Rais Magufuli, Waziri wako Charles Kitwanga hajali Maslahi na Nchi hii

AbasMzeEgyptian

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
407
312
Mheshimiwa Rais,

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi ana mamalaka makuu sana nchi hii na moja kati ya majukumu yake ni kusimamia na kuhakikisha usalama wa wa Raia na nchi kwa ujumla. Hali kadhalika waziri huyu anasimamia Idara nyeti ya Uhamiaji ambayo wiki iliyopita alibadilisha baadhi ya wakurugenzi

Lakini cha kutisha ni kuwa Waziri Charles Kitwanga alikuwa anajua fika kuwa huyu Mama Raia wa Uganda aliyepewa kazi ya Ukurugenzi mkuu NSSF:

1. Sio Raia wa Tanzania

2. Hakuwahi kuwa Raia wa Tanzania

3. Hajawahi kuwa Raia wa Tanzania

4. Hajaomba Uraia wa Tanzania

5. Hataki Uraia wa Tanzania

Lakini pamoja na yooote hayo Waziri wako wa mambo ya ndani ambaye anasimamia na Uhamiaji aliamua kwa makusudi na bila kuzingatia maslahi na usalama wa nchi kumpitisha huyu mama Mganda kuchukua kazi ya Ukurugenzi Mkuu wa NSSF

Mhehsimiwa Rais nikukumbe tuu kuwa Waziri Charles Kitwanga ni mbia wa kibiashara (BUSINESS PARTNER) wa mkurugenzi wa uendeshaji wa NSSF ndugu Crescentious Magori hivyo sitoshangaa sana kuona kuwa Kitwanga alipata baraka zote za Magori kwenye hili jambo bila kuzingatia maslahi ya nchi bali wao waliamua kutazama maslahi yao binafsi.

Mheshimiwa Rais, hivi kweli waziri Kitwanga kwenye hili ana masalahi ya taifa au kaweka mbele
maslahi yake binafsi?

Ushauri naomba umwajibishe waziri Kitwanga na watu wote waliohusika kwenye kumpa kazi SSRA na mwishowe NSSF huyu mama Mganda wajiuzulu maramoja kwani hawaendani na kasi yako ambayo imelenga kumjengea Mtanzania heshima.
 
Huyo waziri hata mie naona kama atashindwa kuendana na kasi ya awamu hii.
 
Hivi ni huyu mama Mke wa Professor Wangwe? Alikuwa Lecturer Mlimani? Ila mama enzi hizo alikuwa mzuri Kama ndo yeye.
 
Wewe mtoa mada mtu yeyote mwenye akili timamu akifuatilia mada zako zote zinazo husu nssf hatakosa kuona uchungu wa dhahiri ulio nao kwa kuondolewa mpendwa wako kwenye nafasi flani na nidhahiri uli nufaika na uwepo wake ila siku zote cheo ni dhamana miaka 15 kwenye nafasi aliyo kuwapo unge mshukuru tu Mungu pamoja naye au uli takaje? kwenye thread tofauti ume wataja Jenister Mhagama,Erick Shitindi,Ombeni Sifue na sasa Charles Kitwanga,Cresentius Magori na sijui atafuata nani bado ili uzidi kuthibitisha nyongo ilivyo kupanda,Stahimili muungwana usijiweke sana wazi watu wakajua unalo simamia,Mungu akupe Faraja.
 
PICHA%2BNAMBA%2B3.jpg
 
Lakini kama ukiangalia kuna upuuzi ulifanywa hivyo utenguzi huu ni sahihi!
 
Kwa nchi za wenzetu za uwazi saga kama hii lazma mamlaka zilizohusika ziwe accountable lkn kibongo bongo ni la kawaida litapotezewa
 
Jamaa mtoa mada naona upo kwenye kampeni ya kuwachafua watu kwa maslahi ya Dr Dau...Jamani kwani NSSF Dau alikuwa anaataka kufia hapo hapo??
 
Dau alikua sultani hapo nssf?watu wengi wametumbiwa watu wametulia,
Nini kipo nyuma ya pazia?
 
Back
Top Bottom