Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete awasili Tunis, Tunisia

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156

Raisi mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mwakilishi wa AU ili kujadili mgogoro wa Libya
.
Mwakilishi wa AU akiagana na rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kufanya mazungumzo kuhusu mgogoro wa Libya

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete awasili Tunis, Tunisia

Machi 22, 2016
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika wa Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya, amewasili jana Jijini Tunis nchini Tunisia kushiriki Mkutano wa 8 wa Nchi majirani wa Libya.

Mkutano huo umeitishwa na Serikali ya Tunisia, na ni muendelezo wa jitihada za nchi majirani kusaidia kuleta hali ya amani na usalama nchini Libya.

Rais Mstaafu Kikwete amewasili Tunis akitokea Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya.

Akiwa Jijini Tunis, Jana tarehe 22 Machi, 2016 Dkt. Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Masuala ya Maghreb, nchi za Kiarabu na Afrika, wa Algeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh, aliyemtembelea hotelini kwake.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Messaleh amempongeza Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya. Amemueleza hali ya usalama na kisiasa ya Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya namna bora ya utatuzi wa mgogoro huo, na akamhakikishia ushirikiano wa Serikali ya Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa Afrika.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete amemshukuru Waziri Abdelkader Messaleh kwa maelezo yake na ushirikiano aliomuahidi na akamueleza matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huo hasa ikizingatiwa kuwa nchi jirani na Libya na Umoja wa Afrika zitashirikiana na wadau wote kuhakikisha mgogoro huo unatatuliwa.

Rais Mstaafu Kikwete amesisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.

Katika ziara yake nchini Tunisia, mbali na kuhudhuria Mkutano wa 8 wa nchi jirani na Libya, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu Mteule na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Libya, (Presidency Council) Mheshimiwa Fayez Al-Sarraj, wadau wengine wa Libya pamoja na kutembelea Ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa Libya iliyoko jijini Tunis.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 25 Machi, 2016.

Imetolewa;
Ofisi ya Rais Mstaafu.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Tunis
22 Machi, 2016
 
Hivi hawa watu B. Mkapa na J. Kikwete wameenda huko kupeleka UNAFKI au kitu gani ?! BWM yuko Burundi na huyu JK yuko Tunis kwa kujifanya wako smart kumbe UNAFKI uliotopea. Ya Zanzibar wamejiridhisha kwenye chama chao na kuudhulumu upande wa pili

Kwa unafiki wa aina hii hatustahili kuwapatanisha wengine.
 
ifikie hatua viongozi wa nchi zingine za Afrika wakatae kusuruhishwa na viongozi wa Tanzania badala yake wawaambie wajenge demokrasia ya kweli kwenye nchi yao ya Tanzania kwanza then ndo wakasuruhishe migogoro ya nchi zingine
 
Akiwa jijini Tunis jana tarehe 22!!!! hivi leo ni tarehe ngapi?? au hii calendar niliyo nayo siku hiz inanipiga chenga!!!!
 
Ofisi ya raisi mstaafu? Aisee hivi kulikuwa na utaratibu huu kwa maraisi wastaafu au umeanzia hapa kwa Jk.
 
Hivi hawa watu B. Mkapa na J. Kikwete wameenda huko kupeleka UNAFKI au kitu gani ?! BWM yuko Burundi na huyu JK yuko Tunis kwa kujifanya wako smart kumbe UNAFKI uliotopea. Ya Zanzibar wamejiridhisha kwenye chama chao na kuudhulumu upande wa pili

Kwa unafiki wa aina hii hatustahili kuwapatanisha wengine.
Kumbuka kila nchi ina matatizo yake. Matatizo yako usiyalinganishe na ya mwenzako!!

Kumbuka marais wastaafu BWM na JK wana historia nzuri ya utatuzi wa migogoro. Machafuko ya yaliyotokea Kenya marais hawa ndio waliosuluhisha baada viongozi kadhaa kushindwa kama Katibu mkuu mstaafu Koffi Annan.....
 
K
Hivi hawa watu B. Mkapa na J. Kikwete wameenda huko kupeleka UNAFKI au kitu gani ?! BWM yuko Burundi na huyu JK yuko Tunis kwa kujifanya wako smart kumbe UNAFKI uliotopea. Ya Zanzibar wamejiridhisha kwenye chama chao na kuudhulumu upande wa pili

Kwa unafiki wa aina hii hatustahili kuwapatanisha wengine.
Kijana wacha kuamini vijineno vya kulishwa..Zanzibar uchaguzi umeisha na Raisi ni Dr.Shein...
 
Back
Top Bottom