Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa dini ya Kiislamu katika Dua ya kumuombea aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Marehemu Salim Turky.
Dua hiyo imefanyika tarehe 20 Julai 2025, nyumbani kwa Marehemu Turky Mpendae, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akitoa salamu zake Rais Dkt. Mwinyi, ametoa wito kwa Watoto wema kuendelea kuwaombea dua Wazee wao waliotangulia mbele ya haki na kuwahimiza kuendelea na mwenendo mzuri.
Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amefahamisha kuwa Amani iliodumu kwa miaka mitano inapaswa kudumishwa kwani kumekuwa na faida kubwa pamoja na Amani na utulivu wa Nchi kwani bila ya Amani hakuna maendeleo yatakayopatikana.
Marehemu Salim Turky ametimiza Miaka 4 tangu alipotangulia mbele ya haki.

Attachments
-
WhatsApp Image 2025-07-20 at 16.41.17.jpeg124.6 KB · Views: 16 -
WhatsApp Image 2025-07-20 at 16.42.09.jpeg78 KB · Views: 17 -
WhatsApp Image 2025-07-20 at 16.41.22.jpeg75.9 KB · Views: 16 -
WhatsApp Image 2025-07-20 at 16.41.21 (1).jpeg87.2 KB · Views: 15 -
WhatsApp Image 2025-07-20 at 16.41.21.jpeg51.4 KB · Views: 13