyama vya upinzani: Je, viamini kuwa sasa imeingia serikali mpya itakayotenda kwa kadiri ya katiba?
Kwa Mtazamo wangu, kila kundi linatakiwa kwenda kwa tahadhari kubwa badala ya kuingiza miguu yote miwili kwa kuamini tu kauli, na huku kuna viashiria vya wazi kuwa kinachotamkwa mdomoni, na utekelezaji wake, ni tofauti.
Kwa wawekezaji, kama ghafla serikali inaweza kuingiza kodi mpya ambayo ni zaidi ya 100% ya pato la mtoa huduma, itashindwa vipi kufanya hivyo hivyo kwa kodi nyingine?
Kwa vyama vya upinzani, kama watu wanakamatwa mahotelini kwa vile tu inafahamika walienda kwa kongamano la katiba, itashindikana vipi mpinzani yeyote kukamatwa wakati wowote akiwa mahali popote?
Kwa jamii ya kimataifa, kama watu wanaweza kukamatwa na kuswekwa ndani bila hata ya hatia yoyote, itashindikana vipi utawala huu kutenda mengine ambayo pengine yatakuwa mabaya zaidi?
Kwa watanzania, kama tuliambiwa utawala utaheshimu haki za makundi yote, lakini siku chache serikali hiyo hiyo inatudondoshea kodi ya kiwango cha zaidi ya 100% kwenye miamala bila ya kujali maoni ya wadau, tuna uhakika gani hatutaendelea kupuuzwa hata katika haki nyingine?
WITO: KATIKA NCHI HII KUAMINI KUWA SERIKALI INAKUPIGANIA ILI UISHI, UPATE MAENDELEO NA FURAHA, NI KUJIDANGANYA. HAYA YATAWEZEKANA TU ENDAPO WANANCHI SIKU MOJA TUTATAMKA KWA UMOJA WETU KUWA SASA IMETOSHA. TUKIENDELEA KUENDEKEZA SIASA ZA uCCM NA uCHADEMA, siku zote watawala wataendelea kuwa vichwa, na wananchi kuwa miia.