Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Watu wanatarajiwa kupunguzwa kazi BOT, kule NIDA wameshapunguzwa. ATC na yenyewe iko njiani kuelekea kwenye zoezi hilo hilo la upunguzaji wa wafanyakazi. Rais JPM amesikika akisema kwamba ni bora achukiwe na wachache kwa faida ya wengi. Ni kauli ya uzalendo lakini uhalisia wa maisha ni kwamba watakaomchukia sio wachache, kwani hao wachache wanalo kundi kubwa la watu wanaowategemea.
Tuseme kwa mfano dada mmoja wa BOT anayesimamishwa kazi ana miliki saloon tano jijini Dar na maduka mawili ya kuuza nguo za kinamama. Maana yake ni kwamba ajira za kinadada wote wanaofanya kazi ndani ya hizo saloon na hayo maduka, zipo shakani, hapa tunaongelea familia kadhaa. Tuseme kwa mfano kaka mmoja analiyepunguzwa BOT anayo maduka yake ya kuuza nguo pale sinza, wale wauzaji wanakuwa wametangaziwa habari mbaya ya kufukuzwa kazi na kurudi mtaani. Biashara nyingi za watu wanaokumbana na punguzo la wafanyakazi wa sekta mbalimbali, zinakwenda kufa.
Matumaini ni kwamba hizi hatua za ubanaji wa matumizi zitakuja kuleta mabadiliko ya kiuchumi ndani ya miezi michache ijayo, vinginevyo kunaweza kuwepo kwa ongezeko la matapeli, waporaji na majambazi wanaotumia bodaboda na kila aina ya utafutaji riziki usiokuwa halali. Ni changamoto nzito sana kwa serikali ya awamu ya tano.