kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,428
- 13,936
Bila kuwepo kwa vyama vya upinzani vyenye nguvu mwaka 2015 nina imani kuwa Rais Magufuli asingependekezwa kuwa mgombea wa CCM katika nafasi ya urais. Hakuna mtanzania mwenye akili timamu na anayependa uwepo wa viongozi wanaowajibika kwa wananchi na taifa ambaye atatamani kuona upinzani wa vyama unadhoofika nchini, labda wale zoazoa tu wasiotafakari kwa kina.
Muumini mkuu wa vyama vya upinzani nchini alikuwa baba wa Taifa, hasa baada ya kuiangalia katiba yetu ilivyo. Kudhoofika kwa CUF kutasababisha kuimarika sana kwa vyama vingine vya upinzani nchini kwakuwa wanaojua maana na umuhimu wa uwepo wa vyama vingi vya upinzani nchini wapo na pengine wanazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Vyama vya upinzani ni kioo, nguvu na yard stick ya chama tawala katika kutimiza majukumu yake kwa wananchi na taifa. Kudhoofika kwa vyama vya upinzani kutaenda sambamba na kudhoofika kwa utoaji wa huduma za jamii pia.
Kudhoofika kwa CUF kutasababisha watanzania kukiacha chama hicho kwa wingi na kwenda kuminyana kwenye chama kingine kimoja sawa na wale waliokiacha NCCR na kwenda Chadema.
Haya ni maoni tu.