tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameupiga mwingi katika sekta ya nishati ya umeme visiwani Zanzibar na kufanikisha kulipa deni la shilingi bilioni 291, ambalo Zanzibar ilikuwa ikidaiwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Gulioni, kuhusu mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la umeme Zanzibar (ZECO), Haji Muhamed Haji, amesema kwa miaka mingi Zanzibar ikidaiwa deni hilo lakini kwa sasa haina deni la umeme.
Soma pia: Deni la Taifa ni deni la Tanzania sio Zanzibar!.
Mkurugenzi huyo amesema licha ya kulipa deni hilo lakini pia serikali ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi imefanikiwa kuunganisha umeme zaidi ya vijiji 186 kati ya hivyo asilimia 33 ni vya Pemba.
Chanzo: Nipashe digital