mgeni wenu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 3,664
- 1,730
Mkuu wangu wa nchi,pengine nia yako ni kuhakikisha nchi yetu inarudi kwenye nidhamu ndo maana unatumbua majipu(msemo ulio ubatiza jina wewe)japo sijawa na uhakika kama ni kupanga safu yako ya watu wako au chama au ni visasi kama wachache wanavyoamini.
Bado katika jeshi la polisi hasa mikoani na wilayani wapo wakuu wa vitengo wenye vyeo vya kati na vikubwa kwenye wilaya zao,sio tu miungu watu bali wanashirikiana na wahalifu kwa miaka mingi na kulepekea jeshi la polisi kuchukiwa na raia,pia kuifanya kazi ya askari hao kuonekana ina viwango vya chini sana kiutendaji.
Mfano ni Kanda ya Ziwa mkoa ambao muasisi wa chama chako anatoka,hali si shwari, najua idara za usalama zimefikisha majalada ya uchunguzi kwako,kwani magendo,uvamizi,wizi,ujambazi,uonevu na mauaji yatokana na baadhi ya wakuu wa vitengo kuwa mbele katika kuhakikisha uhalifu unaongeza kipato kwa askari wachache wenye tamaa .
Wananchi wanasubiri kwa hamu kuona majipu haya yanatumbuliwa haraka sana,hakuna haja yabkuuma uma maneno ila pitia majalada ya uchunguzi na angalia hatua hatua zilizochhukuliwa na walio juu yao ndo utajua kuna genge kubwa la uhalifu ndani ya jeshi la polisi.
Najua umekuwa msomaji mkubwa sana wa Jamiiforums na hasa pale nilipokudokeza kuhusu mafuta na wizi uliofanyika bandari haikupita wiki mbili tukaona matoke ya hatua.
bBsi usingoje Waziri wako aangalie haya maana wanadanganywa kwa kuwa majalada ya matukio ya watu wa aina ya majipu yapo kwako nategemea kama sio wakubwa wao kuchukuwa hatua au kuachia nafasi zao kwa kuwa nia wenzao basi utawatumbua haraka ili jeshi lirudishe heshima na malengo yake yatimie kama ilivyokusudiwa,tunashukuru sana kwa vingamuzi mlivyowapa askari wa usalama barabarani ila bado rushwa iko pale pale.
Uuzaji na ukodishaji wa silaha kwenye matukio ni wa kawaida kwa mikoa ya kanda ya ziwa na kupindisha doria ili wizi ufanyike limegeuka kuwa jukumu la polisi pia.
Tutapoteza askari wengi waaminifu kwa tamaa za wachache, angalau watatu tu kwenye hili wawe mfano ili wengine wajifunze,fautilia pia milipuko iliyokuwa inatokea kwenye mikutano ya kisiasa na uwabaini wapangaji wa mikakti hiyo maana raia waanajua japo hujaambiwa ukweli ili nia yako njema isitiliwe mashaka maana wapinzani wako bado wanaamnini ni visasi au kupanga safu.
Tutaongea mengi zaidi baada ya kulifanya na hili kama ulivyofanya kwenye mafuta na makontena.
Wiki ijayo nitakuja na mahala pengine panapovuja ili usizibe tundu, mgosi mgeni wenu toka Lushoto.