Rais Samia aachane na utopolo ataaibika pasipo sababu

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,293
3,965
Nimesikia watu wanaojiita wazee wa yanga kuwa eti wanataka kwenda kwa mh Rais Samia kulalamikia hukumu ya Haji Manara kwa makosa aliyofanya yasiyo ya kimaadili.

Kwanza nitoe masikitiko yangu makubwa kwa kampuni inayofadhili huu upuuzi ambapo pamoja na project nyingine chafu,kulikuwa na project ya kumshambulia mwekezaji wa Simba Mo kwa matusi yaliyomdhalilisha yeye binafsi ingawa hakuwahi kujibu.

Pili niombe Rais wangu asikubali huu utoto kuingizwa katika mtego wa mambo ya kijinga kwa manufaa ya watu wachache tu wasio na nia njema kwa soka letu.

Rais naweza kusema tu una masuala mengi muhimu kuyafanyia kazi na si huu utopolo wa akina Manara.

Hao wazee waelimishwe tu kuwa serikali haiwezi kuingilia Uhuru wa TFF kwa kuwa ni kinyume na kanuni za FIFA na kwamba ipo hatari ya nchi kufungiwa iwapo Rais ataingilia hukumu hii
 
Mpira wa bongo ni vituko vitupu, Timu zetu haswa Yanga wanapotia mguu kimataifa na kufungwa na kutolewa nje ya michuano mechi ya pili tu, hakuna anayepiga kelele.

Kumbe hayo matokeo ndio ya kutuumiza sisi kuliko hizi siasa za Haji Manara na uhuni mzima uliopo mpirani TZ,

Elimu ni kitu muhimu sana, na hapa ni rahisi kukubaliana na Mzee Lowassa alivyoongea pale Jangwani 2015, Wanachotaka kufanya wazee ni mambo ya kipuuzi tu ya kila siku ya kitanzania.
 
Nimesikia watu wanaojiita wazee wa yanga kuwa eti wanataka kwenda kwa mh Rais Samia kulalamikia hukumu ya Haji Manara kwa makosa aliyofanya yasiyo ya kimaadili.

Kwanza nitoe masikitiko yangu makubwa kwa kampuni inayofadhili huu upuuzi ambapo pamoja na project nyingine chafu,kulikuwa na project ya kumshambulia mwekezaji wa Simba Mo kwa matusi yaliyomdhalilisha yeye binafsi ingawa hakuwahi kujibu.

Pili niombe Rais wangu asikubali huu utoto kuingizwa katika mtego wa mambo ya kijinga kwa manufaa ya watu wachache tu wasio na nia njema kwa soka letu.

Rais naweza kusema tu una masuala mengi muhimu kuyafanyia kazi na si huu utopolo wa akina Manara.

Hao wazee waelimishwe tu kuwa serikali haiwezi kuingilia Uhuru wa TFF kwa kuwa ni kinyume na kanuni za FIFA na kwamba ipo hatari ya nchi kufungiwa iwapo Rais ataingilia hukumu hii

Ndiyo maana nchi hii haitapiga hatua milele kwenye soka! Kama mambo ndiyo haya ya ujinga ndiyo yanaenda kwa Rais kwa vile tu ni shabiki wa Yanga basi wanadhani atawasimamia, badi tutegemee soka letu litaelekea shimoni kaa kweli endapo na huyo Rais atawasikiliza ujinga wao!
 
Back
Top Bottom