kikurajembe Original 2015
Senior Member
- Feb 27, 2016
- 109
- 138
Wana JF
Nachukuwa nafasi hii kumpongeza Rais wetu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Mwl.Dr.John Pombe Magufuli kwa kasi yake ya ajabu na kwa muda mfupi aliyokaa madarakani,kwa maamuzi yake ya papo hapo.wengi tumegundua Tanzania ilikuwa ikimhitaji Rais wa namna hii.Aidha pia napenda kumpongeza waziri wetu mkuu Mh.Mwl.Majaliwa Kassim Majaliwa ambaye pasi na shaka amekuwa kivutio kikubwa katika utendaji wake na pia amekuwa chachu ya mafanikio na utekelezaji wa kauli mbiu ya Mh.Rais ya "hapa kazi tu" aliyoionyesha dhahiri kuwa wanaiishi kwenye utekelezaji wa shughuli zao za kitaifa.
Ama kweli kama alivyojiita tingatinga kwenye kampeni zake za kisiasa akiomba kura, sasa tunashuhudia baada ya tingatinga kupita grader lina-grade njia vizuri na watanzania tunapita njia ya mafanikio kuelekea Tanzania ya viwanda na nchi ya kipato cha kati .Yapo mapungufu lakini hilo linadhihirisha kuwa yeye ni binadamu. Mh.Tundu Antipas Lissu Mb akijibu hoja ya hati ya muungano ipo au haipo,akinukuu baadhi ya maneno kwenye kitabu cha Hayati baba wa Taifa "Tujisahihishe" alisema "mapungufu yake yanadhihirisha ubinadamu wake"
Kwa miaka mingi zaidi ya ishirini Tanzania haina balozi nchini Angola,jambo hili bado halijatolewa ufafanuzi na mamlaka husika,na wahusika wapo kimya.Kutokuwepo balozi nchini Angola kuna sababisha hali ya kimahusiano btn the two countries kuwa tata na wakati wowote kukitokea taarifa za mateso kwa baadhi ya watanzania wanao fanya biashara huko,ama wanaoishi huko kwa maana ya kutafuta "green pasture" ama wanaosoma huko ni vigumu kupata msaada na hawana pa kukimbilia.
Kwa wale wanaosafiri mara kwa mara nje,wanajua umuhimu wa ubalozi nje ya nchi.Pia inaleta shida kufahamu wanasema nini juu ya Taifa letu.Sina maana ya kujipendekeza kwa Mh Rais ili niteuliwe mimi japo ninafiti,lahasha bali hivi karibuni nilipata taarifa juu ya mtanzania Msuya aliyepiga simu nchini anayeishi huko Angola na kufanya shughuli zake za kibiashara kufikwa na hali ngumu na kuanza kukimbilia ubalozi wa Tanzania nchini Angola jambo lililomfanya autafute huku na huko bila mafanikio huku akiomba msaada kwa maafisa kadhaa wamsaidie aweze kupata mawasiliano ya huku ili angalau wawekezaji watanzania wasababishe steady floor of communication btn the two countries,wakamwambia bila ubalozi that can't be possible hakutakuwa na link nzuri
Angola is one of the SADCS countries hivyo imo katika Ushirikiano wa Jumuia ya nchi za kusini mwa Africa kwahiyo kama nchi nyingine,sio dhambi kupeleka balozi kama muwakilishi wetu na mtetezi wetu pale.
Wizi,utapeli,hasara ubalozi wa Angola:
(i)Yapo majengo ya ubalozi wetu pale ya zamani sana yamekuwa kama magofu na baadhi ya thamani zimeibiwa na wenye nchi yao kwakuwa ni kama mji uliotelekezwa. Hii ni hasara kubwa kwa nchi yetu kwakuwa yalikarabatiwa kwa gharama za fedha za walipa kodi hapa nchini.
(ii)Serikali ya Angola walitupa majengo na eneo bure kwa ajili ya matumizi ya ubalozi wetu na sehemu yetu ya kujidai na hati tunazo,lakini wapo matapeli wachache wamefanya ujanja ujanja wameyachukuwa na kuyakarabati yale majengo kwa sasa wameyapangisha wanakula kodi.kitu ambacho wamefanya bila ridhaa yetu kama serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ushauri na hatua:
Mh.Rais wapo watu ambao wanaweza kukusaidia pale Angola na wanaweza kuwa na habari zaidi ya hizi nilizonazo bila wewe kutumia pesa na kutuma our special team kuingia gharama.Yupo mtu mmoja ni mstaafu wa jeshi ambaye aliwahi kuhojiwa sijui nikituo gani cha TV ama Radio kipindi cha mashujaa wetu wa vita vya kagera.Nakumbuka huyu mtu alijitambulisha kwa jina la BR.GENERAL FRANCIS MNDOLWA.
Akihojiwa ktk maelezo yake
1.Ni askari jeshi wa kwanza kuongoza Batalian ya kijeshi yenye jumla ya askari 1,800 baada ya kuongezwa nguvu ambaye alitunza nidhamu ndani ya kikosi chake na kwa mara ya kwanza mpaka vita vya Nduli Amin inaisha na Tanzania kupata ushindi alipoteza askari 6 tu..!
2.Ni askari jeshi wa kwanza kuteuliwa mkuu wa wilaya akiwa na cheo cha meja ili kwenda mpakani kupambana na waasi wa Frelimo wakati wa vuguvugu la msumbiji na makaburu na hatimaye kupotea kwa hayati Samora Masheli wa msumbiji.
3.Ni askari jeshi wa kwanza aliyegundua kutokuwepo kwa balozi nchini Burundi na ndipo Mh.Benjamin William Mkapa aliamua kumteua yeye mwenyewe aliyegundua mapungufu hayo na kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi mwaka 2003.
Akiwa Balozi nchini Burundi alikuwa
4. Ni askari jeshi wa kwanza kwenda msituni peke yake bila hata mlinzi kama alIvyopewa masharti na waasi wa Burundi wa FNL,wakiongozwa na Mtu machachari aliyeogopewa na serikali ya Angola ikiongozwa na Rais Ndiyi Zeye na nchi za ukanda wa Africa mashariki Ndg.AGARTON RUWASA,na alipofika huko aliongoza diplomasia mpaka akamtoa huko porini na kupanda naye kwenye ndege na kumleta kwa Rais Benjamin Mkapa.
5.Hatimaye kufanyika mkutano mkubwa hapa nchini wa kuleta amani Burundi ukifanywa na nchi nne Sauth Africa,Uganda,Burundi na mwenyeji Tanzania.Na mara baada ya kikao hicho kiongozi huyo wa waasi alikubali kutoka porini,kuacha mauaji,kukabidhi silaha na kushirikiana na serikali yake kulinda amani na kuleta maendeleo ya Burundi.
Hii iliiletea sifa sana nchi yetu na pia "jirani akiwa salama na sisi tupo salama". Mabalozi wetu wengi wa leo wanafanya nini huko majuu? Je wanaweza kuja na kitu tofauti dhidi ya kazi zao za kawaida za kibalozi? na kusajili watoto shule za abroad? Wengine walikwenda kufanya biashara mpaka kuuza majengo huko ubalozini sijui hata kama kesi zao zimeisha.eg Roma
Nashauri apatikane mtu shupavu kama BR.GEN.MDOLWA.akatuwakilishe vema huko Angola,Wanao mfahamu vizuri wanaweza kuweka picha yake humu.Japo akihojiwa alikuwa akifanana sana na Hayati LEVY MWANAWASA Former President of Zambia
Mahojiano yale yalinifanya nimkumbuke mtu huyu kujua yuko wapi sasa,anafanya nini,serikali yetu inamtazamaje,je bado anayo nguvu ya kulitumikia taifa?
Tuchangie vema