Rais Rodrigo Duterte na vita ya dawa za kulevya Ufilipino

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
16640789_1140887476020668_3984545302424772931_n.jpg

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la umoja wa mataifa kuhusu madawa ya kulevya ya mwaka 2011 (UN drug report) taifa la Ufilipino ndilo taifa ambalo limeathirika zaidi na madawa ya kulevya yajulikanayo kama 'Methamphetamine' au shabu kama yajulikanavyo katika mitaa, huko kaskazini mwa Asia, huku waathirika au watumiaji wengi zaidi wakiwa ni watu wenye umri kati ya miaka 16 hadi 64. Ukiacha nchi kama Mexico, Afganistani, Marekani, Irani na Brazil n.k ambayo ndiyo mataifa yanayoongoza kwa biashara ya madawa ya kulevya, Ufilipino nayo haiko nyuma sana katika biashara hiyo.

Takribani watu milioni 1.8 walikuwa waathirika wa madawa hayo mwaka 2015, kwa mujibu wa Philippines Dangerous Drugs Board (PDDB) huku idadi hiyo ikiongezeka kufikia milioni 3 katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu iliyopita kwa mujibu wa taarifa ya Philippines Drugs Enforcement Agency (PDEA). Katika harakati zake za kuwania nafasi ya urais hapo mwaka jana, Rodrigo Duterte aliahidi raia wa Ufilipino kuwa atamaliza matukio ya kihalifu pamoja na kuwaua maelfu ya watumiaji na waendeshaji wa biashara ya dawa za kulevya katika kipindi cha miezi sita.

Katika uchaguzi huo Duterte ambaye alishawahi kuwa meya wa Davao city kwa kipindi kirefu, aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Mar Roxas. Tarehe, 30 Juni 2016 baraza la congress lilimuidhinisha kama rais mteule na hatimaye kuapishwa kama rais wa kumi na sita wa Ufilipino. Katika hotuba yake wakati wa kuapishwa Duterte alisema kuwa atahakikisha kuwa polisi wanatekeleza sera ya "Shoot to kill" dhidi ya watuhumiwa na watumiaji au waathirika wa madawa ya kulevya huku akisisitiza raia washiriki katika kufanikisha suala hilo.

Duterte ambaye anaaminika kuwa ni kiongozi mwenye misimamo imara na itikadi kali amekuwa akipingwa vikali na mashirika mbalalimbali kama, shirika la haki za binadamu (Human Right Watch) Amnesty International na Umoja wa mataifa (United Nations) kuhusiana na mauaji yanayoendelea katika vita dhidi ya wahusika wa dawa za kulevya ijulikanayo kama, Vita ya damu yani Drug Blood War.

Kufikia Julai 3, 2016, Kupitia jeshi la polisi la Ufilipino, Philippine National Police (PNP) chini ya utawala wa Duterte, waathirika wa madawa ya kulevya (drug addicts) 30 walikua wamesha uawa, huku baadae tarehe 30 PNP wakitoa taarifa kuwa takribani watu 103 waliuawa katika kipindi cha kuanzia mwezi Mei hadi Julai ambapo inahusija watoto wa mitaani, wahalifu, watumiaji wa dawa za kulevya na huku ikisadikika kuwa mauaji hayo yametekelezwa na Davao Death Squad, na Vigalante groups ambayo makundi hayo yamekuwa yakihusishwa na rais Duterte, huku yeye mwenyewe akipinga madai hayo.

Vita hii imekuwa ikifananishwa na hali iliyokuepo nchini humo wakati wa utawala wa dikteta Ferdinand Marcos ambapo takribani waandishi wa habari 176 waliuawa. Katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 31, Mei 2016, Duterte alisema kuwa: "Most of those killed, to be frank, have done something. You won't be killed if you don't do anything wrong." Huku ikitafsiriwa kuwa alikua akiunga mkono mauaji ya wanahabari waouvu yani (corrupt journalist) na kuendelea kusisitiza kuwa; "just because you're a journalist you are not exempted from assassination if you're a son of a bitch".

Kutokana na mauaji hayo kuongezeka kiasi cha kufikia watu 2000, Philippines Human Rights Commission, ilijiridhisha kuwa mahakama ya uhalifu ya kimataifa (ICC) ingeweza kuchunguza mauaji ya mamia yanayoendelea nchini humo, huku special reporter wa UN Bi Agnes Callamand akipinga vikali kuhusu 'Extrajudicial killings' nchini humo. Yani kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa, (execution) mauaji yanayofanywa na serikali au taasisi zake kwa mtu kama adhabu pasipo kufuata legal procedures and process au hukumu inayotolewa pasipo matwakwa ya kisheria.

Kufuatia malalamiko hayo ya umoja wa mataifa Duterte alitishia kuitoa nchi yake katika umoja huo wa UN na kusema kwamba angeanzisha ushirika na mataifa ya Afrika pamoja na China. Pamoja na kupingwa huko na taasisi pamoja na mashirika mbalimbali rais Duterte hajalegeza msimamo wake kuhusu vita hiyo. Tarehe 3 Agosti 2016 Duterte aliwahusisha Chinese Triad na Sinaloa Cartel na biashara hiyo ya dawa za kulevya Ufilipino, huku tarehe 7, Duterte akitangaza majina 150 hadharani yakihusisha wanasiasa, majudge, wanajeshi na polisi na biashara ya dawa za kulevya.
Leila De Lima senator na cheaf critic wa serikali ya Duterte ambaye pia aliongoza baraza la congress katika investigation ya extrajudicial killings, alishutumiwa na Duterte kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi (an affair) na dereva wake, Bwana Dayan ambaye ni mtu mwenye mke na watoto huku akiongeza kuwa Dayan alikua akimsaidia mwanamama huyo kuendesha biashara hiyo ya dawa za kulevya madai ambayo yaliyopingwa vikali na Leila de Lima.

Kufuatia hatua hiyo Duterte alimtaka mwanamama huyo ajiuzulu na ajinyonge mwenyewe "To Resign and hang herself" hali iliyopelekea congress kupiga kura ya kumuondoa katika uongozi baada ya senator Manny Paquiao kuleta hoja hiyo. Leila alivuliwa uongozi kwa kura zilizopigwa na baraza hilo.

Tarehe 2 mwezi Septemba, Duterte alitangaza hali ya hatari 'State of emergence' mara baada ya mlipuko wa bomu mjini Davao ambapo watu takribani 14 waliuawa. Siku iliyofuata Duterte alitangaza 'State of Lawlessness' hali inayoashiria ukiukwaji au uvunjifu wa sheria kwa mabavu na fujo huku akitoa amri kwa vikosi vya usalama vya AFP na PNP kuhakikisha vinamaliza na kutokomeza vitendo hivyo huko Mindanao. Kufikia tarehe 5 septemba mwaka 2016 watu 2400 walikua wameuawa. Huku Duterte akisema kuwa wengi zaidi watauawa "Plenty will be killed"

Mauaji yaliendelea kutekelezwa huku watu maarufu ambao walikuwa katika list ya Duterte wakiwa walengwa wakubwa. Muigizaji Marton Fernandezi alimpoteza dada yake Aurora Moynihan ambaye baba yake Antony Moynihan alikuwa katika list ya suspects iliyotolewa ikulu na rais Duterte. Kutokana na tension na comment za Marekani kuhusu mauaji yaliyokua yakiendelea Ufilipino, Duterte alimwita aliyekuwa rais wa Marekani, Obama kuwa ni mtoto wa kahaba. "Son of a whore". Hatua ambayo ilipelekea Obama kuifuta ziara yake ya nchino humo. Duterte alisisitiza kuwa Marekani ni wanafiki kwa kuonyesha picha za mauaji yaliyofanyika 1906 na jeshi la marekani (Bud Deyo Massacre).

Kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo zimekua zikimuhusisha Duterte na vikundi visivojulikana vinavyofanya mauaji hayo, jarida la 'Time magazine' limempachika jina la 'The punisher' rais huyo wa Ufilipino. Katika hatua nyingine mwazoni mwa mwezi Oktoba 2016, moja ya maafiasa wa polisi aliripotiwa na 'The Guardian' akitoa ushuhuda kuwa kuna vikosi maalumu vya polisi vinavyotekeleza mauaji (Special official police death squard) ya watuhumiwa na waathirika wa madawa ya kulevya, huku akisisitiza kuwa kila kikosi hubeba polisi 15 na kuwa yeye mwenyewe ameshashiriki mauaji ya watu 87. Taarifa hizo zilipuuzwa na ofisi ya rais kupitia msemaji wake kwani kulikua hamna ushahidi unaojitesheleza wa gazeti hilo.

Duterte The punisher, mara baada ya kumaliza ziara yake nchini Vietnam aliifananisha vita hiyo ya dawa za kulevya Ufilipino na mauji yaliyotekelezwa na Hitler, The holocust dhidi ya wayahudi huku akisisitiza kuwa kama Ujerumani iliwaauwa wayahudi milioni 3, basi kwa kuwa nchini kwake wahusika wa dawa za kulevya wako zaidi ya milioni tatu, haoni shida kuwauwa wote. Kwa sabau ya maneno hayo, serikali ya Ujerumani kupitia ubalozi wake ilitaka rais huyo kuomba radhi kwa matamshi yasiyokubalika, jambo ambalo lilitekelezwa na nchi hiyo.

Kutokana na hofu ya ukiukwaji na uvunjwaji wa haki za binadamu nchi ya Marekani ilisitisha kuiuzia silaha zake (Riffles) Ufilipino huku mkuu wa PNP Chief Ronald Dela Rosa akisema kuwa wanafanya utaratibu wa kupata silaha hizo toka kwa nchi ya China. Mauaji yaliendelea kufanyika huku mwezi Octoba mwaka 2016 Meya Samsodin Dimaukom pamoja na walinzi wake watano pamoja na Datu Saudi Ampatuan waliuawa huko Makilala kaskazini mwa Cotabato.
Pia katika gereza la Baybay city ambapo alikuwa akishikiliwa senator Rolando Espirosa pamoja na Albuera Leyte, Waliuawa ndani ya vyumba vyao gerezani kwa kile kilichoitwa mashambulizi kati yake na kikosi cha CIDG ndani ya gereza hilo. Espirosa ambaye alitajwa katika list ya Duterte na kuamua kujisalimisha kwa sababu za kiusalama anadaiwa kuwa alikua na silaha ndani ya gereza hivo kikosi hicho kilienda kwa ajili ya kupekua. Hata ivo mkanda wa video wa kamera za ulinzi (CCTV) uliodaiwa kurekodi tukio hilo haukuonekana, jambo ambalo liliongeza wasiwasi juu ya vita hiyo.

Katika hatua nyingine mwili wa raia na mfanyabiashara wa korea kusini Jee Ick Joo, uliokotwa eneo la campe crane mwezi Octoba, huku kukiwa na taarifa kuwa mfanyabiashara huyo pamoja na mfanyakazi wake walitekwa na maofisa wa PNP, kwa kuwa alikuwa katika suspect list na hivo baada ya kumtesa walimuua na mwili wake ukatupwa eneo hilo. Tukio hili lilizua tafrani huku serikali ya korea kusini ikimtaka Duterte Kufanya uchunguzi wa haraka na wahusika wachukuliwe hatua stahiki. Pia taasisi mbalimbali ziliomba uchunguzi ufanyike kwa haraka ili kubaini ukweli wa jambo husika.

MWISHO
Pamoja na changamoto nyingi zinazolikabili taifa hilo, Rodrigo Duterte ameelekeza nguvu zake katika Vita dhidi ya dawa za kulevya, hatua ambayo imechukuliwa kama mbinu ya kujiimarisha kisiasa dhidi ya wapinzani wake. Rais Duterte ambaye ameshawahi kusikika akisema kuwa kuwapiga wahalifu risasi ameanza siku nyingi na kudau kuwa ameshawai kuwaua wahalifu watatu kipindi akiwa Meya, ameenda mbali zaidi na kulikashifu kanisa katoliki kwa kusema kuwa ni taasisi iliyojaa unafiki mkubwa "The most hypocritical institution".

Pia rais huyo alienda mbali zaidi na kuwatukana maaskofu na viongozi wa kanisa hilo nchini humo kwa kuwaita ni wala rushwa, wahuni na wasiojali masikini. Duterte alimtolea mfano mmoja wa maaskofu hao kuwa dhambi zake na yeye zinafanana kwani wote wana wake wawili na kuwa dhambi ambayo yeye Duterte hana ni ya rushwa lakini askofu huyo anayo. “I challenge you now. I challenge the Catholic Church. You are full of shit. You all smell bad, corruption and all" hayo ndiyo maneno ya Dutetre. Hiyo ndiyo vita ya rais Rodrigo Duterte dhidi ya wahusika wa dawa za kulevya nchini Ufilipino. Huyo ndiye duterte aliyojitolea kuimaliza biashara ya madawa ya kulevya nchini kwake kwa njia yeyote inayowezekana.
Kila la kheri Duterte, kila la kheri Ufilipino.

Imeandikwa na...
Inno Deo Lumumba
 
Hakuna aliewahi kushinda hii vita ktk dunia hii. Ni vita ngumu sana
Ni vita ngumu ukitumia style ya kuwafunga wahalifu. Ukitumia style hii ya kuwanyonga ni vita rahis sana. Kila mtu anataman kuishi. Kuwanyonga wahalifu bila kuwapeleka Mahakamani kutamaliza kabisa tatizo la madawa ya kulevya.

Huu sio mpango wa mungu kuwa una nguvu za mungu so hauwez kuisha. Huu ni mpango wa shetan na utaisha tu maadam dunia imepata viongozi kawa hawa wa kipindi hiki. Nguvu ya ibilis inaenda kushindwa vibaya sana.
 
Hakuna uhalifu uitwao kwa jina lolote ambao utaondoka kabisa ulimwenguni;bali kupungua.Nafikiri nayeye atauwawa kwa mtutu.
NB:siungi mkono matumizi wala biashara ya madawa ya kulevya;wakati ule ule naona hii njia sio nzuri.
 
Hakuna uhalifu uitwao kwa jina lolote ambao utaondoka kabisa ulimwenguni;bali kupungua.Nafikiri nayeye atauwawa kwa mtutu.
NB:siungi mkono matumizi wala biashara ya madawa ya kulevya;wakati ule ule naona hii njia sio nzuri.
Njia sahihi ni ipi mkuu?
 
Hatari sana president Duterte

Ameanza hii vita aendelee nayo awafagie wote.......usibaki uchafu.

Nayeye ajiandae lazima wahalifu wa drugs wanamuundia mbinu wammalize.

Hapo inabidi awauwe kwa ukatili wa hali ya juu na kwaharaka.

Njia amechagua ni yalawama, ambao hawausiki nao watakubwa na hii gharika.

Vipi marijuana? Nayo inahesabiwa ni narcotics? Hukumu yake ni kifo hata ukipatikana na msokoto mmoja kama wa afande Sirro na bwana Makonda?
 
Jamaa hayumbishwi na yeyote yule ....nmependa msimamo wake .....kutoa roho ya binadamu mwenzako wakati hukuitengeneza wewe yaitaji roho ngumu sana
 
Back
Top Bottom