Rais mstaafu Mkapa yu wapi?

Mkapa alilumiwa lakini sasa anakumbukwa. Kikwete analumiwa sana huenda nae atakumbukwa kwa maana hata Mwalimu Nyerere alilaumiwa sana lakini alikumbikwa na anakumbukwa bado. Basi naona ni vema Mkapa achukue jukumu la kumsaidia Kikwete a critique utawala uliopo aonye asaidie. Tukumuke nchi hii ni yetu sote
 
Bado tunamkumbuka sana,
katuachia meremeta, mwananchi tangold, Anaben bank, EPA, kiwira, soko holela, mikataba mibovu ya madini, kuuzwa kwa shirika la ndege (ATC) likiwa na ndege zaidi ya 15 na kurudishwa likiwa na ndege 1, kuuzwa NBC kwa bei ya chee, na mengine mengi.
Tunamkumbuka sana tu.
 
Tunasubiri muda muafaka na serikali makini pamoja na katika mpya..sidhani kama atapona maana huyu brazamen wetu aliyetuachia yeye kibano si cha kuuliza acha aendelee kutembea tu. Kuna siku hatakuwa na hiyo nafasi.
 
Yuko nyumbani kwake Lushoto kakimbia msongamano wa magari Dar.Alisema kweli mtanikumbuka, maana tangu aingie huyu nuksi Tanzania imekuwa zama za DHIKI KUU

Mkapa anatakiwa kushatkiwa kwa kuingiza nchi kwenye matatizo. Akiwa Rais na Mwenyekiti wa Chama alijua nchi inaenda wapi, alituzira na kusema tutakoma. so anastahili adhabu. sasa yupo anacheka tu.
 
Kipindi cha awamu ya tatu ya uongozi wa inchi ulinufaika sana kwani ubinafsishaji wa mashirika ya umma, migodi ya madini. nyumba za serikali pamoja na mali zingine nyingi za serikali ulifanyika kwa kasi kubwa.

Awamu ya nne imeingia madarakani na kukuta hakuna cha kuuza. Tanaweza kuona kuwa kulikuwa na nafuu ya maisha kipindi cha awamu ya tatu kwa kudhana uchumi unakuwa kumbe wazee walikuwa wanafanya liquidation. Sawa na mtoto wa tajiri mwenye manyumba , magari nk baba yake akifa yeye kazi yake kubwa itakuwa kuuza mali za baba yake na akaonekana ana pesa na maisha mazuri.

Mimi naamini hata serikali ya awamu ya tatu ingebaki madarakani mambo yangekuwa mabaya zaidi.

Serikali ya awamu ya nne hasa mkuu wa inchi ana huruma sana na wanainchi wake ila wasaidizi wake ndiyo wanamuangusha sana ndiyo maana amewaambia wajivue magamba kwani hawana mvuto mbele ya watu.

Nyoka akijivua gamba ngozi yake hounekana nadhifu kama imepakawa mafuta.

Pamoja na ubaya wao wa ndani lakini mbele ya wanainchi wasiuonyeshe ubaya huu.
 
Mkapa atakumbukwa na sisi wana CCM, siyo nyinyi Chadema.

why you don't show your seniority in this community your comments sometimes are very subjective.ones can be a member of cdm and still can appreciate role mode like Mkapa. ni mtazamo tu
 
Nitamkumbuka daima kwa kutupa University yetu sisi wenye kumwabudu Mnyazi tehe tehe tehe
 
Naomba mnijuze yu wapi mzee wa zama za ukweli na uwazi mzee wetu BENJAMINI W MKAPA?

Namkumbuka miye kwani sasa maisha ya watanzania wengi kama miye wanaishia mlo mmoja, ama kweli JK ametutenda!

Nawasilisha

Unamtaka mkapa wa nini, mliambiwa huyo unaemlalamikia si kitu nyie mkadai ana sura nzuri, na bado ikifika hadi 2016 utaanza kuelewa, endelea tu kukumbuka.
 
kuna kampuni moja ya kuchimba madini ilimpa pande la dhahabu usawa wa kichwa chake,..alipolipeleka hatujui,..nadhani atakuwa analikwangua kidogo kidogo,..unauliza kwa nini tunachukua 3% kwenye madini???rwanda walianza hivihivi..
 
Lushoto? Mwizi tu huyo Mkapa ameiba Ikulu yetu ya Lushoto halafu unasema yupo nyumbani kwake Lushoto? yupo kwenye Ikulu yetu aliyoibinafishisha shio Nyumba yake
Mkuu kwa hili hapo kwenye red sio ukweli. Ikulu ipo pale pale ilipojengwa na Wajerumani. Mkapa ananyumba yake aliyonunua kutoka kwa mgosi mmoja.
 
Kiukwel kila binadam na mapungufu yake mkapa alijitahid sana
 
Mkapa hahaaaa! Sijui Kagoda, Meremeta, Kiwira dah! Wananiboa hawa jamaa wa magamba
 
Naomba mnijuze yu wapi mzee wa zama za ukweli na uwazi mzee wetu BENJAMINI W MKAPA?

Namkumbuka miye kwani sasa maisha ya watanzania wengi kama miye wanaishia mlo mmoja, ama kweli JK ametutenda!

Nawasilisha
mnamkumbuka wa nini acheni apumzike -- si mlisema amewaibia kiwira yenu sasa yemewafika shingoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…