Rais Museven kugombea tena Urais Mwakani

Rais Museven kugombea tena Urais Mwakani

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni atawania kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine wa uchaguzi unaotarajiwa mapema mwaka ujao ili kuongeza utawala wake wa takriban miongo minne, kulingana na afisa mkuu kutoka chama tawala.

Ingawa alitarajiwa kugombea tena wadhifa huo, ni uthibitisho wa kwanza kutoka kwa chama chake cha National Resistance Movement (NRM).

Uganda itafanya uchaguzi wake mkuu mwezi Januari, ambapo wapiga kura pia watawachagua wabunge.

Museveni, 80, amekuwa madarakani tangu 1986 na ni kiongozi wa nne barani Afrika aliyeongoza kwa muda mrefu zaidi. Chama tawala kimebadilisha katiba mara mbili huko nyuma ili kumruhusu kuongeza muda wa utawala wake.

Katika video iliyochapishwa Jumatatu jioni na shirika la utangazaji la UBC kwenye mtandao wa kijamii wa X, mwenyekiti wa baraza la uchaguzi la chama tawala Tanga Odoi alisema Museveni atachukua fomu Juni 28 kuwakilisha chama katika uchaguzi huo.

1750754870549.png

1750754138472.png
 
Wapi Amama Mbambazi.
Wapi Kiza Besyige.
Wapi Robert Kyagulanyi AKA Bobby Wine 🍷.

Secretarybird is coming.
 
Back
Top Bottom