Rais rudi huko uliko bungeni kumechemka

Rais rudi huko uliko bungeni kumechemka

Welu

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
852
Reaction score
303
Kama kuna mtu ana namba ya simu ya mkuu wetu huko aliko ampigie simu arudi maana hali inayoendelea bungeni yamtaka mzee awepo. Mawaziri wake baadhi wameambia ni wezi sasa kama ni kweli kuna sababu ya wao kuendelea kuwa wabunge na uwaziri? Je Filikunjombe anamaanisha rais aliteua wezi wamsaidie nini?
 
Hii kauli ya Filikunjombe ina tafsiri nyingi sana kwa serikali ya JK.
 
Hakuna haja ya kumpigia mwacheni abembee wakati huku wabunge wake wakinyukana,acha wapige kura ya kutokuwa na imani na serikali yake akirudi akute kibarua kishaota nyasi
 
Basi akirudi atapewa ujumbe wake, Lakini ameshawavumilia sana anatakiwa atoe maamuzi magumu sasa.
 
Abaki uko uko moja moja kesho serikali inavunjwa na October uchaguzi.
 
Kama yupo SAO Paulo kwa sasa ni 08:44:00 BRT atakuwa anakunywa chai
 
Kama kuna mtu ana namba ya simu ya mkuu wetu huko aliko ampigie simu arudi maana hali inayoendelea bungeni yamtaka mzee awepo. Mawaziri wake baadhi wameambia ni wezi sasa kama ni kweli kuna sababu ya wao kuendelea kuwa wabunge na uwaziri? Je Filikunjombe anamaanisha rais aliteua wezi wamsaidie nini?

Mpigie Maximo.........wako nae
 
Angekuwa ni Rais wa West Africa........... naona angesha rudi haraka sana!! Hapa anajua akina Shimbo wameridhika!!! Huoni hata mazishi ya wastaafu wa jeshi hana time nayo!!
 
Kuna mshikaji wangu ananiambia hapa kwamba Jakaya kaomba appointment ya kukutana na Rais wa SENEGAL, mambo yakiwa poa, akitoka Malawi anaunganisha SENEGAL, Kwa kifupi ni kwamba hawezi kurudi mpaka Bunge liishe.
 
Mpigie Maximo.........wako nae

Kikwete-salutes-Maximo.jpg
 
Mukulu alishajichokea hana habari tena na Taifa hili hata angelikuwepo asingekuwa na jipya.
 
Wabunge wa ccm wameingia kwenye kikao cha chama,jioni utasikia kauli ya kuwaomba msamaha mawaziri.

Mh rais nimemwona kwenye shamba la nyanya.
 
Back
Top Bottom