Rais Nkurunziza akishtaki kituo cha runinga cha Ufaransa

Rais Nkurunziza akishtaki kituo cha runinga cha Ufaransa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
PARIS, UFARANSA

MAHAKAMA nchini Ufaransa imeanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza dhidi Televisheni moja ya nchini Ufaransa, Mwanasheria wa Ubelgiji na Mwandishi wa Habari wa Burundi, David Gakunzi, kwa makosa ya kuikashifu nchi yake na hadhi yake.

Rais Nkurunziza anadai kuwa Televisheni hiyo ya Ufaransa miaka miwili iliyopita ilionyesha picha za video za mauaji ya kimbari kwa madai kuwa chama tawala cha Burundi ndicho kilichohusika.

Aidha, amesema kuwa picha hizo za video zilizoonyeshwa na televisheni ya Ufaransa, Channel 3, zinadai mauaji hayo ya watu wengi yalifanyika katika viunga vya makazi ya Rais Nkurunziza, jambo linalokanushwa na ambalo kwa sasa limefikishwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Rais Nkurunziza amekanusha vikali kwamba picha hizo wala si za ndani ya Burundi, bali zinavyoonekana ni kama zilichukuliwa mahali fulani katika nchi za Afrika Magharibi.

Televisheni hiyo ya Channel -3 ya Ufaransa ilizirusha picha hizo mwaka 2016, wakati wa uchaguzi mkuu wa Burundi, ulioandamana na vurugu.

Video hizo katika matangazo kupitia televisheni ya France Channel 3, zilionyesha mauaji ya watu wengi, yanayodaiwa kutekelezwa na wafuasi wa Rais Pierre Nkurunziza.

Picha hizo za video zimepewa jina la ‘Proof of acts of violence in Burundi”, ikimaanisha ‘Ushahidi wa vitendo vya machafuko ya Burundi.”

Ndani ya picha hizo pia baadhi ya watu wanaonekana wakizungumza lugha ya Kihausa, lugha ambayo haiongelewi nchini Burundi.

Mshitakiwa Bernard Maingai, ambaye ni mwanasheria, anatuhumiwa kwamba ndiye aliyepeleka video hiyo ili ichezwe katika runinga, wakati mwandishi wa habari, David Gakunzi, yeye anashitakiwa na Rais Nkurunziza kwa tuhuma za mahojiano aliyoyafanya kwenye runinga, akizungumzia picha hizo.

Serikali ya Burundi imekuwa ikipata vikwazo kutoka kwa jumuiya za kimataifa, kwa madai ya kukiuka haki za binadamu na kwamba chama tawala nchini humo kina kundi la vijana linaloitwa Imbonerakure. Hata hivyo, Serikali ya Burundi imekuwa ikipinga madai hayo.

Mtanzania
 
Dooh mabeberu wameshikwa pabaya na nkurunzinza .. hata hivyo nauona mwisho mbaya wa nkurunzinza hapo ni sawa na kusema kwamba ameishtaki serikali ya ufaransa "...... asipokuwa makini wata mng'oa kwenye kiti alicho kikalia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom