Hii nchi ina laana si bure. Haiwezekani watu woooote wanaoamka kuzungumza wazunguuuke halafu warudi pale pale kwenye 'TOKEA ZAMANI'. Hivi ni mambo mangapi yanafanywa leo lakini hapo zamani hayakukuwepo?
1. Hapo zamani wanawake walikuwa wakikeketwa, je turudie zamani ili tusilete migogoro na wale wanaoamini kwenye ukeketaji wa wanawake?
2. Hapo zamani huduma za usafiri zilitolewa na UDA na KAMATA tu, je turudie zamani kwa kuwa daladala hazikuwepo?
3. Hapo zamani polisi hawakuwa wakifanya doria na silaha za moto mitaani, walikuwapo mgambo na virungu vyao na ukikamatwa nao unapelekwa ZONE. Je turudie zamani kwa kuwa bunduki zinaogofya?
Tuache huu ujinga wa 'tangu zamani'. Ni watu PRIMITIVE ndio huishi kwa mazoea badala ya fikra pevu zinazoendana na wakati. Hapo zamani, hakukuwa na nchi iliyokuwa na katiba. Watu wote waliishi primitive life na social conduct ilikuwa inasimamiwa na mazoea ya jamii ya watu husika.
Ongezeko la watu na scarcity ya resources ndio iliyoleta katiba miongoni mwa jamii mbali mbali. Katiba imekuja ili kuondoa mikwaruzano kama hii. Sasa linapokuja suala kama hili halafu ananyanyuka mtu mzima na akili zake na kusema 'kwani tangu zamani ilikuwa vipi' huyo mtu anakwenda mbele au anarudi nyuma? Tena mbaya kiongozi wa nchi ambaye anapaswa kuwa wa mbele kuelezea umuhimu wa utawala wa sheria, badala yake analeta MAZOEA.
Kila mtu ana imani yake na sioni sababu ya watu wa imani mojawapo kuwa na kiherehere cha kujifanya wao ndio wana haki ya kuwaamulia wengine wale kitu cha namna gani. Na kwa nini Waislam wawe wenye kuleta mitafaruku kila kukicha, kwani nchi hii ina Waislam na Wakristo tu?
Wahindu traditionally hawali NG'OMBE, je na wao waingie mitaani kupinga ng'ombe kuchinjwa?
Watanzania tutumie akili zetu. Kila kitu kina turning point. Mtoto mdogo wa kiume hulala na mama yake kwa umri fulani, lkn anapokuwa mkubwa, hilo hukoma. Je, mama mtoto akiomba nafasi zaidi kwa mtoto huyo kulala tutamwambia 'kwani siku zote alikuwa analala wapi?'
Kiherehere kiachwe. Naamini hata hiyo dini yenu imewaamuru kutokula 'mnachoita kibudu', lkn haikuwaambia muhakikishe watu wote hawali. Mimi hata sielewi haki hiyo mnaipata kwa wajibu upi.